• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya China na Afrika vyajadiliana kuhusu kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao

    (GMT+08:00) 2009-08-14 15:04:41

    Kongamano la wanahabari la Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lililoandaliwa kwa pamoja na ofisi ya habari ya baraza la serikali la China na wizara ya mambo ya nje ya China lilifanyika hapa Beijing tarehe 15 mwezi Julai. Maofisa wa habari wa serikali na waandishi wa habari kutoka nchi 24 za Afrika na wajumbe wa vyombo 9 vya habari vya China vikiwemo Shirika la habari la China Xinhua, gazeti la Renminribao na Radio China Kimataifa walihudhuria kongamano hilo, ambapo walijadiliana kuhusu kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya vyombo vya habari, na kuzidisha urafiki wa jadi kati ya China na Afrika.

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhai Jun ambaye alihudhuria kongamano hilo alisema, ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na vya Afrika unazisaidia nchi zinazoendelea kuongeza sauti yao katika mawasiliano ya habari duniani. alisema,

    "Mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya habari ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika, bali pia ni sehemu muhimu ya mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika, si kama tu kunaweza kuimarisha maelewano na urafiki, bali pia kunazisaidia nchi zinazoendelea kuongeza sauti yao duniani. Idara za usimamizi wa habari na vyombo vya habari vya China na nchi za Afrika zikipashana habari, kuhimiza ushirikiano wa aina mbalimbali, na kutumia kwa pamoja raslimali za habari, tutaweza kufanya sauti yetu isikike, na kuonesha sura za China na Afrika, na ushirikiano kati yao. "

    Ikiwa ni radio pekee inayotanga kwa nchi za nje nchini China, Radio China Kimataifa inaendelea kujulikana barani Afrika siku hadi siku. Radio China Kimataifa inafanya juhudi kufanya ushirikiano na vyombo vya habari vya nchi za Afrika. Mkurugenzi wa idara ya matangazo ya Asia Magharibi na Afrika ya Radio China Kimataifa Bi. Yu Kuan alisema,

    "China ni nchi inayoendelea, na China na nchi za Afrika zina historia inayofanana, pia zina mahitaji ya pamoja katika kujiendeleza na kufanya ujenzi wa nchi. Hivyo radio yetu inaonesha sauti ya nchi zinazoendelea na kulinda maslahi yao, radio yetu ni rafiki wa nchi zinazoendelea zikiwemo nchi za Afrika, tunafanya juhudi katika kuhimiza utulivu wa jamii, masikilizano ya watu, na mawasiliano na maendeleo kati ya nchi zenye utamaduni tofauti. "

    Bi. Yu Kuan alijulisha hali ya ushirikiano kati ya Radio China Kimataifa na vyombo vya habari vya nchi za Afrika. Alisema,

    "Tunarusha matangazo yetu hewani katika nchi za Afrika kwa lugha 6 zikiwemo lugha ya Kiswahili, Kihausa, na Kiarabu, ili kuwajulisha wasikilizaji hali halisi ya China, na kuonesha urafiki kati ya China na Afrika, na matumaini na jitihada za China na Afrika katika kuhimiza ushirikiano wa kirafiki kati yao. Tumeanza ushirikiano na vyombo vya habari vya Afrika, kwa mfano tumeanza kubadilishana vipindi, na kuanzisha vituo vya radio za huko. Tumefungua radio ya FM mjini Nairobi, ambayo inapendwa na wasikilizaji wetu wa huko. Pia tunafanya ushirikiano na TBC na STZ nchini Tanzania, tumeanzisha darasa la Confucius kwenye radio yetu ili wasikilizaji wetu barani Afrika waweze kujifunza lugha ya Kichina na kuelewa utamaduni wa China.

    Waandishi wa habari kutoka China na Afrika kwenye kongamano hilo walisema, vyombo vya habari vya pande hizo mbili vina historia ndefu ya ushirikiano, katika hali mpya, ni lazima kufanya juhudi kutafuta njia mpya ya ushirikiano.

    Mhariri mkuu wa kundi la magazeti la Kenya Bw. Joseph Otindo alitoa mapendekezo yake kuhusu kuimarisha zaidi mawasiliano na ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika.

    Mwaka 2006 mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ulifanyika kwa mafanikio hapa Beijing. Kwa niaba ya serikali ya China, rais Hu Jintao kwenye mkutano huo alitangaza hatua nane za kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika na kuunga mkono maendeleo ya Afrika. Uhusiano kati ya pande hizo mbili unaendelezwa kwa kasi. Uhusiano kati ya vyombo vya habari vya pande hizo mbili ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, na ushirikiano kati yao pia ni mradi muhimu wa ushirikiano chini ya mfumo wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Mwezi Novemba mwaka huu, mkutano wa 4 wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika huko Sharmd Shekh nchini Misri. Mkutano huo utatathimini hali ya utekelezaji wa hatua zilizotangazwa kwenye mkutano wa wakuu wa baraza hilo uliofanyika hapa Beijing, na kutunga mpango wa ushirikiano katika miaka mitatu ijayo. Huu ni mkutano wa kwanza wa mawaziri tangu mkutano wa wakuu wa baraza hilo ufanyike hapa Beijing, ambao ni muhimu sana kwa China na Afrika katika kukabiliana kwa pamoja na msukosuko wa fedha duniani, kuhimiza kutimiza utekelezaji wa malengo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, na kuimarisha uhusiano mpya wa kiwenzi wa kimkakati.

    Vyombo vya habari vya China na Afrika vitaendelea kuonesha umuhimu wake, ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza urafiki wa jadi na ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako