• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu kutoka India wanavyoielezea China

    (GMT+08:00) 2009-09-07 14:55:20

    Miaka zaidi ya 40 imepita tangu idhaa ya Kitamil ya Redio China Kimataifa ianzishe matangazo, wageni wengi kutoka India na Sri Lanka wamewahi kuja China na kufanya kazi kwenye idhaa hiyo ya Redio China Kimataifa. Katika kipindi cha leo tutasikia jinsi watatu kati yao wanavyoelezea maisha yao nchini China yalivyo, na jinsi wanavyoiona China.

    Bw. Kadikaa Chalam ni mmoja kati ya wageni waliofanya kazi kwa muda mrefu zaidi CRI. Yeye alikuja Beijing kwa mara ya kwanza mwaka 1983, baada ya kukaa nchini China kwa karibu miaka 20, alirudi nyumbani mwaka 2004. Katika miaka hiyo 20 alipokaa nchini China, alishuhudia mabadiliko makubwa yakitokea nchini China. Anajivunia sana kuona China ilivyoendelea kufungua mlango, ambapo sayansi na teknolojia za kisasa na maarifa mazuri ya kimaendeleo zinamiminikia China kutoka nje. Akikumbusha alisema katika kipindi cha mwanzo cha utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango nchini China, bidhaa zilikuwa hazipatikani kwa wingi, watu walitakiwa kununua bidhaa kwa kuponi. Baada ya miongo kadhaa tu, bidhaa za aina mbalimbali hata za kutoka nchi za nje zinapatikana kwenye supamaketi. Mwaka 1999 wakati ambapo Bw. Chalam alipokuja China kwa mara ya tatu, aliona miji ambayo awali ilionekana kama ni vijiji vikubwa, imekuwa miji ya kweli kutokana na majengo mengi marefu na barabara kubwa. Mshahara wa Bw. Chalam pia uliongezeka kutoka Yuan mia kadhaa hadi yuan karibu elfu kumi.

    "Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, China ilipoanza kufungua mlango wake, bado nakumbuka shida zilizoletwa na ukosefu wa bidhaa. Wakati nilipohamia kwenye nyumba yangu mpya, sikuweza kupata mapazia. Na vitambaa pia havikupatikana kwa wingi. Nilipaswa kwenda kwenye Duka la Urafiki lililoko mbali, kununua bidhaa zinazotumiwa katika maisha ya kila siku kwa kuponi za fedha za kigeni. Hata nilipaswa kutumia unga kwa uangalifu. Kuponi ya chakula ni kitu ninachokumbuka mpaka leo."

    Mhindi mwingine aitwaye Raajaaram kutoka kituo cha All India Radio alikuja China mwaka 2003. Kabla ya kuondoka kuja China, Bw. Raajaaram alipata maonyo mengi kutoka kwa wenzake kuhusu China. Lakini wakati alipoishi nchini China alikuwa na picha mpya kabisa kuhusu nchi hiyo. China si kama tu aliona iko wazi kwa sayansi na teknolojia kutoka nchi za magharibi, bali pia iko wazi kwa mitindo tofauti ya maisha, ambayo inawachangamsha vijana. Bw. Raajaaram alisema moyo wa wazi na udhati wa China umeweka msingi mzuri kwa mawasiliano kati yake na nchi za nje.

    "Wakati nilipokuja China nilikuta awamu mpya ya serikali ikiingia madarakani, ambapo kasi ya gari moshi iliongezeka kwa kiasi kikubwa. Nilikwenda kwenye hekalu la Shaolin, mji wa Shenzhen na wenzangu kwa garimoshi, na inachukua saa 10 tu kusafiri kutoka Beijing hadi Shanghai. Nilijionea "kasi ya maendeleo" ya China ambayo ilikuwa ikiendelea kuongezeka. Makampuni ya nchi za nje yanawekeza nchini China, na makampuni ya China pia yaliwekeza katika nchi za nje. Nchini India chapa za China kama vile Lenovo na Haier zinajulikana sana."

    Wakilinganishwa na Bw. Chalam na Bw. Raajaaram, Bw. Maria Michael na mkewe Bibi. Mary Fraskal wanaoishi Beijing wana bahati zaidi, kwa kuwa si kama tu wanaweza kufurahia bidhaa zinazopatikana kwa wingi, bali pia wanaweza kwenda kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa "Kiota", na jumba la maonesho la kitaifa wakati wowote kwa Subway, ambazo zinaunganisha sehemu mbalimbali za Beijing.

    Uraibu wa wanandoa hao ni kusafiri. Ingawa hawajui sana Kichina lakini suala la lugha haliwakwamishi kufanya safari na kuishi maisha ya kila siku. Bibi Fraskal ambaye anajua kuendesha familia, anasifu sana bidhaa zinazotengenezwa na China akisema:

    "Kwenye hekalu la mji huko Shanghai, au barabara ya magharibi ya mji wa Xi'an au masoko ya hapa Beijing, kila nikifika mahali fulani nikiona bidhaa za aina mbalimbali, ninataka kuwanunulia jamaa na marafiki zangu zawadi nyingi. Mama yangu anapenda sana sari inayotengenezwa kwa hariri ya China. Sari ni nguo ya jadi ya wahindi, lakini sari inayotengenezwa nchini China ni bora na bei nafuu, na tunaipenda zaidi."

    Hivi sasa idadi ya wageni wanaofanya kazi na kuishi nchini China inaongezeka siku hadi siku, wakiwemo marafiki wengi wa Bw. Michael na Bibi. Michael kutoka India. Bw. Michael alisema:

    "Uhai na fursa zinazojaa miji ya China zinamaanisha kuwa wahudumu wa mikahawa wanaweza kuwa mameneja, walimu wa Yoga wanaweza kuwa mkuu mtendaji(CEO). China inawapokea watu wa hali mbalimbali wenye ndoto kwa moyo wa dhati na uvumilivu. Kutimiza "Ndoto ya China" kunahitaji upate fursa na kuishikilia. Naamini kuwa mbele ya ofisi ya ubalozi wa China nchini India, misururu ya watu wanaosubiri visa zao itakuwa mirefu siku hadi siku."

    Bw. Michael ameona kwamba wakati China inapofungua mlango wake, pia inajitahidi kufahamisha utamaduni wake mzuri kwa dunia nzima. Anasema:

    "Nimepata habari ya kwamba Chuo cha Confucius kitaanzishwa kwenye maskani yangu mkoa wa Tamil Nadu nchini India. Mkondo wa kujifunza lugha ya Kichina unafuatwa kote duniani. Wasanii wa China wanaonesha kazi zao katika sehemu mbalimbali duniani, na Michezo ya Olympiki imeonesha uwazi wa China kwa dunia nzima. Na wakati msukosuko wa fedha unapoendelea duniani, China imetuma ujumbe kununua vitu katika nchi za nje, na kupita wakati mgumu pamoja na nchi mbalimbali. Naona kuwa nafasi ya China katika jumuiya ya kimataifa inaendelea kubadilika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako