• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya elimu wapata maendeleo makubwa

    (GMT+08:00) 2009-09-11 09:27:50

    Mkutano wa 4 wa mawaziri wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika nchini Misri katika robo ya mwisho ya mwaka huu. Tangu mwaka 2006 mkutano wa wakuu wa baraza hilo ulipofanyika hapa Beijing, uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Afrika umepata maendeleo makubwa, na kazi ya utekelezaji wa ahadi za serikali ya China kwa Afrika pia imepata mafanikio makubwa.

    Kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi ni moja kati ya hatua nane zilizotangazwa na China kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika, pia ni sehemu muhimu ya kazi ya China kutoa misaada kwa nchi za nje. Naibu mkurugenzi wa idara ya kutoa misaada kwa nchi za nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Wang Shichuan alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema,

    "Mpaka sasa, China imeandaa semina 2,500 za aina mbalimbali kwa ajili ya watu kutoka nchi na sehemu zinazoendelea zaidi ya 160, na watu zaidi ya laki moja wamepata mafunzo hayo. Katika mwaka 2007 na mwaka 2008, China iliisaidia Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi wapatao elfu 11. Hivi sasa semina zinazoandaliwa na China zinahudhuriwa na watu wengi wa nchi zinazoendelea, semina hizo zinahusu sekta mbalimbali na zinawashirikisha watu wa ngazi ya juu. "

    Bw. Wang alijulisha kuwa tangu mwaka 2004, wizara ya biashara na wizara ya elimu za China zimejenga uhusiano barabara wa ushirikiano, na kupata mafanikio makubwa. Hadi sasa vyuo vikuu zaidi ya 30 na mashirika ya elimu na mafunzo yameandaa semina 150 za aina mbalimbali chini ya uendeshaji wa wizara ya biashara ya China kwa ajili ya watu 4200 kutoka nchi zinazoendelea. Katika mpango wa mwaka huu wa kuzisaidia nchi zinazoendelea kuwaandaa watu wenye ujuzi, China itaandaa semina 348, kati ya hiyo kuna semina zaidi ya 40 kuhusu elimu. Siku za baadaye, kutokana na bajeti, wizara ya biashara ya China itaandaa semina nyingi zaidi za kutoa mafunzo kwa kutegemea msaada wa vyuo vikuu husika vya China.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Cao Zhongming alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alismea, kutoa msaada wa elimu ni sehemu muhimu ya kazi ya China ya kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi, pia ni njia muhimu ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na Afrika. Alisema,

    "Kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing Rais Hu Jintao wa China alitangaza kuwa, katika miaka mitatu China itazisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi wa aina mbalimbali wapatao elfu 15, kujenga shule 100 vijijini barani Afrika, na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopewa udhamini wa masomo na serikali ya China kufikia 4000 kutoka idadi ya 2000 ya mwaka 2006."

    Bw. Cao alisema, kuzisaidia nchi za Afrika kuwaandaa watu wenye ujuzi ni ushirikiano wa kimkakati na wa muda mrefu kati ya China na Afrika. Tangu miaka ya 50 ya karne iliyopita, ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya elimu umepata maendeleo makubwa. China na nchi za Afrika zinatumiana wanafunzi, maofisa waandamizi wa elimu wa pande hizo mbili wanatembeleana, China inatuma wanafunzi barani Afrika na kuisaidia Afrika kuendeleza mafunzo ya lugha ya Kichina, kuendesha miradi ya ushirikiano wa elimu, na kuandaa makongamano ya aina mbalimbali.

    Naibu waziri wa elimu wa China Bw. Hao Ping alisisitiza kuwa, ingawa kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, lakini serikali ya China itaendelea kuongeza misaada ya elimu kwa Afrika, ili kutimiza ahadi ilizotoa China kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing. Alisema,

    "Mwezi Februari mwaka huu, rais Hu Jintao alipofanya ziara katika nchi nne za Afrika, alieleza kuwa serikali ya China haitapunguza misaada yake kwa Afrika kutokana na msukosuko wa fedha duniani. Rais Mwai Kibaki wa Kenya aliishukuru China kwa msimamo wake wa uaminifu. "

    Bw. Hao alisema, licha ya kuandaa makongamano, wizara ya elimu ya China pia imeongeza idadi ya wanafunzi wa Afrika wanaopewa udhamini wa masomo nchini China. Idadi ya wanafunzi hao mwaka 2008 ilifikia 3,735 kutoka 1,154 ya mwaka 2000, ambapo iliongezeka kwa mara tatu. Hadi kufikia mwaka 2010, China itakuwa na wanafunzi 4,000 kutoka Afrika wanaopewa udhamini wa masomo na serikali ya China.

    Alipozungumzia mpango wa wizara ya elimu ya China kuhusu ushirikiano wa elimu kati ya China na Afrika katika siku za mbele, Bw. Hao alisema wizara hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kuendeleza nguvukazi, kuboresha utaratibu wa kutuma walimu katika nchi za nje, kuinua kiwango cha wanafunzai wa Afrika wanaopewa udhamini wa masomo na serikali ya China, na kuimarisha utafiti wa suala la Afrika na kuwaandaa watu wenye ujuzi kuhusu suala la Afrika.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako