• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing imezidi kuwa nzuri baada ya Michezo ya Olimpiki

    (GMT+08:00) 2009-08-13 16:26:43

    Mwaka mmoja umepita tangu Michezo ya Olimpiki ya Beijing ifanyike, ingawa mashindano makali yamepita, lakini mabadiliko makubwa yaliyoletwa na michezo ya Olimpiki kwa Beijing hayakuacha kutokea kutokana na kumalizika kwa Michezo ya Olimpiki. Katika mwaka uliopita baada ya michezo ya Olimpiki, wageni wengi wanaoishi mjini Beijing wameona kihalisi mabadiliko makubwa ya Beijing.

    Bw. Ahmad Abuzeid anatoka Misri, na amefanya kazi mjini Beijing kwa miaka mitano. Kabla ya hapo, aliwahi kutembelea miji mingi duniani. Alisema,

    "Beijing ni mji mzuri zaidi kuliko miji mingine mingi duniani. Ni mji mzuri, tena ni wa usafi, eneo lake la majani ni kubwa, na utaratibu wa mji pia ni mzuri."

    Kwa kuwa alikuwa na kazi nyingi wakati wa michezo ya Olimpiki ya mwaka jana, hakuenda kutazama mashindano. Lakini baadaye alikwenda mara kadhaa kwenye bustani ya Olimpiki na uwanja wa michezo wa taifa "kiota" na jumba la kuogelea, na kupiga picha nyingi. Alisema kuwa, hii ni kumbukumbu nzuri kwake, na baada ya kurudi nchini Misri, atawaambia jamaa na marafiki zake. Alipozungumzia mabadiliko yaliyoletwa na michezo ya Olimpiki kwa Beijing, alisema,

    "Zamani nilipanda mabasi ambayo yalikuwa machakavu, hali kadhalika kwa subway, na mawasiliano ya barabarani pia yalikuwa na matatizo fulani. Lakini baada ya michezo ya Olimpiki, tunatumia basi ya kisasa, hata kuna skrini mbili kwenye basi. Barabara pia zimekuwa nzuri, na njia za subway zimekuwa nyingi zaidi."

    Pia alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, anajua kuwa serikali ilitenga fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo. Hakika mabadiliko hayo makubwa yamechangiwa juhudi za watu wote wa China.

    Licha ya mabadiliko hayo halisi, Bw. Ahmad pia ameona mabadiliko ya maisha na mienendo ya watu wa Beijing. Bw. Ahmad alisema, Wachina wana urafiki lakini wait wengi hawaoneshi hisia wazi wazi, lakini kabla ya michezo ya Olimpiki, kulikuwa na vipindi mbalimbali vya televisheni vilivyowafundisha watu kuonesha uchangamfu na ukarimu zaidi, hasa kwa watalii wageni.

    Bw. Antonio Lagala ni Mfaransa, alifanya kazi katika vyombo vya habari mjini Beijing kuanzia mwaka jana. Aliona kuwa, mali kubwa ya urithi wa michezo ya Olimpiki kwa Beijing ni kuboreshwa sana kwa sifa yaa hewa. Alisema,

    "Hali ya hewa mjini Beijing ilikuwa nzuri wakati wa michezo ya Olimpiki, kwa sababu kila siku magari yaliendeshwa kwa kufuata shufaa na witiri ambapo nusu ya magari yaliendeshwa barabarani. Ingawa sasa magari mengi yanaruhusiwa kuendeshwa, lakini ikilinganishwa na hali ya kabla ya michezo ya Olimpiki, hali ya hewa imeboreshwa sana. Naona hii ni umali kubwa ya rithi muhimu wa michezo ya Olimpiki kwa wakazi wa Beijing."

    Baada ya kufungwa kwa michezo ya Olimpiki, Beijing ilisimamisha kutekeleza hatua ya muda ya kuendesha magari kwa kufuata namba shufwa na namba witiri, lakini kila siku asilimia 20 ya magari hayawezi kuendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Bibi Albertina Knezevic anayetoka Croatia, ambaye amefanya kazi hapa Beijing kwa miaka minne, alisema,

    "Kwa sisi bila shaka hili ni jambo zuri, naunga mkono hatua hiyo.China inafanya kazi nyingi za kuhifadhi mazingira, hasa katika mji mkubwa kama Beijing. Naona anga ya Beijing ni ya buluu, na hali ya hewa ya Beijing ni nzuri."

    Kuhusu mabadiliko ya Beijing baada ya michezo ya Olimpiki, Bibi Albertina alisema, utamaduni wa michezo unawafanya watu wote wazee kwa watoto mjini Beijing wapende zaidi michezo. Alisema,

    "Ustawi wa utamaduni wa michezo ni moja ya mabadiliko makubwa yaliyotokea baada ya michezo ya Olimpiki. Ingawa utamaduni wa China wenye historia zaidi ya elfu moja umekuwa na utamaduni wa michezo, lakini utamaduni huo unatakiwa kuendelezwa zaidi . Michezo ya Olimpiki imeleta moyo mpya wa michezo kwa watu wote vijana na wazee. Unaweza kuona watu wengi wanaofanya mazoezi ya kujenga afya, na kutumia vifaa vya michezo."

    Bibi Albertina alisema, kutumia tena kwa majengo ya michezo ya Olimpiki pia ni sehemu moja ya utamaduni wa michezo. Muda mfupi uliopita, jumba la kuogelea la taifa limefunguliwa kwa watu, na watu wanaweza kuogelea pale kwa Yuan 50. Bw. Ahmad alisifu hatua hiyo, anaona kuwa baada ya mashindano, majengo ya michezo ya Olimpiki yanapaswa kuwa sehemu ya kuwafanya watu wa kawaida wafurahie michezo.

    Uwanja wa michezo wa taifa "kiota" uliandaa mashindano ya mpira wa soka wa Kombe la Italia na maonesho mbalimbali, ili uwanja huo utatumiwa zaidi. Bw. Antonio alieleza matumaini yake kuwa, mapato hayo yatatumika katika shughuli za kuwasaidia watu wenye shida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako