• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mafanikio yaliyopatika katika mambo ya kidiplomasia nchini China katika miaka 60 iliyopita

    (GMT+08:00) 2009-07-28 18:21:02

    Wasikilizaji wapendwa, katika kipindi hiki cha chemsha bongo kuhusu Miaka 60 ya Jamhuri ya Watu wa China,tunawaletea makala ya 4 kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika mambo ya kidiplomasia katika miaka 60 iliyopita tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe.

    Kabla ya kuwasomea makala ya leo, tunatoa maswali mawili ili msikilize vizuri na muweze kujibu maswali. Swali la kwanza: Jamhuri ya Watu wa China ilirudishwa kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa mwaka gani? Swali la pili: Mpaka sasa China imeanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi ngapi duniani?

    "Sisi wakomunisti siku zote tuna imani na ukomunisti na kuona mfumo wa ujamaa ni mzuri, lakini kwenye mkutano huu hakuna haja ya kueneza fikra na itikadi ya watu binafsi na mfumo wa siasa wa nchi mbalimbali. Ujumbe wa China unakuja hapa siyo kwa ajili ya kuonesha maoni yake tofauti na wengine…." Hayo ni maneno aliyosema waziri mkuu wa serikali ya China ambaye pia alikuwa waziri wa mambo ya nje wa awamu ya kwanza wa China Bw. Zhou Enlai katika hotuba yake aliyotoa kwenye mkutano uliofanyika huko Bandung, Indonesia mwezi Aprili mwaka 1955. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa China mpya kuhudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa, kwenye mkutano huo, kanuni tano inazotetea China kuhusu kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, kutoshambuliana, kutoingiliana mambo ya ndani, kuwa na usawa na kunufaishana na kuishi pamoja kwa amani, ilianza kueleweka kwa nchi nyingi zaidi. Hivi sasa, kanuni tano hizo za kuishi pamoja kwa amani zimeweka mizizi mioyoni mwa watu na kuwa kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, ambazo zinatambuliwa duniani.

    Ingawa China ilipita mabadiliko mengi makubwa duniani, siku zote inashikilia kithabiti kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, hii ni sababu kubwa kwa China kupata marafiki wengi zaidi siku hadi siku, na marafiki hao wengi ni wa nchi zinazoendelea. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, mwanzoni China ilitengwa na nchi kubwa za magharibi, ambapo nchi zilizoanzishwa uhusiano wa kibalozi na China zilikuwa zaidi ya 10 tu wakati huo, lakini hivi sasa nchi 171 zimeanzisha uhusiano wa kibalozi na China.

    Urusi ya zamani ilikuwa nchi ya kwanza duniani iliyoanzisha uhusiano wa kibalozi na China, ambayo ilitangaza uamuzi wake huo Tarehe 2 Oktoba mwaka 1949, siku ya pili baada ya Jamhuri ya watu wa China kuanzishwa. Baada ya kusambaratika kwa Urusi mwezi Desemba mwaka 1991, Russia ikaendelea na uhusiano wa kibalozi na China. Siku chache zilizopita, rais Hu Jintao wa China alipokutana na rais Dimitry Medevedev wa Russia huko London, pande mbili zilifikia makubaliano muhimu kadha wa kadha kuhusu kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Russia, kufanya juhudi za pamoja za kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika mambo ya kimataifa.

    Bw. Tikhvinsky ni mzee mwenye umri wa miaka 90 wa Russia, ambaye amewahi kuwa konsela mkuu wa Urusi mjini Beijing, yeye alishuhudia mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya Urusi na China. Mwezi Oktoba mwaka 2008, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alipofanya ziara huko Moscow alizungumza na mzee Tikhvinsky, ambapo walisema:

    "Mzee Tikhvinsky alisema: Shughuli za "mwaka wa lugha ya Kirusi nchini China" na "mwaka wa lugha ya Kichina nchini Russia" zitakazofanyika zitaanzisha mazingira mazuri kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Russia katika mambo ya utamaduni, tunaweza kuimarisha ushirikiano kati yetu katika mambo ya utamaduni na elimu, na kuvutia vijana wengi washiriki kwenye mawasiliano ya kubadilishana maoni."

    "Waziri mkuu Wen Jiabao alisema, kabla ya miaka 60 iliyopita wewe ulikuwa konsela mkuu wa Urusi mjini Beijing na kuhudhuria sherehe ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, kweli umeshuhudia mengi. Urafiki kati ya wananchi wa China na Russia ni wa kudumu na wa maendeleo endelevu, ambao hautaweza kukatizwa. Kama afya yako ni nzuri, wakati wa kufanyika kwa shughuli za "mwaka wa lugha ya Kichina na Kirusi", nakualika uje Beijing kutembelea."

    Baada ya kuingia katika miaka ya 60 na 70 ya karne iliyopita, uhusiano kati ya China na nchi za magharibi uliokwama ulianza kubadilika, ambapo China na Marekani zilianzisha uhusiano wa kibalozi.

    Kuanzia mwisho wa miaka ya 60 hadi mwisho wa miaka ya 70 ya karne iliyopita, Marekani na nchi nyingine za magharibi zilirekebisha sera zao kwa China kutokana na maslahi yao zenyewe. Mawasiliano kati ya wachezaji wa mpira wa meza wa China na Marekani yaliyojulikana wakati huo yalifungua mlango wa mawasiliano kati ya China na Marekani uliofungwa kwa zaidi ya miaka 20. Mwaka 1971, waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa wakati huo Bw. Henry Kissinger alikuja China kwa siri, hadi rais wa Marekani wa wakati huo Richard Nixon kufanya ziara ya China, na nchi mbili China na Marekani kutoa taarifa ya pamoja, uhusiano kati ya China na Marekani ulipata maendeleo makubwa. Mwezi Januari mwaka 1979, uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani ulianzishwa rasmi. Baada ya hapo, katika kipindi cha mwanzo, thamani ya biashara kati ya China na Marekani ilikuwa chini ya dola za kimarekani bilioni 2.5, mpaka sasa thamani hiyo imezidi dola za kimarekani bilioni 300. Mwezi Aprili mwaka huu, rais Hu Jintao wa China na rais Obama wa Marekani walikutana huko London na kufikia maoni ya pamoja kuhusu kufanya juhudi za kujenga uhusiano wa ushirikiano kati ya China na Marekani kwa pande zote, na kufanya mpango mpya kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo mbili katika siku za baadaye.

    Maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia na kati ya China na Marekani yameonesha mambo ya kidiplomasia ya China yaliyobadilika na yasiyobadilika katika miaka 60 iliyopita, ambapo China haifungamani na nchi yoyote kubwa; inaendeleza uhusiano kati yake na nchi mbalimbali duniani bila kujali tofauti za mifumo ya jamii au itikadi; inashikilia kuanzisha uhusiano wa kirafiki na nchi zote kwenye msingi wa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani; kuboresha na kuendeleza uhusiano na nchi zilizoko pembezoni mwake na nchi nyingi zinazoendelea, ambapo ikifuata sera ya ufunguaji mlango katika kuimarisha nguvu za jumla za nchi, na kupiga hatua kubwa za kujiunga na dunia, pia imepata fursa nyingi zaidi za kutoa maoni katika mambo ya kimataifa.

    Mwezi Oktoba mwaka 1971, Baraza kuu la 26 la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la nambari 2758 la kurudisha haki zote halali za Jamhuri ya watu wa China katika Umoja wa Mataifa. Bw. Ling Qing alikuwa mwakilishi wa kudumu wa China wa awamu iliyopita katika Umoja wa Mataifa, na alikuwa kushiriki katika kazi ya kuifanya China irudishiwe kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa. Bw.Ling Qing alisema: 

    Jamhuri ya watu wa China ilirudishwa kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa ambayo ni jumuiya ya kimataifa kati ya serikali iliyo kubwa zaidi duniani, huu kweli ni ushindi mkubwa wa China katika mambo ya kidiplomasia. Hakika huu pia ulikuwa ushindi mkubwa wa dunia, kwani mambo ya kidiplomasia ya China ni kwa ajili ya kulinda amani ya dunia, kuhimiza maendeleo ya pamoja, na kuunga mkono dunia ya tatu, hii ni sera yetu ya kimsingi, nguvu kama hiyo ya kisiasa hakika inaweza kuonesha umuhimu wake katika Umoja wa Mataifa.

    Kurudishiwa kiti kwa China kwenye Umoja wa Mataifa kulifungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na Umoja Mataifa, ambapo mambo ya kidiplomasia ya China ya kufanya ushirikiano na pande mbalimbali yakaanza kufanyika. Katika miaka 30 hivi kabla ya mwaka 1978, viongozi wa China waliwahi kushiriki kwenye shughuli 6 tu za kidiplomasia zilizohusu ushirikiano wa pande nyingi wa kimataifa. Tangu hapo mpaka sasa, China imejiunga na jumuiya zaidi ya 100 za kimataifa, imejiunga na mikataba ya kimataifa zaidi ya 300, na imeshiriki kwenye shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, ambapo imetuma askari wa kulinda amani zaidi ya elfu 10.

    Baada ya kuingia katika karne mpya, China imetoa wazo la kujenga "dunia yenye masikilizano". Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi alisema:

    "Katika dunia ya sasa, mambo ya kidiplomasia hayapaswi kuwa siri na mchezo, bali yanapaswa kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja. Mambo ya kidiplomasia ya China siku zote yanafanyika kwa kufuata wazo la taifa la China la masikilizano, ushirikiano, kunufaishana na maendeleo ya pamoja."

    Sasa tunatoa maswali mawili ili muweze kujibu: Swali la kwanza: Jamhuri ya Watu wa China ilirudishiwa kiti chake halali kwenye Umoja wa Mataifa mwaka gani? Swali la pili: Mpaka hivi sasa China imeanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi ngapi duniani?

    Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza makala ya 4 ya chemsha bongo kuhusu miaka 60 ya Jamhuri ya watu wa China.

    "kikundi cha huduma za matibabu" ambacho hakitaondoka

    Kampeni ya pamoja ya kutoa misaada ya kimatibabu ya China na Gabon inayoitwa 'malaika wa amani mwaka 2009' ilimalizika tarehe 28 Juni huko Makokou, mji mkuu wa mkoa wa Ogooue-Ivindo ulioko kaskazini mashariki mwa Gabon. Katika kampeni hiyo ya wiki mbili, watoa matibabu wa China si kama tu walitoa huduma za matibabu bila malipo kwa wakazi wa huko na kuondoa maumivu yao, bali pia walieneza urafiki na kuweka 'kikundi cha huduma za matibabu' ambacho hakitaondoka nchini humo.

    Sehemu ya Mekambo iliyoko kilomita 800 kutoka Libreville, mji mkuu wa Gabon ni moja kati ya sehemu nne ambazo kikundi cha matibabu cha China kilitoa misaada ya kimatibabu nchini humo. Kutokana na sehemu hiyo kuwa katikati ya misitu ya kitropiki na hali ya mawasiliano ya huko ni mbaya, sehemu hiyo inakabiliwa na ukosefu wa dawa na kazi za kuzuia magonjwa ya kuambukiza pia ni dhaifu sana. Katika muda mrefu uliopita wakazi wa huko wamekuwa wakikabiliwa na tishio kubwa la magonjwa mbalimbali yanayoenezwa na mbu na inzi, yakiwemo malaria, matende na homa ya manjano. Katika miaka kadhaa iliyopita ugonjwa wa Ebola ulilipuka mara tatu kwenye sehemu hiyo. Mtaalamu wa usimamizi wa wadudu waharibifu wa China ambaye ni mtafiti wa taasisi ya sayansi ya matibabu ya jeshi la China Porfesa Yang Zhenzhou alisema:

    "tumeleta zana ya kusafisha maji na dawa ya kuangamiza vijidudu, ili kukinga na kudhibit magonjwa yanayoenezwa na wadudu, tumetumia mahema yenye dawa ya kuzuia mbu. Aidha tumeleta vifaa vya aina mbalimbali vya kupulizia dawa ili kuhakikisha kwanza sisi watoa matibabu hatuambukizwi na magonjwa hayo. Aidha katika wiki mbili tuliyokuwa huko, tulitoa mafunzo kwa kikundi cha watoa matibabu wenyeji, halafu wataendelea kutoa mafunzo kwa wengine, kwa njia hii ni kama tumeweka 'kikundi cha huduma za matibabu' ambacho hakitaondoka."

    Ofisa wa jeshi la huko anayeshuguhulikia huduma za matibabu Meja Justin Beyassa alisema Mekambo inaaminiwa kuwa ni chanzo cha virusi vya homa ya Ebola, pamoja na hali mbaya ya mawasiliano ya huko, watu wa nje hawataki kwenda sehemu hiyo. Kikundi cha matibabu cha China si kama tu kilipeleka vifaa maalumu vya kuzuia maambukizi ya magonjwa, wataalamu wa China pia walitoa maelekezo kuhusu teknolojia na mbinu za kuzuia maradhi, ambayo ni jambo zuri kwa wakazi wa huko, pia imeonesha urafiki wa jadi kati ya China na Gabon. Bw. Beyassa alisema:

    "tumejifunza mambo mengi ya kiufundi, kwa mfano teknolojia ya kuangamiza vijidudu, teknolojia ya kuangamiza mbu kwenye eneo la makazi tumejifunza mambo mengi kutoka kwao."

    Kwenye shughuli hiyo ya pamoja, kikundi cha matibabu cha China kimetoa vipeperushi vingi vya elimu ya afya pamoja na vitu vingi vya huduma za afya zikiwemo dawa za meno, mswaki na kondom kwenye vituo mbalimbali vya huduma za afya mkoani Ogooue-Ivindo, ili kutangaza ujuzi wa kinga na udhibiti wa magonjwa na kueneza utaratibu wa kiafya wa maisha.

    Kwenye kituo cha kutoa matibabu bila malipo huko Makokou, mji mkuu wa mkoa huo, kijana anayeitwa Adens alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema anafurahi kuona kikundi cha matibabu cha China kimeweza kutoa huduma za matibabu kwa watu wa Gabon baada ya kusafiri kutoka nchi iliyoko mbali sana na Gabon, na shughuli hiyo imeimarisha elimu ya mambo ya afya pia kumesaidia sana wakazi wa huko. Bw. Adens alisema:

    "naona kuna umuhimu mkubwa wa kuwafahamisha wananchi kuhusu madhara ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, misaada ya matibabu na shughuli za kueneza elimu ya afya iliyofanywa na kikundi cha matibabu cha China zimetusaidia sana. Kwenye sehemu hiyo iliyoathiriwa vibaya na magonjwa ya malaria na Ukimwi, kutoa kondom kwa wakazi kunaweza kuzuia watu wasiambukizwe magonjwa hayo na kubadilisha desturi zao katika maisha ya kujamiiana."

    Mkoa wa Ogooue-Ivindo uko karibu na mpaka wa kaskazini mashariki mwa Gabon, hali ya huduma za matibabu ya huko ni mbaya sana, na ni vigumu kwa wakazi wa huko kupata matibabu na dawa. Watoa matibabu wa China walifanya kadiri wawezavyo kusaidia kukamilisha miundombinu ya matibabu ya huko na kutoa mafunzo na maelekezo kwa watoa matibabu wenyeji wa huko.

    Katika shughuli za pamoja za kutoa misaada ya matibabu za 'malaika wa amani mwaka 2009', watoa matibabu 66 wa China waligawanywa katika vikundi vinne, wakishirikiana na watoa matibabu wa Gabon na kutoa dawa na matibabu ya bila malipo kwenye sehemu za mbali mkoani Ogooue-Ivindo. Mbali na hayo, kikundi cha matibabu cha China pia kilitoa mafunzo kwa watoa matibabu zaidi ya 300 wa Gabon, kusaidia kukamilisha miundombinu ya huduma za afya ya sehemu hiyo na kuweka 'kikundi cha huduma za matibabu' ambacho hakitaondoka nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako