• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bonde la mawe mekundu la mlima Yuntai

    (GMT+08:00) 2009-08-31 16:39:54

    Sehemu yenye mandhari nzuri ya mlima Yuntai iko kwenye wilaya ya Xiuwu, mkoani Henan, sehemu ya kati ya China. Sehemu hii yenye eneo la karibu kilomita za mraba 200 na umaalumu wa sura ya ardhi ya mabonde ni ya kundi la kwanza la bustani za jiolojia zilizothibitishwa na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Watalii wanapofika kwenye sehemu hii, wanapelekwa kwa mabasi hadi kwenye bonde la mawe mekundu, mawe ya huko ni ya rangi ya zambarau jinsi ilivyo ni kama yalipasuliwa kwa mapanga na mashoka. Mwongoza watalii, Bi. Lu Ziting alisema,

    "Mawe ya hapa yana madini mengi ya chuma na madini ya aina nyingine, hivyo magenge yote ya milima ya hapa yana rangi ya zambarau."

    Mara tu baada ya kuingia kwenye sehemu hiyo, kuna daraja moja la mawe, watu wakisimama kwenye daraja hilo wanaweza kuona mandhari yote ya bonde la mawe mekundu. Na kama mtu akisogea karibu, ataona mawe ya bonde hilo si laini, bali yana mistari iliyochorwa na maji ya mto. Bi. Lai ambaye anafanya kazi katika sekta ya utalii huko Hong Kong, aliwahi kuona mandhari ya milima na mito ya sehemu nyingi za kusini, lakini alivutiwa na mandhari ya bonde la mawe mekundu, akisema

    "Mandhari ya mlima Yuntai ni nzuri, na ni tofauti na ya sehemu nyingine, hapa kuna milima mingi, pande zote ni milima, baada ya kurudi nitafikiria namna ya kuendeleza shughuli za utalii."

    Kivutio cha Danya ni genge la mlima la rangi nyekundu, ambalo ni kama bonde la ufa lenye urefu wa zaidi ya mita 600.

    Kama ukienda mbele kwa kufuata handaki la pale, inaweza kusikika sauti ya maji ya maporomoko ya maji ya dragon mweupe, ambayo ni moja ya maporomoko ya maji maafuru kwenye bonde la mawe mekundu, maji yake yanaingia kwenye bwawa. Baada ya kutoka kwenye handaki kuna njia moja iliyotandikwa vipande vya mawe, licha ya kusikia sauti ya maji yanayotiririka, watu pia wanaweza kuona maua meupe kwenye genge la mlima karibu na maporomoko ya maji, mwongoza watalii, Bi. Lu Ziting alisema,

    "Maua yale ni chrysanthemum, ambayo ni moja ya aina nne maarufu za dawa za miti-shamba za sehemu ya Jiaozuo. Maua hayo yanaota kwenye magenge ya mlima, na ni dawa nzuri ya kutibu ugonjwa wa hali ya mwili kupata joto."

    Baada ya kupita maporomoko ya maji ya dragon mweupe, hewa inakuwa baridi kidogo mara moja, hivyo wakazi wa huko wanaiita kuwa bonde la Wenpan. Kwani sehemu finyu zaidi kwenye bonde hilo ni yenye upana wa mita 2 hadi 3 hivi, hewa joto ya nje haiwezi kuingia ndani ya bonde kwa urahisi, hivyo hewa ya ndani ya bonde hilo ni ya nyuzi 20 hivi kwa mwaka mzima. Kwa hiyo wakazi wa huko pia wanaliita bonde hilo kuwa ni "bode la changchun" yaani ni majira ya Spring kwa mwaka mzima.

    Mawe yaliyoko kwenye bonde hilo mengi ni ya rangi nyekundu, mawe ya chokaa inayoning'inia ni nadra kuonekana, lakini mawe yaliyoko ndani ya pango moja ni ya chokaa. Mawe hayo yanamulikwa na mwanga wa taa wa rangi nyekundu yanakuwa kivutio cha kupendeza sana. Madini ya Calcium carbonate yaliyomo ndani ya maji yaliyopo kwenye matabaka ya mawe ya bonde la mawe mekundu, yanadondokea kwenye jiwe hilo, baada ya miaka mingi yanakuwa kama chokaa inayodondoka. Jiwe moja lililoko kwenye sehemu ya juu ya pango likionekana kama limetundikwa huko linaitwa "jiwe lililotundikwa la miaka elfu moja iliyopita" linaonekana kama linaangalia maisha ya watu. Bi. Lu Ziting alisema,

    "Wenyeji wa hapa wanaliita jiwe kuwa ni jiwe la kupima moyo, wavulana na wasichana wanaochumbiana wanafika hapa kupima udhati wa mioyo yao, endapo mtu akisema uwongo, vipande vidogo vya mawe vilivyoko karibu na jiwe hilo vitaanguka. Hili ni tarajio la wenyeji wa huko kuhusu mapenzi ya kweli."

    Mbali na hayo, bonde la mawe mekundu lina vivutio vingi ikiwa ni pamoja na maporomoko ya maji yanayoangukia moja kwa moja chini ya bonde hilo kutoka kwenye sehemu ya juu ya genge la mlima. Poromoko la maji lililoko kubwa zaidi kwenye sehemu ya bonde la mawe mekundu ni poromoko la maji linaloitwa kichwa cha dragon, huko kuna maji mengi tena yanatoka juu sana, maji yake yanaanguka chini kwa kasi na kwa wingi, na kuonekana yanaitikiana na maji ya poromoko la maji la dragon mweupe yaliyoko mbali. Maporomoko mengi ya maji yanawafurahisha sana watalii. Bw. Yang kutoka Shanghai alisema,

    "Hapa ni mahali pazuri sana, nimetembelea kwenye sehemu nyingi za China, bonde kubwa la mlima Yuntai ni la kipekee, lina mazingira ajabu ya kijiografia pamoja na mawe ya aina mbalimbali yanayotufurahisha sana, tena kuna maporomoko ya maji na vijito, ni mandhari maalumu ya mlima Yuntai, ambayo sehemu nyingine haziwezi kulingana nayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako