• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeniachia kumbukumbu nyingi

    (GMT+08:00) 2009-08-21 16:43:05

    Wasikilizaji wapendwa, karibuni katika kipindi hiki cha daraja la Urafiki kati ya China na Afrika. Leo kwenye kipindi hiki tunawaletea maelezo kuhusu "Kumbukumbu ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing" na "Utamaduni wa China unavyosaidia kubadilisha maisha ya watoto yatima barani Afrika".

    Ni mwaka mmoja sasa umepita toka Michezo ya Olimpiki ya Beijing ifunguliwe. Michezo hiyo imewaachia mamilioni ya wachina kumbukumbu isiyosahaulika, pia imewaachia wageni wengi kumbukumbu nyingi. Kutokana na mwaliko wa kituo cha habari cha kimataifa cha Beijing 2008, mkurugenzi wa idara ya habari za michezo ya gazeti la "Sunday Mail" la Zimbabwe Bw. Goodwill Zunidza mwaka jana alifanya ziara nchini China mara mbili, na kukusanya habari katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Hivi karibuni Bw. Goodwill alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alikumbusha kuhusu aliyoyaona katika kipindi hicho akisema, haitasahau Michezo ya Olimpiki ya Beijing na michezo hiyo imemwachia kumbukumbu nyingi.

    Bw. Goodwill ni mkurugenzi wa idara ya habari za michezo ya gazeti la "Sunday Mail" la Zimbabwe. Mwaka jana alikuja kuripoti Michezo ya Olimpiki hapa Beijing mara mbili. Alipozungumzia kumbukumbu zake alipokuwa hapa Beijing, alikuwa na furaha akisema,

    "Nataka kusema Michezo ya Olimpiki ya Beijing imeniachia kumbukumbu nyingi. Nilipofika hapa Beijing nilishangazwa na ukubwa wa michezo hiyo. Niliona huu ni mji mkubwa zaidi duniani. Nimeiona miji ya New York, Washington na London kwenye TV au flamu, sijawahi kufika kwenye miji hiyo lakini naona haiwezi kulingana na Beijing katika ukubwa, vivutio na ujenzi wa miundo mbinu. "

    Zimbabwe bado si nchi tajiri , na gazeti la "Sunday Mail" ni gazeti kubwa zaidi nchini Zimbabwe, lakini halina uwezo wa kumtuma mwandishi wake wa habari kuja Beijing kuripoti Michezo ya Olimpiki. Bw. Goodwill anaona ana bahati sana, kwa sababu kituo cha habari cha kimataifa cha Beijing 2008 kilichoanzishwa na serikali ya Beijing mwaka jana kilimlipia gharama zote ili aweze kuja kukusanya habari katika michezo hiyo. Alisema,

    "Hii ni mara yangu ya kwanza kuripoti Michezo ya Olimpiki. Si rahisi kupata fursa ya kushiriki kuripoti Michezo hiyo katika nchi yetu. Gazeti letu halijawahi kutuma waandishi wa habari kuripoti Michezo ya Olimpiki. Lakini mwaka jana China ilitupatia saada kubwa sana, kwa hiyo niliweza kuja hapa kuripoti michezo hiyo. Zamani waandalizi wa michezo ya Olimpiki hawakufikiria kutoa fursa kwa nchi zisizoweza kutuma waandishi wa habari kuripoti michezo hiyo, lakini China ilikuwa imefikiria suala hilo na kutoa mpango kamili uliowapa waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika fursa ya kuripoti Michezo ya Olimpiki nchini China."

    Katika kipindi ambacho alikuwa mjini Beijing, Bw. Goodwill alitazama ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, pia alishiriki kuripoti michezo mingi ambayo awali hakuijua sana. Na watu wanaojitolea wenye uchangamfu wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing na viwanja vikubwa na majumba makubwa ya michezo pia vilimpa picha nzuri sana. Alisema,

    "Baada ya kurudi nchini Zimbabwe, niliandika makala yenye kichwa cha "Hii ni michezo mitukufu zaidi" nikimnukuu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya kimataifa. Hata mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Uingereza alitambua kuwa si rahisi kufanya vizuri zaidi kuliko Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Naona kulikuwa na watu wanaojitolea milioni 1 hivi nje na ndani ya viwanja, ukitaka kuuliza njia au jambo lolote watakusaidia. Pia jumba la michezo ya kuogelea linavutia sana, na wachezaji wengi walivunja rekodi kutokana na maandalizi mazuri ya wachina."

    Aidha, Bw. Goodwill alisema kitu ambacho hatakisahau kuhusu Michezo hiyo ni uchangamfu na ukarimu wa wachina. Alisema,

    "Wachina ni watu wema sana, wao ni marafiki, wachangamfu na wakarimu na wanaopenda kuwasaidia wengine. Wachina wameelimika vizuri na wanajiamini, hawaigi utamaduni wa nchi za nje, bali wanathamini utamaduni wao."

    Alipokumbusha hali ya mwaka jana, Bw. Goodwill anaona safari yake nchini China ni mali yake katika maisha, Safari hii imezidisha ufahamu wake juu ya michezo pia imemfahamisha utamaduni wa China. Alisema,

    "Safari hiyo ilifumbua macho yangu, niliweza kufahamu michezo kutoka pande mpya. Naona hata nimeleta utamaduni nchini Zimbabwe, utamaduni wa China unaisaidia sana kwenye kazi yangu. Kuendelea kujifunza utamaduni wa China kutaongeza ufahamu wangu katika michezo. Kwa jumla, safari hiyo mjini Beijing imeinua ufahamu wangu wa michezo, nina matumaini kuwa nitashiriki kwenye kuripoti michezo mingi zaidi katika siku za baadaye."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako