• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0603

    (GMT+08:00) 2009-06-03 15:17:32

    Msikilizaji wetu Bw. Haji ambaye barua pepe yake ni Hajiwazanzibar@yahoo.com Anasema naipongeza sana CRI na pia tunataka nasi Zanzibar kuekewa mtambo ambao tutaweza kuipata kwa urahisi.

    Msikilizaji wetu Osaki Kunsha wa Tanzania anasema tunashukuru kusikia hivyo, ila hiyo redio Tanzania haipo, sijui kwa sasa kwani nimeondoka nyumbani mwaka jana, naipata kwenye internet tu, tutashukuru kama itarusha matangangazo yake Tanzania, kwa historia ya China na Tanzania ilivyo inashangaza kuona hadi sasa redio hii ya CRI ina muda mrefu na Watanzania hawaijui na lugha inayotumia ni kiswahili na nyumbani kwa kiswahili ni Tanzania. maomba hili lifikiriwe kuwa na redio hii Tanzania.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu Haji na Osaki Kunsha wa Tanzania kwa barua zenu, na hivi sasa juhudi zinaendelea kufanyika ili na wasikilizaji wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla waweze kuisikia Vyema CRI. Hivyo msiwe na wasiwasi kuhusiana na hilo.

    Mchana J. Mchana wa Salvatorian Morogoro Tanzania anasema maoni yangu ni kuhusu watangazaji, kwanza nimefurahi kumsikia mtangazaji maarufu fadhili mpunji, je amerudi tena au ni kwa muda tu. Nionavyo mimi heri abaki kwani Redio China Kimataifa ilianza kutetereka kiutangazaji sina maana waliokuwepo hawafai, la hasha, ninachokisema hapa ni uzoefu wa utangazaji. Kama ni mtangazaji huko alikotokea huyo sina matatizo naye lakini kama ni mtu amekuja kusoma na fani yake ni kilimo halafu anapewa utangazaji hii kwangu naiona kama Radio China Kimataifa inarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kwa sababu mtangazaji aliyeisomea fani hii anatumia kiswahili fasaha. Narudia lengo langu sio baya bali nikukumbushana tu.

    Ahsante sana Mchana J. Mchana kwa barua yako, na kwa taarifa yako Fadhili mpunji amerudi CRI kuendelea na kazi kama ilivyokuwa awali na kuhusu wasiwasi wako wa watangazaji hivi sasa unaweza kuuondoa kwani kweli tunakiri kwamba kipindi kile tulikuwa na upungufu wa watangazaji ndio maana tuliwaajiri wanafunzi kwa muda hata hivyo sasa wanafunzi hao wameshaondoka kwa tatizo hilo limeshatatuliwa.

    Msikilizaji wetu lydiah dola lidowllar@yahoo.com Nawapongeza nyote kwa kuanzisha idhaa hii ya kiswahili. nawaombea kila la heri! Siku njema.

    Msikilizaji wetu Aliy Abdurahim S.L.P. 2477,Zanzibar anasema ahsante sana kwa tovuti na matangazo ya kupigiwa mfano kwa redio zote za Kiswahili duniani.

    Msikilizaji wetu Hassan Kombo hssnkombo@yahoo.co.uk naye anasema Hongereni sana CRI kwa kutupatia habari zinazokwenda na wakati. Mimi ni mkereketwa wa habari na napenda sana kuzisoma. Hata hivyo baadhi ya habari mnazozichapisha ni fupi. Naomba ikiwezekana mzichapishe kwa urefu kidogo ili tupate ufafanuzi wa matukio mbali mbali.

    Msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo Kemogemba Club Box 71 Tarime anasema Nashukuru sana tena najivunia kwa Idhaa ya Kiswahili kuanzisha shindano maalumu la Chemsha Bongo juu ya miaka 45 ya uhusiano wa Kibalozi kati ya China Na Tanzania. Naahidi kuwa nitashiriki na nyuma yangu pengine wakawepo wanachama wenzangu wa KEMOGEMBA ,ili angalau kutuwezesha kukutana wasikilizaji wa kutoka pande mbali mbali.Nawatakia ushiriki mzuri wa maendeleo na ushindi wa kishindo.

    Ahsanteni sana wasikilizaji wetu kwa maoni na michango yenu mbalimbali mnayotutumia, kuhusu habari kuchapisha fupi kwa kweli mara nyingi huwa inategemea na habari yenyewe, lakini mara nyingi huwa maelezo yanayotolewa kwenye habari yanajitosheleza na kumfahamisha msikilizaji kile kilichokusudiwa, hata hivyo ushauri wako tumeupokea kwa mikono miwili.

    Barua pepe kutoka kwa Amin NAJMI amony_hi_22@yahoo.com yeye ameandika barua yake kwa kichina na anasema: Marafiki wapendwa, Siku ya Duanwu imefika, mtakula Zongzi, ninawatakia nyinyi na watu wa familia zenu kila la heri, na furaha ya siku ya Duanwu.

    Msikilizaji wetu Erick Ezekiel itserick@excite.com anasema ni kweli baiskeli ina manufaa sana kwa afya ya binadamu, mazingira na hata kwa kujenga uchumi wa mtu binafsi, hapa Tanzania kwa mfano watu wengi pia wanatumia baiskeli kama njia ya usafiri.

    lakini nataka kujua kwa kifupi historia ya baiskeli, najua wachina ni watengenezaji wa baiskeli.

    Shukrani za dhati msikilizaji wetu Erick Ezekiel kwa barua yako ni kweli baiskeli ni chombo muhimu kwa binaadamu kwani gharama zake sio kubwa na vilevile haichafui mazingira, kuhusu hustoria ya baiskeli tutakuandalia maelezo mazuri kabisa ili iwe kwa faida yako na wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako