• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washington-Jeshi la Marekani kutoa ombi la kuongeza askari nchini Afghanistan katika wiki kadhaa zijazo

    (GMT+08:00) 2009-09-01 19:50:27

    Msemaji wa ikulu ya Marekani Bw. Robert Gibbs tarehe 31, Agosti alisema, kamanda mkuu wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan na jeshi la jumuiya ya NATO nchini Afghanistan Bw. Stanley McChrystal hakutoa ombi la kuongeza askari kwenye ripoti ya kutathmini vita vya Afghanistan, lakini inakadiriwa kuwa jeshi la Marekani litatoa ombi hilo kwa rais Barack Obama katika wiki kadhaa zijazo.

    Siku hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ikulu ya Marekani Bw. Gibbs alisema, ripoti hiyo inatathmini hali ya Afghanistan na operesheni za Marekani na kutoa mashauri kuhusu marekebisho ya sera. Ombi la kuongeza askari halijawekwa kwenye ripoti hiyo, ambapo ombi hilo linatazamiwa kutolewa kwenye wiki kadhaa zijazo.

    Na jeshi la utoaji msaada wa usalama wa kimataifa nchini Afghanistan linaloongozwa na jumuiya ya NATO tarehe 1, mwezi wa Septemba lilitoa taarifa ikisema, askari wawili wa NATO tarehe 31, Agosti waliuawa walipokuwa wakirushiana risasi na watu wenye silaha kusini mwa Afghanistan, hii imefanya idadi ya wanajeshi wa nchi za nje nchini Afghanistan waliokufa katika mwezi huu iongezeke hadi 77, na kuweka rekodi mpya kutokana na idadi kubwa ya wanajeshi wa nchi za nje waliouawa nchini Afghanistan ndani ya mwaka mmoja tokea mwaka 2001.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako