• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shughuli za usafiri wa ndege na vyombo vya safari za anga ya juu zaendelezwa kwa kasi nchini China

    (GMT+08:00) 2009-09-03 17:06:29

    Huu ni mwaka wa 60 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe. Baada ya kufanya juhudi kwa miongo kadhaa, katika miaka ya hivi karibuni China imepata mafanikio makubwa katika usafiri wa ndege na vyomgo vya safari za anga ya juu ambazo zinaonesha nguvu ya jumla ya sayansi na teknolojia. "Nimetoka nje ya chombo cha Shenzhou No.7. Najisikia vizuri. Nawasalimia wachina wote na watu wa nchi nyingine duniani."

    Tarehe 27 Setemba mwaka 2008, kwenye anga ya juu umbali wa zaidi ya kilomita 300 kutoka ardhi ya dunia, mwanaanga wa China Bw. Zhai Zhigang alitoka nje ya chombo cha Shenzhou No.7 cha kuwasafirisha watu kwenda anga ya juu, na kuwa mchina wa kwanza kutembelea kwenye anga ya juu. Mliosikia ni sauti yake kutoka angani. Jambo hili linamaanisha kuwa, China imekuwa nchi ya tatu yenye teknolojia ya kuwawezesha wanaanga kufanya shughuli angani nje ya vyombo vya safari za anga ya juu baada ya Russia na Marekani.

    Teknolojia ya chombo cha kusafirisha watu kwenye anga ya juu inahusisha sekta mbalimbali za sayansi zikiwemo roketi, chombo cha safari angani, mfumo wa usimamizi na udhibiti, na mawasiliano ya habari, na hivi sasa teknolojia hiyo ni teknolojia kubwa na yenye utatanishi na hatari zaidi duniani. Naibu kiongozi wa mradi wa chombo cha kuwasafirisha watu kwenye anga ya juu wa China Bw. Zhang Jianqi alisema, China isingekuwa na uwezo mkubwa wa sayansi na teknolojia, isingeweza kutimiza lengo la mwanaanga kutembea angani nje ya chombo cha safari. Alisema,

    "Tumefanikiwa katika utafiti wa teknolojia ya kuondoa na kurejesha hewa katika chumba kinachounganisha nje cha chombo cha safari za anga ya juu, utengenezaji wa nguo wanazovaa wanaanga wakati wa kutembea angani nje ya chombo cha safari, teknolojia za mfumo wa mikroelectoniki na malighafi mpya."

    Lakini miaka 60 iliyopita, kuwa na nguvu kubwa ya sayansi na teknolojia ilikuwa ni ndoto tu kwa wachina. Wakati huo kote nchini China kulikuwa na watu wasiofikia 500 walioshughulikia utafiti wa sayansi na teknolojia.

    Baada ya kuasisiwa kwa China mpya, serikali ya China ilitilia mkazo kuendeleza shughuli za sayansi na teknolojia, na kutunga mwongozo wa mipango ya muda mrefu kuhusu maendeleo ya sayansi na teknolojia. Mwaka 1964, China ilifanikiwa kutengeneza mabomu ya atomiki, na miaka mitatu baadaye, ilitengeneza mabomu ya haidrojeni. Mwaka 1970, satelaiti ya kwanza ya China ilifanikiwa kurushwa katika anga ya juu. Mafanikio hayo muhimu si kama tu kuongezea China uwezo wa sayansi na teknolojia na ulinzi wa taifa, na kuweka msingi wa China kupata hadhi muhimu duniani, bali pia yalifanya maandalizi mazuri ya teknolojia na watu wenye ujuzi kwa ajili ya maendeleo ya vyombvo safari za anga ya juu. Ofisa mwandamizi mhusika wa wizara ya sayansi na teknolojia ya China Bw. Mei Yonghong alisema,

    "China imekuwa na msingi imara wa sayansi na teknolojia, na ina mfumo kamilifu wa sekta mbalimbali za sayansi na teknolojia ambao umejengwa katika nchi chache tu duniani. Mbali na hayo, China ina idadi kubwa ya watu wanaoshughulikia sayansi na teknolojia wakiwemo watafiti."

    Mwaka 1978, China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Tokea mwaka huo, China ilihakikisha wazo la kimkakati la "Sayansi na Teknolojia kuwa Nguvu kubwa zaidi katika Uzalishaji Mali", na kuanzisha miradi mbalimbali ya utafiti wa sayansi na teknolojia. Katika miongo kadhaa iliyopita, sura ya shughuli za sayansi na teknolojia nchini China zimebadilishwa kabisa, na nguvu ya sayansi na teknolojia ya China imeongezeka kwa kasi. Wachina wananufaishwa na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, huku wakiona fahari kubwa kwa maendeleo hayo. Wakazi wa Beijing walipohojiwa na mwaandishi wetu wa habari walisema,

    "Naona fahari kubwa. Mradi wa chombo cha safari za anga ya juu umeonesha maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia na ongezeko la nguvu ya taifa nchini kwetu. Naona kuwa mradi huo una maana ya muda mrefu. Nataka kuwaambia wanaanga wetu kuwa, wao ni mashujaa wa taifa letu."

    "Kurusha kwa mafanikio kwa chombo cha Shenzhou No.7 ni hatua kubwa nyingine ya nchi yetu katika historia ya vyombo vya safari za anga ya juu. Hali hii pia ilifuatiliwa sana na nchi nyingine duniani. Tunaona fahari kubwa."

    Mradi wa kuwafarisha watu katika anga ya juu ulianza mwanzoni mwa mwaka 1990. Kabla ya hapo, China ilikuwa na akiba kubwa ya teknolojia. Kabla China haijatekeleza hatua ya kuwasafirisha watu katika anga ya juu mara ya kwanza, imetengeneza na kurusha kwa kujitegemea satilaiti zaidi ya 50 za aina 15. Aidha China pia imetengeneza kwa kujitegemea roketi za aina zaidi ya 10 ya "Changzheng", na kufanikiwa kurusha satilaiti zaidi ya 70 za nchi za nje katika anga ya juu.

    Kutokana na msingi huo imara, mradi wa kuwasafirisha watu katika anga ya juu umeendelezwa kwa kasi ya kuwashangaza watu. Mwezi Oktoba mwaka 2003, China ilifanikiwa kumsafirisha mtu katika anga ya juu kwa mara ya kwanza, mwanaanga wa China Bw. Yang Liwei alikuwa katika anga ya juu kwa saa zaidi ya 21. Mwaka 2005, wanaanga wawili wa China walikuwepo tena katika anga ya juu kwa siku tano. Mwezi Septemba mwaka 2008, wanaanga watatu walisafiri katika anga ya juu kwa siku karibu 3, ambapo Bw. Zhai Zhigang alitembea angani nje ya chombo cha safari.

    Hali kadhalika, China pia imetupia macho sayari ya mwezi. Mwezi Oktoba mwaka 2007, satilaiti ya kwanza ya China ya kuchunguzia sayari ya mwezi "Chang'e No.1" ilirushwa angani, na katika mwaka mmoja satilaiti hiyo ilifanikiwa kumaliza kazi zake zilizopangwa za uchunguzi. Mbunifu mkuu wa mradi wa kuchunguza sayari ya mwezi kwa kuizingira Bw. Sun Jiadong alisema,

    "Kabla ya hapo, shughuli za nchi yetu ya safari za anga ya juu zilifanyika katika anga isiyoko mbali na sayari ya dunia, na umbali huo ulikuwa kati ya kilomita mia kadhaa na elfu kumi kadhaa. Baada ya kuwa na teknolojia ya kiwango cha juu zaidi, China imelengea anga ya juu zaidi, na kusafiri katika sayari ya mwezi ni hatua ya kwanza."

    Zaidi ya hayo, mradi wa kutafiti na kutengeneza ndege kubwa uliosimamishwa kwa miaka mingi ulirejeshwa na kupitishwa na serikali ya China mwaka 2007. Mhandisi wa ngazi ya juu wa Kampuni ya Sayansi na Teknolojia ya Safari ya Anga ya China Bw. Gan Liwei alisema, China inatazamiwa kufanikiwa kutengeneza ndege kubwa kwa kujitegemea hadi kufikia mwaka 2020. Alisema,

    "Endapo tutaweza kutengeneza ndege kubwa mwaka 2020, nguvu ya nchi yetu itaongezeka kwa kiasi kikubwa. Hali hii pia itahimiza sana sekta nyingi za viwanda ziendelezwe zaidi."

    Katika miaka ya hivi karibuni taathira ya China kwenye mambo ya dunia ya usafiri wa ndege na vyombo vya safari ya anga ya juu imeongezeka siku hadi siku. Ndege mpya za ARJ21 zinazotumiwa kwenye matawi ya njia kuu ambayo zilibuniwa na kutengenezwa na China kwa kujitegemea zinauzwa katika Marekani na nchi za Ulaya. Satilaiti ya kuchunguza maliasili ya sayari ya dunia iliyobuniwa na kutengenezwa na China pamoja na Brazil imetoa hudumu nzuri kwa China na nchi nyingine katika kuchunguza, kuendeleza, kutumia na kuendesha maliasili ya ardhi. Aidha China pia imezirushia Venezuela na Nigeria satilaiti za mawasiliano ya habari, ambazo zinatumiwa kutoa huduma za afya na elimu kwa watu wanaoishi katika sehemu za mbali.

    Ingawa China imepata mafanikio makubwa katika shughuli za safari za anga ya juu, lakini mafanikio hayo ni hatua ya mwanzo tu, na China itaendelea na juhudi zake katika shughuli hizo. Msanifu mkuu wa Chombo cha Shenzhou No.7 Bw. Zhou Jianping alisema,

    "Kuchunguza mifumo ya sayari na kupanua sehemu ya kuisha kwa binadamu ni ndoto ya muda mrefu ya binadamu. China itadumisha hatua inayolingana na nguvu ya kiuchumi katika kuendeleza shughuli za kuwapeleka binadamu kwenye anga ya juu, ili binadamu wafike sehemu za mbali zaidi na kugundua mambo mengi mapya zaidi katika mifumo ya sayari."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako