• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ijue China 16: Makazi ya wachina na majengo ya kisasa

    (GMT+08:00) 2009-07-16 15:09:10

    China ni nchi kubwa yenye sehemu tofauti na utamaduni tofauti. Kutokana na hali hiyo makazi ya watu pia yanatofautiana.

    Katika sehemu wanazoishi watu wa kabila la Wahan, makazi ya watu hujengwa kwa nyumba zenye nyua za mraba, mfano wa ujenzi huo ni makazi yaliyopo mjini Beijing. Nyumba zenye nyua za mraba mjini Beijing zimegawanyika kuwa ua wa mbele na ua wa nyuma. Nyumba iliyopo katikati ni ya heshima kabisa, ni mahali pa kufanyia sherehe za familia, na kupokelea wageni wa heshima. Nyumba zote pembeni mwa ua wa mbele na ua wa nyuma zinaelekea katikati ya ua na zinaunganishwa kwa ujia wenye paa. Kuishi katika nyumba kama hizi ni starehe na kutokana na kuishi pamoja katika nyumba hizo uhusiano wa jamaa unakuwa ni wa karibu sana. Nyumba za aina hiyo zipo katika sehemu za kaskazini, na kaskazini mashariki za China.

    Majumba ya ghorofa yanajengwa zaidi katika sehemu za kusini za China, umbo la nyumba ni la duara, mraba au la yai, mithili ya ngome. Katikati ya jumba hilo kunakuwa na kiwanja ambacho kuna kisima na ghala la nafaka. Milango ya nyumba ikifungwa kwa ajili ya kuzuia wezi au katika siku za vita, watu wanaoishi ndani ya nyumba hiyo wanaweza kukaa humo bila wasiwasi wa kukosa maji wala chakula kwa miezi kadhaa. Kwa kawaida nyumba kama hizo huwa na ghorofa tatu au nne.

    Nyumba za ghorofa za udongo zinajengwa kwa mchanganyiko wa udongo, kokoto, mchanga na mbao, katika siku za majira ya baridi, ndani nyumba kunakuwa na joto, na katika siku za majira ya joto ndani ya nyumba huwa na baridi, na tena nyumba hizo ni madhubuti na zinaweza kuhimili hata tetemeko la ardhi.

    Pia kuna aina nyingi za makazi ya watu wa makabila madogo madogo. Makazi ya kabila la Wauygur mkoani Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, yanajengwa kwa paa lililo bapa, kuta za udongo na ghorofa moja au mbili, na kuna ua mbele ya nyumba; Makazi ya kabila la Watibet yanajengwa kama ngome, kuta za mawe kwa nje na mbao kwa ndani na paa lililo bapa; Watu wa kabila la Wamongolia ni wafugaji, wanaishi katika mahema ambayo ni rahisi kuyahamisha kufuata malisho ya mifugo; Watu wa makabila madogo madogo katika sehemu ya kusini magharibi mwa China wanaishi katika nyumba zilizojengwa milimani karibu na maji, ghorofani wanaishi watu, na chini inaishi mifugo au kunahifadhiwa vitu mbalimbali. Majumba hayo hujengwa kwa mianzi na kusimamishwa kwa nguzo bila kuwa na msingi ardhini.

    China ni nchi kubwa yenye makabila mengi, kwa hiyo makazi pia ni ya aina nyingi. Makazi katika sehemu za mwanzo na katikati ya Mto Huanghe, mengi zaidi yanajengwa kwa mapango, makazi hayo yako katika mikoa ya Shan'xi, Gansu, Henan na Shanxi. Wakazi wa sehemu hizo wanachimba mapango kwenye milima ya udongo na familia moja huwa na mapango kadhaa yanayounganishwa kwa ndani. Pia kwa ndani mapango hujengwa kwa matofali. Mapango hayo hayashiki moto, yanazuia kelele, na huwa na baridi wakati wa majira ya joto na joto katika majira ya baridi, na hayatumii ardhi ya kilimo.

    Nchini China kuna miji ya kale ambayo mpaka sasa bado iko vilevile. Ndani ya miji hiyo kuna makazi mengi ya kale. Kati ya miji hiyo, mji wa Pingyao, mkoani Shanxi, kaskazini mwa China, mwaka 1998 mji wa Lijing, mkoani Yunan kusini mwa China, imeorodheshwa katika kumbukumbu za urithi wa dunia mwaka 1998.

    Mji wa Pingyao ni mji kamili uliobaki tangu Enzi ya Ming na Qing, ni mfano wa ujenzi wa miji ya kale katika sehemu ya kati ya China. Hadi sasa mji huo bado uko kama ulivyokuwa zamani. Kuta zake za mji, barabara, makazi, maduka na mahekalu bado yapo. Ni sehemu muhimu kwa ajili ya utafiti wa kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, mambo ya kijeshi, ujenzi na sanaa katika histroria ya China.

    Mji wa Lijiang ni mji uliokuwepo toka Enzi ya Song Kusini. Ujenzi wa mji huo ni mchanganyiko wa mitindo ya kabila la Wanaxi na mitindo ya nchi za nje. Kutokana kutoathiriwa na itikadi ya kimwinyi iliyotawala sehemu za ndani za China, barabara za mjini hazikupangwa kwa utaratibu, wala hakuna kuta za mji. Ziwa la Heilong ni chanzo cha maji, mito midogo mingi inaanzia kwenye ziwa hilo na kupeleka maji kwenye makazi, kwa hiyo ndani ya mji mito midogo inaonekana kila mahali, na kwenye kingo za mito hiyo kuna miti mingi.

     

    Majengo ya kisasa yanamaanisha majengo yaliyojengwa kuanzia katikati ya karne ya 19 hadi sasa.

    Tokea vita vya kasumba vya mwaka 1840 hadi Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, majengo yenye mtindo wa kichina na wa kimagharibi yalitokea nchini China. Katika kipindi hiki, majengo ya mtindo wa kichina yanaendelea kuongezeka, lakini majumba ya michezo, mahoteli, maduka, na maduka makubwa yanajengwa kwa mchanganyiko wa mitindo ya kichina na ya kimagharibi; na majengo ya aina ya kimagharibi yalitokea katika miji ya Shanghai, Tianjin, Qingdao na Harbin kwenye sehemu zilizokodiwa na nchi za nje, na pia majengo ya ubalozi, benki za nchi za nje na mahoteli na klabu za nchi za nje zilijengwa katika miji hiyo.

    Baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, ujenzi wa nyumba uliingia katika kipindi kipya cha kihistoria, kutokana na jinsi uchumi ulivyoendelea kwa haraka, ujenzi wa majengo uliongezeka. Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, majengo yalianza kuwa ya aina tofauti.

    Ukumbi Mkuu wa Umma uko katika upande wa magharibi wa uwanja wa Tian An Men, ni mahali ambapo viongozi wa taifa na umma wanashughulika mambo ya siasa, na pia ni moja kati ya majengo makubwa nchini China. Ukumbi huo ulijengwa mwaka 1959, eneo lake ni mita za mraba laki 1.7. Ukumbi Mkuu wa Umma unaonekana kwa ufahari, na unalingana na mazingira ya uwanja wa Tian An Men. Mlango wa mbele unatazama uwanja wa Tian An Men, na juu ya mlango huo imebandikwa nembo ya taifa, na pande mbili za mlango huo ni nguzo 12 ya marumaru yenye urefu wa mita 25. Baada ya kuingia kwenye mlango huo kuna ukumbi mkubwa, nyuma ya ukumbi huo ni ukumbi wa mikutano wenye eneo la mita 76 kwa upana na mita 60 kwa urefu, kwenye upande wa kulia wa ukumbi huo wa mkutano kuna ukumbi wa sherehe wenye nafasi 5,000. Ndani ya Ukumbi Mkuu wa Umma kuna kumbi zaidi ya mia moja, na kila ukumbi una uzuri wake wa kipekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako