• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mvuto wa mlima Jinggang

    (GMT+08:00) 2009-08-03 16:20:25

    Wageni wa nchi za nje wenye shauku juu ya historia ya China, wanaona mlima Jinggang ni mahali pa mapinduzi, hayati Mao Zedong aliongoza watu wa China kujenga kituo cha mapinduzi huko kabla ya miaka zaidi ya 80 iliyopita, na hatimaye kupata ushindi wa mapinduzi. Lakini kwa kweli Mlima Jinggang licha ya kuwa ni kituo cha mapinduzi, vilevile ni sehemu yenye utamaduni wa kung'ara na historia ndefu, na hivi sasa sehemu hiyo imejengwa kuwa bustani ya msitu ya taifa. Watu wanaona baridi na furaha mara tu baada ya kuingia kwenye maeneo ya mlima Jinggang. Huko kuna mandhari nzuri, msitu mnene, mlima mrefu, mabonde makubwa, maporomoko ya maji, mapango ya mawe na mawingu meupe. Wanyama na mimea wanaishi kwa kutegemeana, binadamu wanaishi katika hali ya kupatana na mazingira. Mandhari nzuri ya mlima Jinggang yanavutia sana watalii kutoka sehemu mbalimbali. Bw. Feng Shuyi kutoka sehemu ya kaskazini mashariki ya China alisema"Naona hapa ni sehemu inayopendeza sana, milima na mito ni mizuri sana, wakazi ni wapole, hakuna viwanda vingi, na mazingira ya asili ya hapa yamehifadhiwa vizuri."

    Mlima Jinggang ulioko sehemu ya kusini magharibi ya mkoa wa Jiangxi uko katika sehemu ya kati ya mlima Luoxiao ulioko kwenye sehemu ya kusini ya China. Sehemu muhimu yenye mandhari nzuri ni kiasi cha kilomita za mraba 260.

    Mazingira ya mlima Jinggang ni ya kuvutia sana, hewa ya huko ni safi, ambayo katika kila centimita za ujazo kuna oxygen ions hasi zaidi ya 8,000, hata kuna zaidi ya 12,000 katika baadhi ya sehemu, hivyo watu wanapaita ni "baa ya oksijin ya kimaumbile". Huko hakuna vitu vinavyotolewa ambavyo vinachafua mazingira ya asili wala hakuna makelele, 86% ya ardhi ya huko ni misitu, na mazingira ya ikolojia yanafikia ngazi ya kwanza ya kitaifa na ni mahali pazuri sana kwa utalii, kukwepa joto na kupumzika, kila ifikapo kipindi cha majira ya joto, kuna idadi kubwa ya watalii wanaokwenda huko kupumzika.

    Ukilinganishwa na nchi na sehemu nyingine, mlima Jinggang unavutia watu zaidi kutokana na hali yake nzuri ya hewa. Mwongoza watalii Bw. Zhao Wu alisemaļ¼š"Mlima Jinggang una misitu mikubwa ya miti yenye majani makubwa, ambayo hayapukutiki hata katika majira ya baridi, na ni ya kipekee katika bara la Asia.

    Mlima Jinggang sasa ni hifadhi ya maumbile ya ngazi ya taifa na umeorodheshwa katika "hifadhi ya eneo la binadamu na viumbe". Huko panaitwa kuwa ni "bustani ya wanyama na mimea ya kimaumbile" na "ghala la hazina ya kijani". Maendeleo hayo yanahusiana sana na kuinuka kwa wazo la kuhifadhi mazingira la wakazi wa sehemu ya mlima Jinggang.

    Mtalii kutoka Yingde, mkoani Guangdong Bi. Hong Mei alifurahishwa sana na juhudi za watunza usafi wa mazingira wa huko. Alisema: "Nimefurahishwa sana na juhudi za watunza usafi wa mazingira wa sehemu hiyo, kwani wao wanafanya kazi hata kama ni saa 4 na nusu usiku wanaokota takataka kwa mikono. Kutunza usafi wa mazingira hapa ni kazi ngumu, kwani kuna idadi kubwa ya watalii kila siku."

    Kutunza usafi wa mazingira hakutekelezwi na wafanyakazi wanaofanya usafi tu, bali hata wakazi wa kawaida na wafanyakazi wa sehemu nzima ya vivutio wamekuwa na desturi ya kuokota takataka kila wanapoona takataka chini. Alisema: "Sisi sote hapa tunatakiwa kutunza usafi wa mazingira, kwani watalii wanakuja kwa wingi. Na kama wewe unaambiwa uende kwenye mahali pachafu, naona hakika hutakubali kwenda."

    Pamoja na kuinuka kwa wazo la watu la kuhifadhi mazingira ya asili, mazingira ya sehemu nzima yanaboreshwa na hewa inakuwa safi siku hadi siku. Watu wote wanahifadhi ulingano wa mfumo wa viumbe wa huko.

    Wakazi wa sehemu ya Mlima Jinggang wanajitahidi kuhimiza maendeleo ya mwafaka ya shughuli za utalii na mazingira ya viumbe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako