• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ala ya muziki ya Tsuur ya tawi la Tuvas la kabila la Wamongolia

    (GMT+08:00) 2009-08-27 17:39:50

    Watuvas ni wa tawi la kabila la Wamongolia ambalo idadi ya watu zaidi ya 2,000, watuvas hasa wanaishi katika misitu na milima mikubwa iliyoko sehemu ya kaskazini ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur. Kuhusu chimbuko latawi hilo la Wamongolia, baadhi ya wasomi wanaona kuwa, watuvas ni watoto wa vizazi vya baadaye ya askari wa mfalme maarufu wa Mongolia Genghis Khan waliovamia sehemu ya magharibi karibu miaka 800 iliyopita, ambapo wengine wanasema mababu zao ni watu waliohamia sehemu hiyo kutoka Siberia miaka 500 iliyopita. Watuvas bado wanaishi maisha ya jadi, na wanategemea ufugaji na uwindaji. Watu hao wanapenda kutumia ala moja ya jadi ya muziki iitwayo Tsuur, sauti ya ala hiyo ni ya chini na taratibu, pia sauti yake inavutia masikioni mwa watu.

    Nyasi za mbuga ya mlima Altai hustawi mwezi Mezi kila mwaka. Mbuga hiyo ina nyasi za Zalaat ambazo zinatumika kutengeneza ala ya muziki ya Tsuur, wafugaji wanapotengeneza ala hiyo wanachuma bua la unyasi, halafu wanavitoa vitu ndani na kutoboa matundu matatu, na kulitengeneza kuwa ni ala ya muziki ya Tsuur. Baada ya kufanya uchunguzi, wataalamu wanaohusika wanaona kuwa, Tsuur ina historia zaidi ya miaka 1,600, na ilijulikana kama ni Hujia katika zama za kale. Lakini kulikuwa na Mujia za aina mbalimbali, na Tsuur ni moja kati yao. Kuhusu chimbuko la ala ya Tsuur, watuvas wana hadithi moja nzuri. Bw. Taivan ambaye ni mtuvas alisema, "Siku moja mfugaji mmoja wa Tuvas alikuwa akichunga mifugo yake mbugani. Wakati upepo ulipovuma, alisikia mlio wa sauti nzuri. Mtuvas huyo alitafuta tafuta mpaka akagundua kuwa mlio huo ulitokana na unyasi wa Zalaat, ambao bua lake lilikuwa wazi, unyasi huo unatoa mlio mwororo wakati upepo unapovuma. Hivyo alichuma mabua ya nyasi na kwenda nayo nyumbani akitaka kuyatengeneza kuwa ala ya muziki. Hatua kwa hatua, mfugaji huyo alivumbua ala ya Tsuur. Kwanza alijaribu kuitoboa Tsuur matundu 10, na baadaye 5 na hatimaye 3, na aligundua kuwa Tsuur yenye matundu matatu inaweza kutoa sauti nzuri zaidi."

    Tsuur ni bomba lenye urefu wa sentimita 66 na upana kama kidole gumba cha binadamu. Ingawa ina matundu matatu tu, lakini inaweza kutoa sauti 5 au 6 tofauti. Bw. Taivan aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, kimsingi Tsuur si chombo cha kuwaburudisha watu, bali ni njia ya watuvas ya kuwasiliana na dunia ya kimaumbile. Alisema, "Zamani tulipokuwa tunachunga mifugo, tuliwapigia Tsuur ng'ombe na kondoo tuliofuga na wanyama wa porini, hata wanyama hao waliacha kula nyasi, wakasikiliza muziki tuliopiga."

    Bw. Taivan alisema sauti zinazotoka kwenye Tsuur zote zinahusu dunia ya maumbile, kama vile sauti ya mawimbi ya ziwa Kanas na sauti za ndege wa aina mbalimbali. Ala hiyo ya muziki hupigwa wakati wa sikukuu, kwenye harusi, wakati wa kuchunga mifugo na kufanya mikutano ya umma.

    Lakini ustadi wa kupuliza Tsuur ulikuwa unakabiliwa na hatari ya kutoweka. Kutokana na maendeleo ya shughuli za utalii, watuvas wanawasiliana zaidi na watu wa nje siku hadi siku, hivyo kuwafanya vijana wengi kutojua namna ya kupiga ala hiyo. Hayati mzee Evdes alikuwa mrithi wa mwisho aliyekuwa hodari sana katika kupiga ala ya Tsuur,

    Wapendwa wasikilizaji, mliyosikia ni rekodi ya muziki ya Tsuur uliopigwa na Bw. Evdes miaka mitatu iliyopita. Bw. Evdes alikuwa mtu maarufu kati ya watuvas. Watalii kutoka sehemu mbalimbali wanapotembelea sehemu ya Kanas, wanakwenda nyumbani kwake ili kusikiliza muziki wa Tsuur aliopiga vizuri. Lakini kwa bahati mbaya watoto watatu wa Bw. Evdes wote hawapendi kupiga ala ya Tsuur, na hali hii inamsikitisha sana. Mtoto wake mkubwa alifanya kazi ya ufugaji, na mtoto wa tatu ni mdogo sana, hivyo anapenda kupanda farasi tu, na mtoto wake wa pili Bw. Munkh ndiyo chaguo lake pekee. Bw. Munkh alisema, "Baba yangu alirithi muziki uliopigwa kwa ala ya Tsuur. Alinitaka nami nijifunze kupiga ala hiyo ya muziki, ili niwabunrudishe wageni kutoka sehemu mbalimbali. Mwanzoni nilikataa, lakini baba yangu alisema ni lazima mmoja kati yetu ajifunze kupiga ala ya Tsuur, na mwishoni alinichagua mimi. Sasa ninamshukuru sana baba yangu."

    Hivi sasa ni miaka 10 imepita tangu Bw. Munkh ajifunza kucheza Tsuur kwa miaka 10, na hivi sasa anaweza kupiga muziki kwa ala hiyo ya muziki. Kutokana na maendeleo ya utalii katika sehemu ya Kanas, watu wengi zaidi siku hadi siku wameanza kufuatilia watuvas na muziki wa Tsuur, na mara kwa mara watalii wanakwenda nyumbani kwa Bw. Munkh kusikiliza muziki anaopiga. Bw. Munkh alisema, "Nimejifunza kupiga ala ya Tsuur kwa miaka 10. Ala ya tsuur ni utamaduni wetu wenye historia ndefu, ambapo baba yangu alikuwa mpigaji hodari zaidi wa ala ya Tsuur. Hivyo ni lazima mimi nirithi ustadi wake. Katika miaka 10 iliyopita, nilifanya mazoezi kila siku, na sasa nimefanikiwa. Sasa nina matumaini ya kupiga muziki kwa ala ya Tsuur kwa kuwaburudisha wageni wa kimataifa, kwani muziki huo ni wa jadi kwa sisi watuvas."

    Hapo kabla baada ya mzee Evedes kufariki dunia, baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi kuwa ustadi wa kupiga ala ya Tsuur huenda utatoweka, lakini hivi sasa, mbali na Bw. Munkh, vijana wengi wa Tuvas wameanza kujifunza kupiga ala ya Tsuur, na tunaimani kuwa utamaduni huo wa jadi wa watuvas utarithshwa kizazi baada ya kizazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako