Chuo Kikuu cha Udaktari cha Xinjiang kilichoko sehemu ya katikati mjini Urumqi kina wanafunzi zaidi ya 13,000, na nusu ya wanafunzi hao wanatoka makabila madogo madogo. Wakati ghasia zilipotokea tarehe 5 Julai mjini Urumuchi, chuo kikuu hicho hakikukumbwa na viendo vya kimabavu. Mwandishi wetu wa habari hivi karibuni alitembelea chuo hicho, na kuona kuwa hali ya huko ni shwari sana, ambapo wanafunzi na walimu wa chuo hicho wanaishi pamoja kwa mshikamano kama ilivyokuwa ya hapa awali. Yusufucan mwenye umri wa miaka 21 ni mwanafunzi wa chuo hicho, na anatoka kabila la Wauygur. Alipozungumzia tukio la tarehe 5, Julai, alisema,
"Mambo hayo hayakutokea zamani. Wakati tukio hilo lilipotokea, hali ya chuo chetu ilikuwa shwari, ambapo tunaendelea na masomo yetu chuoni kama kawaida, ili kufanya maandalizi kwa ajili ya mitihani. Maisha yetu hayakuathiriwa na tukio hilo."
Ma Liang mwenye umri wa miaka 23 anatoka kabila la Wahan, lakini alizaliwa na kukua mkoani Xinjiang. Alisema tukio la tarehe 5, Julai la Urumqi lilizushwa na wafarakanishaji walioko nchini na nchi za nje, ambao waliwadanganya na kuwachochea wauyghur wasiofahamu ukweli wa mambo kufanya ghasia dhidi ya watu wa kabila la Wahan na makabila mengine, lakini jambo hilo si mwelekeo mkuu wa jamii ya Xinjiang. Aliwataka watu wa nje ya mkoa wa Xinjiang wasione kuwa kuna uhasama kati ya wauyghur na watu wa makabila mengine. Alisema,
"Kabla ya tukio la tarehe 5, Julai la Urumqi, sikuweza kukubali kuwa hali ya usalama mkoani Xinjiang sio nzuri. Naona kuwa Xinjiang ni mkoa wenye utulivu, mandhari ya mkoa wetu ni nzuri, na watu wake ni wachangamfu sana. Napenda sana maskani yangu, na babu, bibi, baba na mama yangu wote wanaishi hapa. Katika chuo chetu, sisi watu wa makabila mbalimbali tunaelewana sana. Wanafunzi wa kabila la Wahan na wa makabila madogo madogo wanacheza kwa pamoja mara kwa mara."
Ma Liang na Yusufucan wanakaa ghofora moja kwenye bweni lao. Ingawa wanatoka makabila tofauti, lakini wanadumisha urafiki mkubwa, na mara kwa mara wanakwenda kucheza mpira kwa pamoja. Baada ya tukio la tarehe 5, Julai, wanafunzi hao wawili na kusaidiana zaidi, na kuishi kama ndugu wa familia moja. Yusufucan alisema,
"Sisi ni marafiki wakubwa. Chuo chetu ni kama familia moja, tunaishi na kucheza vizuri kwa pamoja."
Ma Liang alisema,
"Tunaishi pamoja kwa furaha. Tunakaa kwenye jengo moja, na tunasaidiana mara kwa mara. Tukikutana tunasalimiana kwa njia ya jadi ya watu wa Xinjiang."
Yusufucan aliwaambia waandishi wa habari kuwa, mwaka jana mwanafunzi mmoja wa kike wa Chuo Kikuu cha Xinjiang kutoka kabila la Wahan aitwaye Wang Yanna alichangia figo lake moja kwa mwanafunzi mmoja wa sekondari kutoka kabila la Wauyghur aitwaye Maulacan ambaye alikuwa na ugonjwa wa mafigo. Jambo hilo liligusa hisia za watu wengi kutoka makabila mbalimbali mkoani Xinjiang. Yusufucan alisema,
"Wang Yanna aliwashawishi wazazi wake wamkubali atoe figo lake moja kwa Maulacan mwenye ugonjwa wa mafigo. Maulacan anatoka kabila la Wauygur, ambapo Wang Yanna anatoka kabila la Wahan. Sisi watu kutoka makabila mbalimbali kweli ni kama wa familia moja."
Yusufucan alisema Wang Yanna alimchukua Maulacan kama ni mdogo wake. Ma Liang alisema anakubali sana maoni ya Yusufucan. Alisema,
"Huu ni mfano halisi kuwa watu wa makabila mbalimbali wanaishi vizuri kwa pamoja mkoani Xinjiang. Na jambo hilo linaonesha kuwa umoja wa makabila nchini China si wa maneno matupu, bali ni halisi."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |