• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matangazo

    (GMT+08:00) 2009-05-26 18:33:39
    Tangu tuanze kurusha hewani kipindi maalum cha chemsha bongo kuhusu maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Jamhuri ya watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 19 mwezi huu, tumepata majibu ya wasikilizaji kadha wa kadha wakiwemo Ngereja Mgejwa wa sanduku la posta 11409 Dar es Salaam, Tanzania na Juma Abdallah ambaye anuani yake ya barua pepe ni jabdali2004@yahoo. com, ambao wamejibu maswali na kutoa maoni machache. Tunawashukuru sana, ni matumaini yetu kuwa, wasikilizaji wetu wengi zaidi watashiriki kwenye chemsha bongo hii.

    Na mkurugenzi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar Bw. Yusuf Chunda ametuletea barua pepe tena akifahamisha kuwa, Vipindi vyetu vya Chemsha Bongo vinaruka hewani kama alivyoeleza na tayari viwili visharuka hewani. Pia amesema ameamuwa yeye mwenyewe kuwa mara vitakapomalizika vyote vinne kuruka hewani avirejee tena kuvirusha hewani kama ifuatavyo.

    1 kipindi cha Chemsha Bongo namba moja kitarushwa hewani tena tarehe 6-5-09 saa 11.30 jioni.

    2 Kipindi cha Chemsha Bongo namba mbili kitarushwa hewani tena tarehe 27-5-09 saa 10.15 jioni

    3 Kipindi cha Chemsha Bongo namba tatu kitarushwa hewani tena tarehe 30-5-09 saa10.30 jioni.

    4. Kipindi cha Chemsha Bongo namba nne kitarushwa hewani tena tarehe 1-6-09 saa 11.15 jioni.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako