• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchoraji wa kwanza wa China Bw. Liu Zhong aliyeshiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya sanaa huko Venice Italia

    (GMT+08:00) 2009-07-27 17:12:21

      

    Bw. Liu Zhong

    Maonesho ya 53 ya kimataifa ya sanaa yanayofanyika kila baada ya miaka miwili hivi sasa yanafanyika huko Vinice Italia, hili ni tamasha kubwa linaloshirikisha wasanii 30 wakubwa duniani kufanya maonesho yao binafsi, mmoja kati ya wasanii hao ni mchoraji Liu Zhong ambaye ni mchoraji wa kwanza kabisa kutoka China kushiriki kwenye maonesho hayo. Kwenye ufunguzi wa maonesho hayo balozi mdogo wa China nchini Italia Bw. Guo Shizong kwa niaba ya balozi Sun Yuxi alisema,

      "Kwa niaba ya Bw. Sun Yuxi, balozi wa China nchini Italia, natoa pongezi nyingi kwa mwandaaji wa maonesho haya, na vile vile kwa moyo wa dhati natoa pongezi kwa Bw. Liu Zhong, kwani kushiriki kwake kwenye maonesho hayo yenye heshima kubwa duniani kumethibitisha vya kutosha ufanisi wake."

    Maonesho hayo ya kimataifa ya sanaa yanayofanyika huko Venice kila baada ya miaka miwili yalianza mwaka 1895, ni maonesho yanayosifiwa kuwa ni "Olimpiki ya Sanaa", kila mara wanachaguliwa wasanii 30 wakubwa duniani kushiriki kwenye maonesho hayo ili wafanye maonesho yao binafsi. Hapo kabla wachoraji wa China walikuwa wakishiriki kwenye maonesho hayo kwa kikundi. Katika historia ya maonesho ya Venice hii ni mara ya kwanza kwa mchoraji wa China kufanya maonesho binafsi. Bw. Liu Zhong alipozungumzia nafasi aliyoipata ya kushiriki kwenye maonesho hayo alisema, anamshukuru mwenyekiti wa kituo cha utamaduni cha Italia ambaye pia ni mkurugenzi wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo Bw. Vincenzo Sanfo, akisema,

      "Bw. Vincenzo Sanfo aliwahi kuziona picha nilizochora kwenye maonesho yaliyofanywa katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka jana, alivutiwa sana na alisema atanisaidia nipate nafasi ya kushiriki kwenye maonesho nje ya China."

      Bw. Vincenzo Sanfo anaona kwamba picha za mtindo wa Kichina alizochora Liu Zhong zimeonesha zaidi moyo wa kutunza mazingira ya asili, na moyo huo ulimvutia sana. Alisema,

      "Sababu ya kumchagua Bw. Liu Zhong kushiriki kwenye maonesho hayo ni kuwa picha alizochora kwa brashi na wino hazijawahi kuoneshwa katika historia ya maonesho ya Venice. Nia yangu ni kuwafahamisha watu jinsi gani picha za mtindo wa Kichina zilivyo. Bw. Liu Zhong anatilia maanani utunzaji wa mazingira ya asili na hasa wanyamapori. Picha zilizochorwa naye kwa makini zimeonesha heshima kwa wanyama, moyo wake huo umeniathiri sana."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako