• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0505

    (GMT+08:00) 2009-05-08 16:07:52

    Msikilizaji wetu Gulam Haji Karimu wa sanduku la barua 504 Lindi, Tanzania ametuletea barua akianza kwa kusema, salamu sana na baada ya salamu napenda kujua hali zenu natumaini mnaendela na kazi za kila siku vizuri. Nashukuru kwa kunitumia orodha ya washindi wa chemsha Bongo-vivutio vya utalii mkoani Guangxi ya mwaka 2008 na majina ya washindi.Safari hii naona wakenya wamechangamka kati ya washindi 29, 18 ni wakenya ,Tanzania hakuna na 1 Arabuni.Inaonesha kiwango cha washiriki kutoka Tanzania kimepungua sana .Nawahimiza watanzania kushiriki sana katika chemsha bongo ili kujiletea ujuzi wa kujua nchi rafiki ya watu wa china na Tanzania.

    Mimi kwa upande wangu ni mgumu kwani wakati mwingine hakuna mawasiliano kabisa. Kutokana na hali ya hewa. Nashukuru sana japo sijashiriki mmenitumia orodha ya washindi, nikiwa kama veterani wa usikilizaji. Nakutumia kadi ya kumbukumbu ya usikilizaji wangu wa miaka 20 lakini, kama mjuavyo nilianza kusikiliza zamani kati ya mwaka 1966 na 1970.

    Asanteni sana.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Gulam Haji Karimu kwa barua yako na vilevile kuwa miongoni mwa magwiji wa usikilizaji wa CRI, sisi tunakuunga mkono na kuwashauri watanzania washiriki zaidi kwenye Chemsha bongo kwani kama hawatashiriki basi mambo mengi tu watayakosa hasa zawadi mbalimbali zinazotolewa na CRI pamoja na habari zinazoambatana na chemsha bongo hiyo..

    Msomaji wetu kwenye tovuti yetu ya mtandao wa internet Salum Kilipamwambu box 2371, Dar es salaam, Tanzania ametuletea barua pepe akisema, kwanza, nimefurahi sana kusikia na kuona makala za kiswahili na maoni ya mtanzania mwenzangu Magreth Komba kuhusu elimu ya Tanzania na China. napendekeza uhusiano kati ya Tanzania na China uendelee hasa katika nyanja ya elimu.

    Mimi pia kama mwalimu, nimefurahishwa sana na mfumo wa elimu wa watu wa china kwamba ni mzuri sana. Tatu nampongeza sana magreth, kuipata nafasi hiyo ya pekee, aitumie vema kwa manufaa yake na jamii nzima kwa ujumla. Kwani nami nikipata nafasi kama niyo nitaitumia vizuri.

    Mwisho, nawaomba wenzetu wa nchi zilizoendelea kama China ziendelee kuzisaidia nchi maskini kama Tanzania kwani mimi kama mwalimu wa hesabu na fizikia naona kuwa tuna upungufu wa maabara, vifaa vya kufundishia na kukosa mafunzo ya mara kwa mara kwa walimu ili kwenda sambamba na ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Hongera sana China.

    Mimi pia kama mwalimu nimefurahi sana kusikia habari za mtanzania mwenzetu magreth komba, kwa namna alivyoelezea vema mustakabali wa nchi ya Tanzania kielimu na ikilinganishwa na nchi ya china ambayo imeendeleaa sana.

    Napendekeza china iendelee na mpango wake mzuri wa kusaidia nchi maskini, mimi pia kama mwalimu wa masomo ya hisabati na fizikia naelewa jinsi walimu wanavyohangaika namna ya kufundisha masomo haya kwa kukosa maabara na vifaa vya kufundishia pamoja na mafunzo ya mara kwa mara kwa walimu waliopo makazini, ili waweze kwenda sambamba na ulimwengu wa sayansi na teknolojia. hongera na udumu uhusiano wa Tanzania na China.

    Mimi kama mwalimu pia nimependa namna ambapo magreth ameelezea mstakabali wa elimu kati ya tanzania na china, nimependa jinsi china inavyofanya vizuri katika elimu.

    Ahsante sana mwalimu Salum Kilipamwambu kwa maoni yako juu ya makala kuhusu mwalimu Magreth Komba kwani inaonesha jinsi gani unavyofuatilia sana masuala ya elimu, pia uhusiano wa China na Tanzania hasa katika masuala ya elimu unazidi kuimarika kwani kila mwaka China inatoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa fani mbalimbali na kama uliifuatilia ziara ya rais Hu Jintao nchini Tanzania aliyoifanya mwaka huu, aliahidi kutoa misaada zaidi ya kielimu na hata ya kiuchumi.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako