• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0623

    (GMT+08:00) 2009-06-23 20:39:22

    Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa sanduku la posta 1067 Kahama Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema, Nidhahiri kuwa nachukua fursa hii nikitumaini kuwa wafanyakazi wote wa idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa natumanini kuwa muko wazima sana na munaendelea kutuletea matagazo yenu mulwa na nyeti kutoka hapa mjini Beijing China. Mini huku ni mzima wa afya njema, ila tu nasikitika sana kwa kutopata barua pamoja na magazeti ya China Today kwa muda kitambo kutoka kwenu. Ambapo tangu nianze kuzituma barua zangu kwa mwaka huu wa 2009 kwa makisiyo ya haraka haraka zimefikia barua kama 20 tangu Januari mpaka mwezi mei mwaka huu ambapo barua hizo zote bado sijasikia barua hata moja ikisomwa katika kipindi chetu cha sanduku la barua. Je kulikoni? Ama barua zangu zinapotelea njiani, kusema hivyo shirika la posta Tanzania hususan tawi la kahama wahusika wa posta wanaosafirisha barua wanalalamika kuwa bahasha munazotutumia kutoka hapa Beijing China, bahasha zilizokwisha lipiwa gharama ya stempu eti bahasha hizo zinahusu nchi ya China tu. Hivyo basi huenda barua zangu zote za mwezi Januari mpaka Mei mwaka huu hazisafirishwi na shirika la posta tawi langu la kahama zinabanwa tu.

    Na vilevile nilishiriki katika mashindano ya chemshabongo ya mwaka jana lakini sikusikia jina langu linasomwa. Hususan hata hivyo naomba wafanyakazi wa serikali ya watu wa China, hususa kitengo cha shirika la posta la China na shirika la posta Tanzania hususa tawi la kahama mfanye mawasiliano mwana na ili bahasha munazo tutumia kutoka hapa China ziwe zina kubaliwa na shirika la posta Tanzania. Naomba sana kwa hilo.

    Mwishowe imenilazimu nimutumie barua yangu hii kwa kutumia bahasha ya Tanzania. Mwisho naomba munitumie salamu kwa wapendwa wangu wafuatao: Ras Franz Mankongogo, Julias Dr. Ng'lja, Jofrey Njeleka, Kasimu Abed Ngeya, Mchana John Mchana, Daniel Mponeja, Wales Masanja pamoja na Kilulu Kulwa hawa wakiwa sehemu mbalimbali Tanzania. Wengine ni Joseph Milolo, Lebaca Bomboka, Lomu Apele Andeka, Robert Olinga, Mutanda Ayub Sharff, Helena Ayoma Andeka, Mbaraka Mohamed Abucheri, Xavier Telly Wambwa, Jackline Andeyo, Yaaqub Said Indambila, Jofrey Jimu Wanyama, William Makenye, Dominic Nduku Muholo, Mogire Machuki pamoja na John Makenye wote hawa wakiwa sehemu mbalimbali wa Dubai Umoja wa falme za kiarabu. Ujumbe kwa wasikilizaji wenzangu niliowataja asanteni sana kwa kunikumbuka mara kwa mara kwa salamu kwani salamu hujenga undugu na urafiki mwema. Hivyo basi ninawapongezeni sana kwa kunikumbuka nikiwa sihi wote tuendelee kukumbukana kwa salamu kupitia idhaa yetu ya kiswahili ya redio China kimataifa.

    Msikilizaji wetu Kilulu Kulwa SLP 161 Bariadi Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema, Wapendwa wafanyakazi wa idhaa ya kiswahili ya Radio China Kimataifa, tarehe 12 mwezi wa tano mwaka uliopita wa 2008 ilikuwa ni siku ya huzuni na masikitiko makubwa kwa wakazi wa mkoa wa Sichuan, wananchi wote wa China na marafiki wa China na watu wote wapendao amani na maendeleo duniani. Ambapo tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha maafa makubwa liliukumba mkoa wa Sichuan. Kama ilivyoripotiwa maelfu ya watu walipoteza maisha na wengine kupoteza makazi yao kutokana na tetemeko hilo.

    Tunapokumbuka tukio hilo la kimaumbile lililoleta maafa makubwa mwaka mmoja uliopita, kwa mara nyingine tena ninawapa pole wakaazi wa mkoani Sichuan na wananchi wote wa China kutokana na tukio hilo la kusikitisha mno. Waraka maalumu kupitia Radio China Kimatafia ili kuwafariji walioathirika kwa njia moja ama nyingine na tetemeko hilo la ardhi. Aidha katika waraka wangu huo wa mwaka jana kuhusu tukio hilo nilisema kwamba kama ningepata fursa ya kutembelea China kwa mwaliko au kwa safari yangu binafsi, hata kama itakuwa imepita miaka kadhaa hivi tangu kutokea janga hilo la tetemeko la ardhi mkoani Sichuan, nitataka kufika huko na kutoa msaada wangu mdogo na kutia saini katika kitabu cha wageni kwa mamlaka za huko. Kwani "kutoa ni moyo si utajiri" na binadamu wote ni sawa na dunia ni moja. Juhudi na mikakati mingi na ya uhakika, ikiwemo ya dharura iliyofanywa na serikali kuu ya China, serikali za mikoa na mitaa pamoja na jumuiya ya kimataifa, asasi nyingine za kiraia nchini China zimetutia moyo sana katika utoaji misaada ya hali na mali kwa wahanga wote wa tetemeko la ardhi mkoani Sichuan.

    Radio China Kimataifa ilitaarifa na kuripoti kwa kina shughuli nzima ya uokoaji, utoaji misaada na ukarabati wa miundo mbinu ilivyoendelea. Ni imani yangu kwamba baada ya miaka michache hivi kupita, maisha ya wakazi wa mkoani Sichuan nchini China yatarejea katika hali ya kawaida na kuendelea na mchakato wa ujenzi wa taifa lao la China. Mwisho kabisa natoa shukrani nyingi kwa Radio China Kimataifa kwa ajili ya mfululizo wa vipindi kuhusu kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani Sichuan mlivyotutangazia mwezi Mei mwaka huu wa 2009. Asante sana.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako