• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China"-Nyimbo za Jadi Wilayani Dangtu katika mkoa wa Anhui China

    (GMT+08:00) 2009-08-31 16:41:03

    Wilaya ya Dangtu iliyoko kwenye ukingo wa Mto Changjiang mkoani Anhui, mashariki mwa China, inasifiwa kuwa ni "Bahari ya Nyimbo za Wenyeji". Nyimbo za Dangtu maana yake ni nyimbo za aina zote za jadi zinazoenea miongoni mwa wenyeji wa wilaya hiyo, mambo yanayoimbwa kwenye nyimbo hizo ni kuhusu maisha kwenye jamii. Kwa mujibu wa kumbukumbu za historia, nyimbo za jadi katika wilaya hiyo zilianza mwaka 220, nyimbo zenyewe ni za jadi ambazo zilitungwa na wenyeji wa huko, zinafundishwa uso kwa uso na kuimbwa kizazi kwa kizazi hadi hivi leo. Hivi sasa nyimbo za huko Dangtu zimechaguliwa kuwa urithi wa utamaduni usioonekana wa China, hali kuhusu nyimbo na waimbaji zimekusanywa pamoja na kutunzwa na serikali.

    Mliosikia ni wimbo uitwao "Mbegu za Mayungiyungi" ulioimbwa na mkulima Tao Xiaomei. Bibi Tao Xiaomei ana umri wa miaka 30. Siku moja ya mwaka 2004, Bi. Tao Xiaomei alipokuwa akicheza ngoma pamoja na wenzake aliimba wimbo huo bila kuweza kujizuia, uimbaji wake mzuri wa wimbo huo uliwavutia watu wote waliokuwepo, baadaye alipendekezwa ashiriki kwenye mashindano ya taifa ya waimbaji wakulima. Katika mashindano hayo alipata tuzo ya pili kwa kuimba wimbo huo. Bi. Tao Xiaomei alikulia katika mazingira ya nyimbo za jadi, kwa hiyo anapenda sana kuimba toka alipokuwa mtoto. Alisema,

    "Nilipokuwa mtoto wazazi wangu walikuwa wanapenda kuimbaimba walipokuwa wanalima mashambani, nami nilikuwa nacheza huku nikiwasikiliza, baadaye nikajua kuimba."

    Kutokana na mazingira tofauti ya kimaisha, kuna nyimbo za aina nyingi na mambo mengi yanayoimbwa, nyimbo hizo ni pamoja na nyimbo za kupiga makasia, za uvuvi, za kucheza ngoma na nyimbo za kuulizana maswali na kujibizana. Mtaalamu wa nyimbo za Dangtu Bw. Xu Jiazhen alisema,

    "Uimbaji wa nyimbo hizo nyingi ni wa laini, nyimbo hizo nyingi zinahusu maisha ya wavuvi, na mitindo ya nyimbo ni ya aina mbalimbali, hii imeonesha vilivyo mvuto wa usanii wa wenyeji wa huko."

    Nyimbo za jadi katika wilaya ya Dangtu zimekuwa na historia ndefu, kumbukumbu kuhusu uimbaji wa nyimbo za Dangtu zilikuwepo mapema kabla ya miaka elfu mbili iliyopita, wakati huo mfalme aliyekuwa anajulikana kwa jina la Liu Song alisimamia kazi ya kuhariri kitabu kiitwacho "Nyimbo na Dansi za Nguo Nyeupe za katani". Mtaalamu Xu Jiazhen akijulisha alisema,

    "Wakati huo watu walioshiriki kwenye maonesho ya uimbaji wa nyimbo hizo walikuwa wanavaa nguo nyeupe za katani, hivyo nyimbo hizo zilipewa jina la 'Nyimbo na Dansi za Nguo Nyeupe za Katani'."

    Mliosikia ni wimbo uitwao "Kuchuma Majani ya Mforosadi" ulioimbwa na Xia Guichang. Mwimbaji huyo hivi sasa ana umri wa miaka zaidi ya 70, ni mmoja kati ya warithi watatu wa nyimbo za kienyeji za Dangtu, kuimba nyimbo kumekuwa desturi yake toka alipokuwa mtoto.

    Mliosikia ni "Wimbo wa Kushindilia Udongo". Kufuatia kuenea kwa matumizi ya mashine, hivi leo wakulima hawafanyi tena kazi za sulubu kama zamani, na kutokana na kuenea kwa televisheni na aina nyingine za burudani, wakulima hawakusanyiki tena pamoja na kuimba, hivyo nyimbo zao hazisikiki sana.

    Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, kazi za kukusanya nyimbo za jadi zilianza kushughulikiwa. Bw. Huang Xiyun ambaye alikuwa wa kwanza kabisa kufanya kazi hiyo alitembea kwa miguu kutoka kijiji kimoja hadi kingine akikusanya nyimbo, kazi ilikuwa ngumu sana. Mtaalamu Xu Jiazhen alisema,

    "Wakati wa mwaka 1951 na 1952, vyombo vya usafiri vilikuwa shida. Bw. Huang Xiyun alitembea peke yake kwa miguu katika vijiji vyote wilayani ili kukusanya nyimbo za jadi. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wilaya hiyo kukusanya nyimbo."

    Baada ya nyimbo za jadi za wilayani Dangtu kukusanywa kwa mara tatu hivi, sasa nyimbo hizo zimeenea. Licha ya kuoneshwa wilayani pia zinaoneshwa katika mikoa mingine na hata nchi za nje."

    Bi. Zhang Youzhen ambaye ni mzee anayeendesha hosteli moja kijijini mwake, ndani ya hosteli hiyo ametundika ukutani kibao kilichoandikwa: "Mwimbaji wa Nyimbo za Dangtu". Katika ua wa nyuma ya hosteli yake karibu na bwawa aliimba wimbo mmoja alioupenda sana toka alipokuwa kijana. Ingawa amekuwa na umri wa miaka 85, sauti yake nyororo inayosikika mbali bado inaonekana haiba yake ya kipekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako