• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshairi mzalendo Bw. Lu You na ndoa yake ya kusikitisha

    (GMT+08:00) 2009-05-14 17:06:05

     

    Bw. Lu You ni mshairi wa kabla ya miaka zaidi ya 800 iliyopita katika Enzi ya Song Kusini nchini China, na ni mshairi ambaye mashairi yake yanapatikana kwa wingi zaidi hivi leo kati ya washiri wote wa kale, Bw. Lu You aliwahi kujisifu kwa kusema ameandika "mashairi elfu kumi katika miaka 60", mashairi yanayopatikana hivi leo yanafikia zaidi ya 9,300. Mashairi yake yanatia moyo wa kizalendo, lakini ndoa yake inasikitisha.

    Bw. Lu You alizaliwa katika ukoo wa maofisa wakubwa, baba yake mdogo na ndugu zake pia walikuwa maofisa wazito. Katika mazingira hayo mazuri ya hali na mali Bw. Lu You alilelewa vizuri kielemu toka alipokuwa mtoto. Hata hivyo kwa sababu miaka yake ilikuwa ya vurugu za vita, Lu You alilazimika kuhamahama pamoja na baba yake tangu alipokuwa na umri wa miaka mitatu.

    Bw. Lu You alikuwa na tabia ya kusoma, alipokuwa shuleni alifundishwa jinsi ya kuandika makala na mashairi, maendeleo yake yalikuwa ya haraka kiasi kwamba alipokuwa na umri wa miaka 12 aliweza kuandika makala na mashairi mazuri ya ajabu. Kutokana na kuwa toka alipokuwa mtoto alilelewa kwa fikra za uzalendo siku zote akihofia hatima ya taifa lake lililokumbwa na uvamizi wa maadui. Katika mashairi yake yaliyo mengi ameonesha nia yake ya kuwafukuza wavamizi na kurudisha sehemu iliyonyakuliwa na maadui. Ili aweze kutimiza nia yake hiyo alijitosa kusoma vitabu vya mbinu za kivita na kufanya mazoezi ya kuua kwa upanga akijitayarisha kuingia kwenye medani za kivita wakati wote.

    Bw. Lu You aliandika mashairi mengi kuonesha ushupavu wake wa kuwafyeka maadui na chuki zake kwa wasaliti. Lakini wakati huo serikali ya Enzi ya Song Kusini ilikuwa dhaifu, haiwezi kumsaidia Lu You kutimiza nia yake. Bw. Lu You alikuwa na masikitiko makubwa rohoni mwake, hadi alipokufa alikuwa bado ana wasiwasi juu ya hatima ya taifa lake. Katika mashairi yake ya mwisho kabla ya kifo chake alimwambia mtoto wake aende kwenye kaburi lake amfanyie tambiko baada ya maadui kufukuzwa, Bw. Lu You aliiaga dunia akiwa na masikitiko hayo. Mashairi yake yana ushawishi mkubwa kwa vizazi vya baadaye, kila taifa la China lilipokuwa hatarini mashairi yake hutuimika na kuwa nguvu za kushajihisha wananchi dhidi ya maadui.

    Bw. Lu You ni mshairi mkubwa mwenye fikra za uzalendo, lakini ndoa yake yalisikitisha sana. Alipokuwa na umri wa miaka 20 alimwoa mpenzi wake Bi. Tang Wan. Lakini kutokana na kipaji cha bibi huyo na jinsi walivyopendana, mama mzazi wa Lu You alipinga sana ndoa yao mpaka mwishowe aliwalazimisha wanandoa hao waachane.

    Baada ya miaka kadhaa kupita, siku moja kwa bahati wapenzi hao walikutana wakati walipotembelea bustani, Bw. Lu You aliandika shairi moja kwenye ukuta ndani ya bustani hiyo akionesha uchungu wa kuachana naye. Bi. Tang Wan naye pia aliandika shairi moja akieleza msononeko mkali wa kumkumbuka, muda si mrefu baadaye Bi. Tang Wan alifariki dunia kutokana na jakamoyo. Mashairi hayo mawili yaliyoandikwa kwenye ukuta wa bustani yamekuwa ushahidi wa ndoa yao ya kusikitisha.

    Baada ya hapo Bw. Lu You alikwenda kaskazini mwa China akashiriki mapambano dhidi ya maadui. Katika miaka mingi alipokuwa akipigana vita hakuweza kujizuia asimkumbuke mpenzi wake. Alipokuwa na umri wa miaka 67 alirudi kwenye ile bustani, aliona yale mashairi yalikuwa bado yangalipo ingawa maandishi hayakuwa wazi tena baada ya miaka 40 kupita, aliposoma alilowa na machozi. Lu You alipita uzee wake huko huko alipokutana na mpenzi wake, kila aliposononeka na mapenzi yake alikuwa huandika mashairi kumkumbuka. Mapenzi kati yake na Tang Wan na mashairi yao yamekuwa hadithi nzuri katika historia ya fasihi ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako