• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mandhari nzuri ya mlima Lushan

    (GMT+08:00) 2009-08-31 16:38:39

    Mlima Lushan ni mlima maarufu ulioko kwenye mji wa Jiujiang, mkoani Jiangxi, sehemu ya kati ya China, mlima huu uko kwenye sehemu tambarare ya mtiririko wa kati na wa chini ya mto Changjiang na kando ya ziwa Boyang. Hali ya hewa ya huko ni ya milimani, na wastani wa halijoto ni kiasi cha nyuzi 22. Mlima Lushan uko kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 900 kutoka Shanghai, kufika kwenye mlima Lushan kutoka Shanghai kwa garimoshi inatumia saa 10 hivi.

    Sauti unayosikia ni ya maporomoko ya maji ya chemchemi ya Sandie, ambayo ni kivutio kikubwa zaidi kwenye sehemu ya mlima Lushan. Watu husema, "mtu haonekani kama ametembelea mlima Lushan kama hajafika kwenye chemchemi ya Sandie". Katika majira ya Spring, maji ya chemchemi yanaanguka chini mara tatu kutoka sehemu ya juu yenye urefu wa mita 155, hali hii inawafurahisha sana watu. Kila moja ya maanguko hayo matatu yana umaalumu wake, mtu akisimama chini kabisa na kuangalia sehemu ya juu, maji yanayorushwa mbali yanaonekana kama ni lulu zilizotupwa kutoka juu, hususan katika majira yenye mvua nyingi, maporomoko ya maji yanaunguruma kama radi. Mtalii Wang Yan alisema,

    "Maporomoko ya maji yanavutia sana, maji ya maporomoko ni mengi, watalii pia ni wengi, watu wote wanafurahi sana, mlima Lushan ni mrefu na unapendeza sana."

    Mandhari ya mlima Lushan ni nzuri sana katika majira yote manne ya mwaka. Katika enzi ya Tang zaidi ya miaka 1,000 iliyopita, mshairi mmoja alitunga shairi akisema, mlima Lushan unapendeza zaidi katika majira ya Spring, ambapo mvua ya manyunyu inanyesha na maua ya mipichi yanachanua. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya mlima Lushan, Bw. Dai Jian alisema,

    "Katika majira ya Spring Mlima Lushan ni kama shairi na ndoto, kutokana na kuweko kwa mawingu na ukungu mwingi katika mwezi Machi na Aprili, ambapo vilele vya milima mara vinatoweka na mara vikaonekana tena. Vivutio vikubwa zaidi ni bustani ya mimea, bonde la Jinxiu, Huajing na chemchemi yenye maanguko matatu ya maji."

    Kwenye mlima Lushan, majira ya Spring yanaanza katikati hadi mwishoni mwa mwezi April, wakati sehemu nyingine zimeingia kwenye majira ya joto. Mwaka 1988, bustani ya Huajing ya mlima Lushan ilijenga ukumbi wa maonesho ya Caotang ya mshairi Bai Juyi, jiwe moja lililoko katika kibanda cha Huajing limechongwa maneno mawili ya Huajing, ambayo yanasemekana ni hati ya mkono ya mshairi Bai Juyi. Katika majira ya Spring, maua yaliyoko kwenye kibanda cha Huajing yanachanua vizuri na kuwa ya kupendeza sana. Mtalii Chen Kun alisema,

    "Ninaishi kwenye mji wenye kelele nyingi, kufika hapa kunanifanya nione kama nimerejea katika mazingira ya kimaumbile, kuna maeneo makubwa ya maua, ambayo ni tofauti na sehemu nyingine."

    Kwa kuwa huko kuna aina nyingi za maua, hivyo maua ya mipichi ya Huajing yanachanua kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi hadi mwanzoni mwa mwezi Mei, hivi sasa kila siku kuna watalii zaidi ya 3,000 wanaofika huko kuangalia maua. Mkurugenzi wa bustani ya Huajing, Qian Yifei alisema,

    "Maua yanachanua sana mwezi Mei kwenye mlima Lushan, tokea mwanzoni mwa mwezi Aprili, maua ya mipichi yanachanua vizuri, ambayo yanavutia idadi kubwa ya watalii. Mwezi Novemba mwaka 2008, tuliingiza baadhi ya maua hasa maua ya mipichi kutoka mikoa ya Zhejiang, Fujian na Hunan."

    Mwishoni mwa majira ya Spring na mwanzoni mwa majira ya joto, bonde la Jinxiu, ambalo liko karibu na bustani ya Huajing, ni mahali pazuri pa kutembelea. Bonde hilo lina urefu wa kilomita 1.5 hivi, lakini kote ni mandhari nzuri ya kuvutia. Mtalii Bi. Xu Li alisema,

    "Bonde la Jinxiu linapendeza sana, na leo tumeona bahari ya mawingu, ni mazuri sana."

    Mtalii kutoka Taiwan Bw. Wang Songrong alisema,

    "Niliwahi kufika kwenye mlima Manjano, pia niliwahi kufika kwenye mlima Taishan, lakini ninaona uzuri wa mlima wa Lu ni tofauti nayo, ingawa mlima Lushan hauna magenge marefu kama mlima Manjano na siyo mrefu kama mlima Taishan, lakini uzuri wake ni wa kupendeza."

    Katika Mlima Lusha kuna maliasili nyingi za viumbe. Misitu inachukua zaidi ya 76.6%. Kuna wadudu wa aina zaidi ya 2,000, ndege wa aina zaidi ya 170, na wanyama wa aina 37. Mkurugenzi wa bustani ya mimea ya mlima Lushan Bw. Wei Zongxian alisema,

    "Bustani ya mimea ya mlima Lushan ilijengwa mwaka 1934, sasa bustani hii ina misonobari na mivinje ya aina 247, ambayo dunia nzima ina aina 600 hivi. Bustani hii ina maua ya azelia ya aina 300 hivi, wakati China nzima ina aina 600 hivi. Licha ya hayo bustani hii ina mimea mbalimbali ya aina nyingi .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako