• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtunzi mkubwa wa muziki Bw. Wu Zuqiang

    (GMT+08:00) 2009-06-15 16:59:04

    Bw. Wu Zuqiang

    Mtunzi mkubwa wa muziki wa China Bw. Wu Zuqiang mwenye umri wa miaka 82, amekuwa akiandamana katika maisha yake ya muziki, na masomo aliyopata Russia katika miaka ya 50 ya karne iliyopita yalimwekea msingi imara wa utunzi wa muziki.

    Mliosikia ni wimbo uitwao "Maji ya Mto Wanquanhe Ni Maangavu". Huu ni wimbo unaoeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya wananchi na jeshi la China ambao ni kama samaki na maji.

    Bw. Wu Zuqiang alizaliwa Beijing, baba yake alikuwa mchoraji ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa Jumba la makumbusho ya Kasri la wafalme la China. Alipokuwa na umri wa miaka 9 alivutiwa na muziki wa piano aliokuwa akipiga dada yake, baadaye naye alipiga muziki mmoja kwa piano hiyo. Jamaa zake walishangaa sana, waliona kuwa ana kipaji cha muziki, hivyo akapangiwa kufundishwa muziki. Mwaka 1947 alijiunga na Chuo Kikuu cha Muziki cha Nanjing na kusomea nadharia ya utunzi wa muziki. Baada ya kuhitimu masomo yake mwaka 1952, alikwenda Moscow kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Muziki cha Tchaikovsky. Alipokumbusha miaka mitano alipokuwa katika chuo hicho alisema,

    "Katika miaka niliyokuwa chuoni maisha ya kiutamaduni yalikuwa mazuri, na masomo yetu ya wanafunzi wa China yalitakiwa yawe mazuri kwa lazima, kwa hiyo nilijifunza mengi katika miaka hiyo. Katika miaka miwili ya mwanzo, wakati wa likizo wanafunzi wote tulikuwa haturuhusiwi kurudi nyumbani, uongozi wa chuo ulitupangia kwenda kutalii Siberia, Mto Don na maeneo mengine mengi nchini Russia. Wakati huo sisi wanafunzi wa China na wa Russia tulikuwa na uhusiano mzuri sana kwa sababu China na Urusi zilikuwa nchi rafiki. Uongozi wa chuo ulituchagulia walimu bora zaidi kutufundisha lugha ya Kirusi. Kutokana na juhudi zetu, wanafunzi wa China mara kwa mara tulisifiwa, na kwa kweli matokeo yetu ya mitihani yalikuwa mazuri."

    Bw. Wu Zuqiang alisema, yeye na wanafunzi wenzake wa Russia walikuwa marafiki wakubwa. Alikumbuka kwamba, wakati huo kitabu kimoja cha "Upatanishi wa Sauti Tofauti" kilikuwa hakipatikani madukani, lakini kilikuwa ni cha lazima kwa masomo, mwanafunzi mmoja wa Russia alimpa kitabu chake alichomaliza kukitumia katika masomo yake. Baadaye alitumia kitabu hicho kwa miaka mingi katika chuo hicho baada ya Bw. Wu Zuqiang kukitafsiri kwa Kichina. Hadi leo Bw. Wu Zuqiang bado ana mawasiliano na wanafunzi wenzake na mara nyingi anawaalika kuja kwenye Chuo Kikuu cha Muziki cha China kufanya maonesho na kutoa mihadhara. Alisema,

      "Mpaka sasa aliyekuwa mwanafunzi mwenzangu tuliyekuwa tukikaa chumba kimoja bwenini, ni kiongozi wa kwaya na ni rafiki yangu mkubwa, nilimwalika kuja China mara mbili kufanya maonesho ya muziki, kufundisha wanafunzi wangu, na mwaka huu nitamwalika tena kuja kushiriki kwenye tamasha la kimataifa la kwaya. Ingawa baadaye uhusiano kati ya nchi hizi mbili ulipita katika kipindi cha hali mbaya lakini uhusiano mzuri kati ya raia ulidumishwa vizuri siku zote, sisi ni marafiki toka mwanzo."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako