• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0609

    (GMT+08:00) 2009-06-09 21:05:08
    Tokea tupeperushe hewani matangazo ya chemsha bongo kuhusu maadhimisho ya miaka 45 tangu Jamhuri ya watu wa China na Jamhuri ya muungano wa Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi, tumepata majibu kutoka kwa wasikilizaji wengi waliopo popote pale nchini Tanzania.

    Msikilizaji wetu Mchana J. Mchana wa sanduku la posta 1878 Salvatorian Morogoro Tanzania ametuletea majibu pamoja na maoni yake, akisema, maoni yangu kwa nia nzuri kabisa kwani kelele tunazisikia kila mara, kama halitashughuliwa kwa haraka, kizazi kinachokuja hakitaelewa undani wa urafiki kati ya China na Tanzania. Kuna swala la vifaa vinavyongizwa Tanzania kutoka China, vitu vingi havina sifa inayotakiwa na vinaumiza sana wale walio na kipato cha chini, na kinachoniumiza sana moyoni. Ninaposikia kinatoka nchi ya China, kwa mwingine haelewi siri kubwa ya vifaa hivi. Ni ujanja tu na tama za wafanyabiashara. Naamini kuwa nchi rafiki hawahusiki kabisa. Ila ni hila za wafanyabiashara wanaotaka kujitajirisha kwa njia rahisi. Naamini suala hili litafanyiwa kazi na viognozi wan chi mbili China na Tanzania, nadhani litaweza kupunguza vilio vya wasio na uwezo. Nafikiri kwa hilo kuwe na utendaji zaidi kuliko maneno.

    Tunamshukuru sana Bw. Mchana J. Mchana kwa maoni yake na kutuambia kuhusu baadhi ya bidhaa zisizo na sifa nzuri ambazo zilisafirishwa nchini Tanzania na baadhi ya wafanyabiashara binafusi wasiojali maslahi ya wateja. Serikali ya China hivi karibuni imeweka utaratibu mpya ambao bidhaa zilizouzwa kwenye soko la nchi za nje, kama zikilalamikiwa na wateja wa huko, zitaweza kurudishwa nchini China, na viwanda vilivyotengeneza bidhaa hizo vitapata adhabu na kutozwa faili

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk katika barua yake ya majibu pamoja na maoni amesema, mbali mna sekta ya elimu, nchi za China na Tanzania zinatakiwa kuimarisha kwa dharura ushirikiano katika sekta mbalimbali muhimu kwa wakati huu, kama vile uhifadhi wa mazingira, kushirikiana katika swala la mgogoro wa kiuchumi na kifedha ulioikumba dunia kwa hivi sasa pamoja na kuboresha sekta ya mawasiliano ya usafiri kama vile safari za moja kwa moja kutoka maeneo ya kibiashara kusini mwa China, mfano mjini Guangzhou au Hongkong hadi Dar es Salaam Tanzania kwa kutumia Shirika la ndege la China ama kuisaidia Tanzania katika sekta hiyo ya usafiri wa anga ili shughuli za kibiashara kwa padne mbili zididi kuimarika zaidi.

    Na anaona kuwa mustakbali wa uhusiano kati ya China na Tanzania utaimarika zaidi katika Karen hii mpya chini ya kivuli cha kufanikisha malengo ya mkutano mkuu wa ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Beijing mwaka 2006, kwani kwa maoni yangu binafsi ukurasa huu mpya uliofunguliwa katika kuboresha mahusiano ya pande mbili, umekita katika dhamira za kuendeleza mbele sekta mbalimbali za uchumi na elimu kwa mataifa yetu ya Bara la Afrika ili tuweze kujikwamua katika uchumi duni na udhaifu wa maendeleo. Bila shaka yoyote Jamhuri ya watu wa China kwa siku zijazo itaweza kutumia mafanikio na ufanisi wake wa kiuchumi na kimaendeleo ulioupat katika kipindi chote cha miaka 30 ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Pia ni jabmo la kutia moyo sana kuona kwamba kumekwua na ziara nyingi za mara kwa mara za viongozi wakuu wa China na Tanzania kutembelea na kuafikiana ushirikiano wa miradi mbalimbali ya maendeleo baina ya nchi za China na Tanzania, jambo ambalo ni dalili nzuri za mustakabali wa uhusiano wa pande hizi mbili.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako