• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ijue China 21 Siku ya kufanya tambiko

    (GMT+08:00) 2009-07-23 16:31:20

    Tarehe 8 Desemba katika kalenda ya kichina ni siku ya jadi ya kabila la Wahan ambayo pia inaashiria sikukuu ya mwaka mpya wa kichina kukaribia.

    Kutokanna na maandishi ya kale, siku ya 8 Desemba katika kalenda ya kichina ni siku ya kufanya tambiko katika China ya kale. China ni nchi inayotilia maanani sana kilimo. Kila mwaka mavuno mazuri yalipopatikana watu wa kale walikuwa wanafanya tambiko ili kumshukuru mungu. Baada ya tambiko watu hukusanyika kufanya sherehe za burudani, kupika uji wa mseto na kula pamoja. Katika karne ya 5 serikali ya enzi zile iliweka siku hiyo yaani 8 Desemba kuwa ni sikukuu.

    Baada ya dini ya Buddha kuingia nchini China, maana ya siku hiyo ya 8 Desemba ilikuwa imeongezeka. Inasemekana kwamba kabla ya Sakyamuni kuwa Buddha alikuwa na maisha magumu, na alikonda vibaya. Katika siku hiyo alimkuta mchungaji msichana ambaye alimpa bakuli moja la uji wa mseto kutokana na kuona jinsi alivyokonda. Kwa hiyo waumini wa dini wa Buddha pia wanapika uji wa mseto katika siku hiyo.

    Watu wa China wana desturi ya kunywa uji wa mseto kuanzia Enzi ya Song yaani miaka elfu moja iliyopita. Katika siku hiyo ya 8 Desema kila familia na hata maofisa wa serikali walikuwa wanakunywa uji wenye mchanganyiko wa mchele na kunde.

    Aina za uji wa mseto ni nyingi kutokana michele na kunde tofauti zilizotiwa ndani ya uji, lakini kwa kawaida huwa ni mchele, muwele, ngano na mahindi, mtama, choroko, maharage na kunde nyekundu.

    Vitu vilivyokuwa vinatiwa ndani ya uji pia kulikuwa na matunda yaliyokaushwa, na mbegu za matunda kama karanga, njugumawe, alizeti, zabibu, tende, n.k.

    Baada ya vitu vyote kuwa tayari, uji hupikwa kwa moto mdogo na kwa muda mrefu. Katika majira ya baridi jamaa wanajikusanya pamoja kando ya meza na kunywa uji kama huo.

    Wenyeji wa Beijing wanaichukulia siku hiyo kama ni ishara ya kukaribia kwa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina. Licha ya kunywa uji wa mseto, katika siku hiyo watu hutia saumu ndani ya siki ili watumie katika mkesha wa mwaka mpya wakati wanapokula Jiaozi, chakula kama sambusa ndogo kilichochemshwa.

    Katika miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita, Wachina wamekuwa na mila ya kufanya tambiko kwa mungu wa jiko katika tarehe 23 mwezi wa 12 kwa kalenda ya kichina. Mungu wa Jiko alitokea katika hadithi za mapokeo, yeye ni ofisa aliyetumwa na mungu kwenye kila familia, na kila mwaka anakwenda kwa mungu kutoa ripoti. Kwa hiyo watu humwabudu sana na kwa ajili ya kumfurahisha, kila mwaka katika siku hiyo watu hufanya tambiko. Kuna masimulizi mengi kuhusu mila hiyo.

    Zamani za kale kulikuwa na tajiri mmoja aliyeitwa Zhang Sheng, mke wake Ding Xiang alikuwa kisura na mwenye akili. Mwanzoni waliishi kwa furaha sana. Siku moja tajiri huyo alipofanya biashara alimkuta msichana mmoja mrembo aliyeitwa Hai Tang, mara walianza kupendana. Muda si mrefu baadaye Zhang Sheng alimwoa Hai Tang na kumleta nyumbani. Msichana Hai Tang alipoona mke wa tajiri alikuwa mrembo na ni mke halali alikuwa na wivu, alimtaka tajiri kumfukuza.

    Tokea hapo Zhang Sheng na mkewe waliishi maisha ya anasa, na baada ya miaka miwili, walifuja mali zote na wote walikuwa maskini. Kwa kuona kuwa Zhang Sheng amekuwa maskini, Hai Tang alimwacha na kuolewa na mwingine. Zhang Sheng alibaki peke yake, kwa kulazimika na umaskini alibadilika kuwa ombaomba. Siku moja theluji ilikuwa kubwa, Zhang Sheng alisikia baridi na njaa, alianguka mbele ya mlango wa nyumba ya tajiri mmoja. Mtumishi alipotoka nyumbani alimwona na kumsaidia kumpeleka jikoni. Dakika chache baadaye mwenye nyumba alikuja kumwangalia, Zhang Sheng alishtuka alipofahamu kuwa huyo mwenye nyumba ndiye aliyekuwa mkewe Ding Xiang. Kwa kuona aibu alijipenyeza ndani ya tundu la kijiko cha kuwashia kuni. Ding Xiang alipoingia jikoni hakumwona yeyote, aliona ajabu, kisha baadaye aligundua kitu fulani kilichoziba tundu la kijiko, alikivuta kitu hicho akatambua ni mtu aliyekuwa mumewe ambaye amekwisha kufa kutokana na kuungua na moto. Siku chache baadaye Ding Xiang alikufa kutokana na huzuni. Mungu alipopata habari hiyo aliona kuwa Zhang Sheng ni mtu mwema, alijuta makosa yake, alimteua kuwa mungu wa jiko. Watu walimwabudu mungu huyo wa jiko na mkewe pia, na kuweka sanamu zao ndani ya jiko.

    Ili mungu awasemee wema mbele ya mungu, watu hupika sukari ya kimea iliyonatanata kwa nafaka, ili mungu wa jiko anapokula sukari hiyo ulimi utakuwa ladha tamu na kusema maneno mazuri juu ya familia aliyokaa.

    Usiku wa siku ya mwisho ya Desemba katika kalenda ya kichina ni mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina.

    Katika usiku huo wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya, mila na desturi za Wachina ni nyingi. Moja ni kufagia nyumba. Kabla ya kufikia siku ya mwisho ya mwaka, watu hufagia nyumba kwa maana ya kuondoa uchafu na kusherehekea mwaka mpya katika hali ya kila kitu kuwa safi. Baada ya kusafisha, wanapamba nyumba kwa maandishi yenye maneno ya kuomba baraka na picha, na kutundika taa nyekundu.

    Katika mkesha wa mwaka mpya, jamaa hula pamoja, hata fulani akiwa mbali kwa kazi lakini katika siku hiyo hurudi nyumbani kujumuika na jamaa zake na kula nao pamoja.

    Chakula cha usiku wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya katika sehemu ya kusini na sehemu ya kaskazini ni tofauti. Watu wa sehemu ya kusini hupika vitoweo vingi zaidi na kumi na watu wa sehemu ya kaskazini wana mila ya kula Jiaozi kwa kuchovya kwenye siki iliyotiwa saumu.

    Katika usiku huo watu wazima huwachukua watoto na kwenda nao kwa jamaa na kuwapelekea zawadi, na watoto katika usiku huo wanawasibiliza wazee wosia wao. Katika usiku huo watoto hupewa fedha ambazo zinaitwa "fedha za kuaga mwaka". Si wazee si watoto, katika usiku huo hawalali, baada ya chakula, wanaongea huku wanakunywa chai na kula vyakula vya udohodoho na kuangalia michezo ya televisheni mpaka alfajiri.

    Katika usiku huo watoto huwa na furaha tele, wanapitisha usiku huo wakiwa pamoja na wazee na kuwasha fataki. Mshairi mkubwa wa China ya kale Lu You aliwahi kueleza watoto walivyokuwa katika usiku huo "Watoto wavumilia usingizi na kuwa na furaha hadi alfajiri".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako