• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa bustani na mapumziko

    (GMT+08:00) 2009-09-14 10:12:00

    Yangzhou ni mji wa kale wenye utamaduni na historia ya karibu miaka 2,500, na ulichaguliwa kuwa ni mmoja kati ya miji 24 ya kundi la kwanza la miji maarufu ya kihistoria na utamaduni, mwaka 2006 mji huu ulipewa tuzo ya mazingira ya makazi ya Umoja wa Mataifa. Mji Yangzhou uko kwenye sehemu ya kati ya mkoa wa Jiangsu, toka zamani mji huu umekuwa ni kiunganisho muhimu cha mawasiliano kwa njia ya majini na nchi kavu. Kama mtu akisafiri kutoka mji wa Shanghai kwenda Yangzhou kwa basi inahitaji karibu saa 4. Kuna gari moja la kasi la kwenda huko kutoka Beijing, kama mtu akiondoka asubuhi anaweza kufika huko jioni.

    Mji wa Yangzhou, ambao unajulikana kwa mji tajiri toka zamani, pia ni mji wenye mandhari nzuri na unasifiwa kuwa ni mji wa bustani. Mwezi Machi, mvua za rasharasha zinanyesha huku maua yakichanua vizuri, huu ni wakati mzuri zaidi wa kutembelea Yangzhou, na tamasha la shughuli za biashara na utalii linafanyika wakati huo kila mwaka. Kati ya mwezi Septemba na Oktoba hufanyika tamasha ya utamaduni huko, na pia ni wakati mzuri wa kujiburudisha kwa mbalamwezi. Shughuli muhimu katika wakati hou ni kuangalia mbalamwezi kwenye bustani, kujiburudisha katika mashua wakati wa usiku kwenye mfereji mkubwa na kuonja vyakula maalumu vya huko.

    Mji wa Yangzhou una mabaki mengi maarufu ya kale na bustani nyingi nzuri. Wakati inapoelezwa Yangzhou, inastahili kulitaja ziwa dogo la Shouxihu lililopo kwenye mji huo, Shouxihu, maana yake ya kichina ni ziwa jembamba, ziwa hilo linapewa jina hilo ili kulitofautisha na ziwa Shouxihu ambalo ni ziwa maarufu la mji wa Hangzhou, kwani ziwa hili ni dogo zaidi. Mwongoza watalii Xia Liangping alisema, ziwa hili ni dogo, lakini hali hii inalifanya ziwa hilo liwe la kupendeza kwa namna yake. Akisema

    "Ninaona uzuri wa ziwa dogo Shouxihu ni hali ya wembamba wake. Sasa watu wanaona watu wembamba ni warembo kwa hiyo ziwa letu ni ziwa zuri kutokana na hali yake ya wembamba."

    Ziwa dogo la Shouxihu linajulikana toka zamani, na linapendwa na mabingwa wa sanaa ya bustani katika enzi mbalimbali, kwenye kando mbili za sehemu ya ziwa yenye urefu wa kilomita 5 imeendelezwa kuwa sehemu nzuri ya kujiburudisha kwa mandhari ya mbalamwezi. Mwongoza watalii Bi Xia Liangping alisema,

    "Ziwa dogo la Shouxihu lina urefu wa kilomita 5 hivi, unaweza kujiburudisha kwa mandhari nzuri ya ziwa na bustani ukiwa kwenye mashua au kwa kutembea kwa miguu, kwani mandhari yake ya bustani kadhaa binafsi inapendeza, ambazo kila moja ina umaalumu wake."

    Mbali na hayo, Yangzhou ina hekalu maarufu la kale linaloitwa Daming, pamoja na bustani ya He Yuan inayosifiwa kama "msitu wa mji ulioko mlimani", bustani Ge Yuan yenye vilima vilivyotengenezwa na binadamu na makazi ya muda ya wafalme ya Suiyang, Kangxi na Qianlong.

    Hivi sasa Yangzhou ni mji unaofungua mlango na ni mji mpya unaostawi. Hali halisi ni kuwa katika historia Yangzhou ilikuwa mji maarufu uliofungua mlango. Ulikuwa ni mji uliostawi zaidi kwenye sehemu ya kusini mashariki na ilikuwa moja kati ya bandari nne kubwa zenye maingiliano ya kiuchumi na kiutamaduni na nchi za nje katika enzi ya Tang, wakati ule mji wa Yangzhou ulikuwa na wafanyabiashara zaidi ya elfu 10 kutoka nchi za nje. Mtawa mkongwe maarufu Jianzhen alisafiri mara 6 had Japan. Wasafiri maarufu Cui Zhiyuan wa Korea ya kusini na Marco Polo wa Italia wamewahi kufika Yangzhou. Hivi sasa mji wa Yangzhou umeanzisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na miji 13 ya nchi 10. Meya wa mji wa Breda wa Uholanzi, ambao umejenga uhusiano wa kirafiki na mji wa Yangzhou Bw Vander Velden amewahi kufika Yangzhou mara nyingi, na kila mara anaona mambo mapya, alisema,

    "Naona mji wa Yangzhou utakuwa na mustakabali mzuri iwe katika uchumi, jamii au utamaduni. Yangzhou ni mji mzuri sana, baada ya kurejea mji Breda, nitawaambia watu wa huko, Yangzhou ni mji mzuri sana, ambao wanaweza kuja na kupumzika."

    Maisha ya wakazi wa Yangzhou ni ya starehe, wakazi wa Yangzhou wakiulizwa vitu maalumu vya Yangzhou ni nini, watajibu ni vyakula vidogo vidogo na mapumziko. Naibu meya wa Yangzhou Bw. Wang Yuxin alisema,

    "Katika historia Yangzhou ulikuwa mji wa jadi wa mapumziko, mji huu una mazingira bora ya kupumzika, utamaduni mkubwa na shughuli nyingi za utalii. Watalii wanaona hali mpya, licha ya kuburudika kwa kuona mandhari nzuri, pia wanaburudishwa kimawazo. Tunajitahidi kuwafanya wageni wote wanaofika Yangzhou waone mji huu vizuri, na wafurahi sana wanapokuwa Yangzhou."

    Meya Wang alisema, hivi sasa mji wa Yangzhou unabuni mpango wa "mji wa utalii", mji mzima utakuwa na vivutio vizuri, watalii wanaofika Yangzhou, watafurahishwa zaidi na mazingira ya kupumzika kuliko mandhari nzuri ya kimaumbile. Alisema,

    "Ninawaalika wageni wa nchini na wa nchi za nje waje kuwekeza mjini Yangzhou na wapate fursa ya kujiendeleza. Mandhari nzuri inawavutia watalii mara moja tu, lakini utalii wa mapumziko utawavutia waje mara nyingi, tunajitahisi sasa, na tunatarajia kuwa watalii wataridhika na hali hiyo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako