• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumba la maonesho la Hispania kuonesha mambo yake ya zamani na mambo yake ya baadaye

    (GMT+08:00) 2009-06-22 17:04:46

    Maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 yatafunguliwa tarehe 1, Mei huko Shanghai, China. Kila nchi itakayoshiriki kwenye maonesho hayo, itawaonesha watazamaji haiba ya utamaduni wake maalumu wa mijini kwa mambo yatakayooneshwa kwenye jumba lake. Leo mtasikia maelezo kuhusu jumba la Hispania linaloendelea kujengwa. Jumba hili ni jengo lenye umbo kama kikapu kilichosukwa kwa mihenzirani, kwa lengo la kuwaonesha watu mambo ya zamani na mambo ya baadaye ya Hispania.

    Jumba la Hispania lilianza kujengwa mwezi Machi mwaka huu. Mjumbe mkuu wa jumba hilo kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, ambaye ni mwenyekiti wa idara kuu ya maonesho ya kimataifa ya Hispania Bw. Javier Conde alimweleza mwandishi wetu wa habari wazo na kauli mbiu ya maonesho ya jumba la Hispania, akisema:

    "Wazo muhimu la maonesho ya kimataifa badala ya kuonesha tu maendeleo ya nchi mshiriki, sasa linabadilika kuwa la kujadili masuala yanayofuatiliwa na binadamu kwa pamoja, hususan baada ya maonesho ya kimataifa ya Seville ya mwaka 1992. Maonesho ya kimataifa yaliyofanyika katika miaka ya karibuni, kwa mfano kauli mbiu za maonesho ya kimataifa ya Hanover, Ujerumani na maonesho ya kimataifa ya Aichi, Japan zilihusu masuala ya pamoja na binadamu yakiwemo ya mazingira, binadamu kuishi katika hali ya kupatana na mazingira ya asili na maendeleo ya ujenzi wa miji. Ili kuambatana na kauli mbiu ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai ya 'Miji bora, maisha bora', tukizingatia 'miji yetu tuliyopokezana kizazi kwa kizazi', tunatumia mihenzirani ambayo ni moja ya aina za vifaa vya hifadhi ya mazingira ya kimaumbile, tunaonesha kufungamana kwa mambo ya jadi na ya kisasa. Kauli mbiu ya maonesho ya jumba la Hispania yanahusu sehemu tatu: 'kutoka dunia ya maumbile hadi miji' ikionesha kuhusu mababu wa zama za kale na zamani za awali; 'toka miji ya wazazi wetu hadi hivi sasa' ikionesha hali ya zamani na ya hivi sasa ya miji wanayoishi wazazi wetu; 'miji yetu ya hivi sasa hadi miji ya kizazi kijacho' ikionesha maisha yetu ya mijini ya kutoka sasa hadi siku za baadaye."


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako