Mkurugenzi wa idara ya kimataifa ya kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai Bw. Zhou Jun hivi karibuni alisema, hadi sasa nchi 234 duniani zimethibitishwa kushiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai, na miongoni mwao nchi 45 kati ya nchi zote 48 za Asia, nchi 50 kati ya nchi zote 53 za Afrika, na nchi 16 zote za Bara la Australia zimethibitishwa kushiriki kwenye maonesho hayo. Alisema,
"Nchi nyingi za mabara ya Asia na Oceania zitashiriki kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai, ambapo nchi zote zenye uhusiano wa kibalozi na China zitashiriki kwenye maonesho hayo. Idadi ya nchi kutoka mabara hayo matatu zilizothibitishwa kushiriki kwenye maonesho hayo imeweka rekodi mpya."
Bw. Zhou Jun alisema Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai yametiliwa maanani na kuungwa mkono sana na jumuiya ya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |