• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makala maalum kuhusu kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu tetemeko kubwa la ardhi litokee huko Wenchuan tarehe 12 Mei

    (GMT+08:00) 2009-05-12 19:16:52

    Kwa wachina, tarehe 12 Mei ni siku ya huzuni ambayo haitasahaulika daima. Tarehe 12 Mei mwaka jana, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea huko Wenchuan mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China, na kusababisha vifo vya watu 68,712, na wengine 17,921 kutojulikana walipo. Ni mwaka mmoja sasa umepita toka tetemeko hilo litokee, je hali ya mkoani Sichuan ikoje? Wasichuan hawajambo?

    Kutembea pamoja na ndege anaowafuga katika Kijiji cha Qipan cha Tarafa ya Xiang 'e ya Dujiangyan ni desturi ya kila siku ya mzee Dong Zhenji. Kijiji anachoishi mzee huyo kwa hivi sasa kinaundwa na nyumba ndogo za safu moja moja zilizoegemea mlima, kijiji hicho kinaonekana kama ni eneo la makazi la mjini nchini China. Mzee Dong alisema, anafurahia sana maisha ya hivi sasa. Alisema:

    "Sikutegemea kama ningeweza kuishi kwenye nyumba nzuri kama hii. Ingawa hali ya nyumba yangu ya zamani ni nzuri kuliko ya nyumba za wengine, lakini si nzuri kama nyumba yangu ya sasa, nyumbani kwangu sasa tunaweza kutumia maji, umeme na gesi kwa pamoja, hali hii ni nzuri kuliko nyumba yangu ya zamani iliyojengwa kwa matofali."

    Katika Kijiji cha Qipan, zamani wakazi waliishi katika nyumba zilizojengwa nao wenyewe ambazo zilitapakaa kwenye mlima. Katika tetemeko la ardhi, nyumba hizo nyingi zilibomoka, ikiwemo nyumba ya Mzee Dong. Tarehe 22 Januari mwaka huu ambapo miezi 7 tu baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, mzee Dong na wenzake wapatao zaidi ya 1500 walihamia kwenye nyumba mpya, ambao ni watu waliotangulia kuhamia kwenye nyumba mpya katika sehemu zilizokumbwa na maafa. Kijiji chao kilijengwa na serikali ya mtaa kwa kufuata mpango wa pamoja, halafu nyumba ziligawanywa kwa wakazi wa kijiji, ambapo kila mkazi anaweza kupata eneo la mita 35 za mraba kwenye nyumba. Familia ya Mzee Dong yenye watu 9 imepata seti mbili za nyumba, ambazo kila moja ina vyumba vinne na sebule moja.

    Katika tetemeko kubwa la ardhi, karibu nyumba zote za kijiji kimoja cha Qipan, na za tarafa zima ya Xiang 'e zilibomoka. Hivi sasa mji wa Chengdu unasaidia tarafa ya Xiang 'e kusanifu maeneo 16 ya vijiji kama eneo la Kijiji cha Qipan, ili wanavijiji wote waliokumbwa na maafa wahamie kwenye nyumba mpya kabla ya majira ya baridi ya mwaka huu. Kwenye tarafa ya Xiang 'e, shule moja ya sekondari na shule nyingine za msingi zote ziliharibiwa katika tetemeko kubwa la ardhi, hivi sasa kutokana na msaada wa mji wa Shanghai, ujenzi wa shule moja mpya unakaribia kukamilika.

    Kwenye sehemu ya ujenzi wa shule, wafanyakazi wapatao zaidi ya 100 wanaendelea na pilikapilika, ambao wanajenga Shule ya msingi ya Xiang'e, shule hiyo inajengwa kwa mbao, raslimali zote zilitolewa serikali ya Canada, shule hiyo itakuwa shule ya kwanza inayojengwa kwa raslimali za mbao tu nchini China.

    Ofisa anayeshughulikia miradi ya ukarabati baada ya maafa wa Idara ya elimu ya mji wa Dujiangyan mkoani Sichuan Bw. Zhang Ping alisema, ujenzi wa Shule ya Xiang'e unafuata kigezo cha juu zaidi cha kinga ya tetemeko katika ujenzi wa majengo ya raia. Alisema:

    "Ujenzi wa Shule ya Xiang'e unafuata taratibu za kimsingi za usanifu, uchunguzi wa hali ya kijiolojia, usimamizi wa ujenzi na ukaguzi wa sifa, na tutatuma vikundi kadhaa kusimamia mahsusi sifa ya ujenzi, maendeleo ya kazi na mambo mengine ya pande mbalimbali."

    Kazi ya ukarabati wa Tarafa ya Xiang'e imeonesha sehemu moja tu ya kazi ya ukarabati wa sehemu nzima iliyokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Sichuan. Serikali kuu ya China iliagiza mikoa na miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ipatayo 19, kwamba kila mkoa au mji usaidie wilaya moja ya Mkoa wa Sichuan iliyokumbwa na hali mbaya zaidi ya maafa, ili kufanya vizuri kazi ya ukarabati wa sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi. Kutokana na juhudi za pamoja, kazi ya ukarabati mkoani Sichuan inaendelea vizuri na kwa kasi, katika sehemu zilizoathiriwa vibaya na maafa kama vile Shifang, Beichuan, Wenchuan na Mianzhu, kila mahali kuna pilikapilika za ujenzi wa shule, nyumba au barabara.

    Katibu wa kamati ya chama ya Idara ya ujenzi ya Mkoa wa Sichuan Bibi Tian Liya alifahamisha kuwa, kwa nyumba zilizoharibiwa ambazo bado watu wanaweza kuishi, serikali imepanga mpango wa kuzikarabati au kuziimarisha. Na ilianzisha kazi ya kujenga upya nyumba za wakulima zipatazo zaidi ya milioni moja ambazo zilibomoka au ziko hatarini kubomoka kutokana na tetemeko la ardhi. Alisema:

    "Ili kuhakikisha sifa ya nyumba mpya na kasi ya ujenzi katika mkoa mzima wa Sichuan, tumewashirikisha wataalamu kutunga kanuni za ujenzi wa nyumba za wakulima; na tumechora ramani za aina karibu 400 za nyumba mpya zitakazojengwa kwa mujibu wa kinga ya tetemeko la ardhi kwenye maeneo, makabila na sehemu tofauti."

    Hivi sasa wakazi wa mkoa wa Sichuan waliokumbwa na maafa wapatao zaidi ya elfu 70 wamehamia kwenye nyumba mpya zilizojengwa baada ya tetemeko la ardhi, Mkoa wa Sichuan umepanga kukamilisha ujenzi wa nyumba mpya za vijiji vyote kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, na kukamilisha kazi ya ukarabati wa nyumba za wilayani na mijini kabla ya mwezi Mei mwaka kesho, ambapo watu wote waliopoteza nyumba kutokana na tetemeko la ardhi watahamia kwenye nyumba mpya.

    Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa ya China Bw. Mo Hong alisema, kazi ya kujenga upya shule kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa pia inaendelea vizuri. Alisema:

    "Hivi sasa ujenzi wa shule unafanyika kwa kasi zaidi. Mpaka sasa karibu asilimia 70 ya watoto wamehamia kwenye shule za kudumu zilizojengwa baada ya tetemeko la ardhi.

    Aidha katika mchakato wa ukarabati baada ya tetemeko la ardhi, watu si kama tu wanatafuta kasi ya ujenzi, bali pia wana matakwa ya juu zaidi juu ya mipango na sifa ya miradi ya ujenzi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako