• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwimbaji wa opera wa China Dai Yuqiang

    (GMT+08:00) 2009-05-01 18:30:18

    Hivi karibuni "tamasha la kimataifa la opera" limefanyika Beijing China. Mwimbaji Dai Yuqiang licha ya kuwa mwimbaji mkuu katika Opera za Turandot na Tosca bali pia ni balozi wa matangazo ya tamasha hilo.

    Mliosikia ni wimbo alioimba katika Opera ya Turandot, watu hujiuliza kwamba Da Yuqiang aliyezaliwa kijijini na kuanza kujifunza uimbaji alipokuwa na umri mkubwa wa miaka 22 anawezaje kuimba opera hiyo kwa lugha ya Kiitalia?

    Ni kweli kwamba kuimba opera kwa lugha ya Kitalia kwa Mchina si mchezo hata kidogo. Dai Yuqiang alisema,

    "Mwimbaji wa opera ambaye ni Mchina itambidi afanye juhudi mara kumi kuliko mwimbaji wa Italia, kwa sababu anatakiwa kuimba kwa lugha ya Kitalia, na hawezi kujisamehe kwa kiwango kwa sababu yeye ni Mchina, hapana, bali anatakiwa afikie kiwango sawa na mwimbaji wa Italia."

    Bw. Dai Yuqiang anapenda kuimba toka alipokuwa mtoto, lakini safari yake ya uimbaji haikuwa shwari. Mwaka 1982 alihitimu masomo yake katika shule ya ufundi na kupewa kazi katika mgodi wa makaa ya mawe katika mji wa Taiyuan wa mkoa wa Shanxi. Miaka miwili baadaye alijiunga na Kundi la Nyimbo na Ngoma la Taiyuan, na muda mfupi baadaye alipelekwa katika Chuo Kikuu cha Tamthilia cha Beijing. Baada ya miaka mitatu ya masomo katika chuo hicho alirudi tena kwenye kundi lake alilotoka, lakini kundi hilo lilikuwa haliwezi kumpatia jukwaa la opera, hivyo aliacha kazi yake akaja Beijing. Mwaka 1989 Alijiunga na Kundi la Nyimbo na Ngoma la Jeshi, na haikuchukua muda mrefu akajiunga na Chuo cha Sanaa cha Jeshi mjini Beijing.

    Mwaka 1992 alishiriki mashindano ya waimbaji yaliyoandaliwa na Kituo Kikuu cha Televisheni cha China, lakini alitolewa katika duru ya kwanza ya mchujo wa waimbaji; katika mashindano hayo ya mwaka 1994 alitolewa katika duru ya pili. Mwaka 1993 alipata fursa ya kushiriki mashindano ya waimbaji mjini Vienna, lakini bahati mbaya kutokana na uchovu wa safari alipoteza sauti.

    Mabadiliko ya safari yake ya uimbaji yalitokea mwaka 1996, kwamba alipata matokeo mazuri katika mashindano ya waimbaji vijana yaliyoandaliwa na Kituo Kikuu cha Televisheni cha China na mashindano ya kimataifa ya waimbaji wa opera yaliyofanyika Japan. Mwaka 2001 alisaini mkataba na Tibe Lud ambaye ni wakala wa waimbaji wakubwa watatu wa opera duniani, tokea hapo alianza kuibuka katika jukwaa la kimataifa la opera.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako