• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la Kiswahili la Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin

    (GMT+08:00) 2009-07-24 16:24:59

    Ikilinganishwa na vyuo vikuu viwili tulivyojulisha katika vipindi vilivyopita, Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin ni kama kijana kwenye upande wa ufundishaji wa lugha ya Kiswahili. Mwaka 2007 Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin kilianzisha kozi ya lugha ya Kiswahili, hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa chuo hicho kuanzisha kozi hiyo katika historia yake. Mkurugenzi wa kitivo cha lugha ya Kiswahili cha Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin Bi. Rui Jufen alisema, katika miaka ya hivi karibuni watu wenye ujuzi wa lugha ya Kiswahili wamekuwa wanahitajiwa zaidi kutokana na ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika, hivyo chuo hicho kiliamua kuanzisha kozi ya lugha ya Kiswahili. Alisema,

    Vijana huwa ni nguvu uhai. Ingawa hivi sasa kuna wanafunzi sita tu wanaojifunza lugha ya Kiswahili katika Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin, lakini shirika la lugha ya Kiswahili lililoanzishwa na vijana hao linajulikana sana katika chuo hicho, na linawavutia wanafunzi wa kozi nyingine.

    (wimbo)

    Wasikilizaji wapendwa, wimbo mliosikia ni wimbo wa taifa wa Tanzania, waimbaji ni wanafunzi wa darasa la Kiswahili la Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin, ambao wameanzisha "shirika la lugha ya Kiswahili".

    Msichana Hu Yue ni mkuu wa shirika hilo, ambaye pia ni monita wa darasa la lugha ya Kiswahili. Msichana huyo alisema wanafunzi waliopo ni kundi la kwanza la wanafunzi wa Kiswahili katika historia ya Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin, Wanafunzi wa kozi nyingine wanaona ajabu sana kuhusu lugha hiyo. Watu wengi waliwauliza maswali kama lugha ya Kiswahili inatumika katika nchi gani? ni rahisi kuongea kwa lugha hiyo? Licha ya hayo watu wengi hawafahamu sana hali ya Afrika, waliambiwa zaidi ni hali ya umaskini, magonjwa na migogoro vimeenea barani Afrika. Hivyo Hu Yuen na wenzake wanaona kuwa ni lazima kueneza ujuzi kuhusu Afrika. Alisema,

    "Wakati ule tulifikiri kuunda kikundi cha lugha ya Kiswahili, ambapo tunaweza kuendesha shughuli mbalimbali, kuwafundisha wanafunzi wengine maneno rahisi ya Kiswahili, ili waweze kuelewa lugha hiyo na hali ya Afrika. Tunataka kuwajulisha Afrika yenye hali mpya, hili ni lengo letu la kuandaa shirika la lugha ya Kiswahili."

    Mwezi Novemba mwaka 2007, yaani miezi mitano baada ya Hu Yue na wenzake kuingia kwenye Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin, walianzisha shirika la lugha ya Kiswahili la Chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin. Hu Yue na wenzake walifanya juhudi kupanga shughuli, kuagiza darasa la kuandaa shughuli, kuweka mazingira, kutengeneza kadi ya mwaliko, kuandaa zawadi, na kuwaalika wageni. Kutokana na jitihada za pamaoja za Hu Yue na wenzake, shughuli za shirika la lugha ya Kiswahili zimefuatiliwa sana na wanafunzi wengine wa chuo hicho, na watu wengi walishiriki kwenye shughuli hizo. Hu Yue alisema,

    "Watu wengi wanataka kushiriki kwenye shughuli za shirika la lugha ya Kiswahili, lakini darasa letu linaweza kujaa watu hamsini tu, hivyo kila mara tunaweza kupokea wanafunzi hamsini tu."

    Katika shughuli za shirika la lugha ya Kiswahili, wanafunzi wa kozi ya lugha ya Kiswahili wanafundisha wanachama wa shirika hilo la lugha ya Kiswahili kuhusu namna ya kusalimiana, pia wanajulisha desturi, utamaduni na ujuzi wa Afrika Mashariki. Hadi sasa shirika hilo limeandaa shughuli nyingi zilizojulisha vyakula, nguo, na sikukuu za Afrika Mashariki, na hali ya jumla ya Tanzania na ya Kenya. Vilevile linawaalika wanafunzi kutoka Tanzania na Kenya wanaosoma mjini Tianjin kushiriki kwenye shughuli hizo, ambapo wanafanya mawasiliano na wanafunzi wa China.

    Wanafunzi wanaochukua kozi ya lugha ya Kiswahili katika chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin wanaona kuwa, shughuli za shirika la lugha ya Kiswahili zimepanua ushawishi wa kozi hiyo chuoni, wakati huo huo zinatoa msaada kwa masomo yao wenyewe. Mvulana Yu Sunqian alisema,

    "Ingawa tuliwafundisha watu wa nje ya darasa letu maneno rahisi ya Kiswahili, lakini wakati tulipofundisha maneno hayo, tulikuwa tunaweza kukumbuka masomo tuliyojifunza. Aidha, tulijulisha utamaduni, jiografia, na hali ya nchi za Afrika kwa watu wengine, tuliweza pia kuzidisha uelewa wetu, na kuongeza hamu zetu juu ya masomo. "

    Kwenye mchakato wa maendeleo ya shirika la lugha ya Kiswahili, walimu wanawaunga mkono wanafunzi hao, Bi. Rui Jufen alisema, wanafunzi hao wameanzisha shirika hilo na kufahamisha utamaduni wa Afrika Mashariki, hii inaonesha umuhimu wa lugha yenyewe. Aliona kuwa lugha ni chombo cha mawasiliano, na nia ya kufanya mawasiliano ni kuhimiza maelewano na kuimarisha urafiki.

    Shirika la lugha ya Kiswahili linaendelezwa siku hadi siku, na wanafunzi wa kozi ya lugha ya Kiswahili wa chuo kikuu cha lugha za kigeni cha Tianjin wanaona kuwa wanabeba wajibu mzito zaidi. Lakini wana imani na mustakabali wa maendeleo ya shirika hilo. Wanakumbuka kuwa, kwenye mkutano mkubwa wa walimu na wanafunzi wote uliofanyika mwaka 2007, mkuu wa chuo hicho alipowakaribisha wanafunzi hao sita aliwaambia, ingawa nyini ni wanafunzi sita, lakini nyuma yenu, kuna Afrika yenye nguvu kubwa. Maneno hayo yanawahimiza siku hadi siku katika masomo yao.

    Wasikilizaji wapendwa, kipindi hiki cha daraja la urafiki kati ya China na Afrika kwa leo kinaishia hapa. Kwa herini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako