• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Safari ya kujiburudisha mjini Qingdao

    (GMT+08:00) 2009-08-03 16:23:48

    Watu wengi duniani wameshuhudia mvuto wa Qingdao kutokana na mji huo kuandaa michezo ya mashua yenye matanga mjini humo wakati wa michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008. Baada ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya Beijing, katika mji huo unaojulikana kwa utalii, zimeongezeka shughuli za utalii za aina mbalimbali pamoja na kutembelea viwanja na majumba ya michezo ya Olimpiki, kupanda mashua yenye matanga na kufanya matembezi kwenye sehemu isiyo na watu ya kisiwani, ambazo zinapendwa na watu wengi. Katika siku za majira ya joto, kucheza kwenye maji ya pwani ya Qingdao ni chaguo zuri.

    Kituo cha mashua yenye matanga cha Qingdao kilikuwa ni moja kati ya viwanja na majumba muhimu ya michezo ya Olimpiki, na kinajulikana sana nchini na nje kutokana na kufanyika kwa michezo ya mashua yenye matanga ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Hivi sasa kituo hicho kimefungua mlango kwa watu na kutembelewa na watu wengi zaidi ikilinganishwa na sehemu nyingine za utalii mjini Qingdao.

    Baada ya kutembelea kituo hicho, watu wanaweza kupanda kwenye meli au mashua kubwa zenye matanga kuona hali ya kufurahisha kwenye bahari, au kutembelea kwenye sehemu isiyo na watu kwenye kisiwa, au kuvua samaki kwa ndoano baharini, ambapo watu wataburudika sana na kupata kupumzika vizuri.

    Hivi sasa, klabu ya michezo ya boti ya kimataifa ya Qingdao inafanya juhudi kutayarisha "utalii wa siku moja kwenye kisiwa", baada ya siku chache watu wataweza kufanya matembezi kwenye kisiwa cha Dagong na kisiwa cha Zhucha, meneja mkuu wa klabu hiyo, Bw. Dong Yongquan alisema:"Hivi sasa tunaendeleza utalii wa matembezi kwenye kisiwa, hizi ni shughuli za kushiriki kufurahia mazingira ya kimaumbile, kwa hatua ya mwanzo tunawasafirisha watalii kwa safari nne kwa siku, tunakadiria kuwa matumizi ya kila mtu ni chini ya Yuan za Renminbi 100."

    Gharama ya usafirishaji ya Yuan 100 inawawezesha watu wengi waimudu, klabu hiyo itajitahidi kufanya shughuli za kukamata samaki kwa ndoano baharini za kuvutia zaidi, ili kuongeza mvuto wa utalii wa baharini. Watu wanaopenda mashua yenye matanga, wataweza kusafiri baharini wao wenyewe baada ya kupewa mafunzo rahisi.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako