• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tehran-Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran aapishwa

    (GMT+08:00) 2009-08-05 19:06:07

    Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 5 ameapishwa kwenye bunge la Iran, ambapo ameanza kutumikia kipindi chake cha pili urais wa Iran.

    Sherehe ya kuapishwa kwa rais Ahmadinejad imefanyika katika ukumbi wa bunge la Iran, na spika wa bunge la Iran Bw. Ali Larijani aliendesha sherehe hiyo, mkurugenzi mkuu wa idara ya utekelezaji wa sheria ya Iran Ayatollah Mahmoud Hashemi Shahroudi, mwenyekiti wa kamati ya usimamizi na ulinzi wa katiba ya nchi hiyo Ayatollah Ahmad Jannati, maofisa wengine waandamizi na mabalozi wa baadhi ya nchi nchini humo walihudhuria sherehe hiyo.

    Baada ya kuapishwa, rais Ahmadinejad alitoa hotuba akieleza kwa ufupi sera za serikali mpya ya Iran kuhusu mambo ya nchini na za nchi za nje, na kutoa mwito wa kuwataka watu wa sekta mbalimbali za nchi hiyo walinde utulivu wa taifa na kujitahidi kushiriki kwenye ujenzi wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako