Tarehe 1 Oktoba mwaka 2009 ni siku ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe. Katika siku za hivi karibuni, maofisa wa serikali na wataalamu wa nchi mbalimbali za Afrika walipohojiwa na waandishi wa habari wa China walitoa salamu za pongezi kwa siku ya taifa ya China na kusifu sana uhusiano wa kirafiki na ushirikiano uliopo kati ya China na Afrika.
Wataalamu wa Kenya: maendeleo ya China yanufaisha watu wake na dunia nzima
Wataalamu wa Chuo kikuu cha Nairobi wamesema, maendeleo ya China si kama tu yananufaisha watu wake, bali pia yameleta maslahi kwa dunia nzima. Misaada inayotolewa na China kwa nchi za Afrika imewanufaisha waafrika. Waafrika wanatoa psalamu za ongezi kwa China kuadhimisho miaka 60 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe, na kutarajia kuwa China itapata maendeleo makubwa zaidi katika siku za baadaye.
Mkuu wa chuo cha sayansi ya kijamii ya chuo kikuu cha Nairobi ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi Issak Mubeki alisema, wakati dunia ipo kwenye msukosuko wa fedha, hali ya uchumi wa China inaonekana kuwa ya utulivu, hii imeonesha busara ya wachina kwamba, wakati wa kuingiza mfumo wa uchumi wa soko huria, China inazingatia kuimarisha udhibiti wa mambo ya uchumi wa jumla.
Bw. Mbeki alisema, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Kenya na China unapanuliwa siku hadi siku, na maingiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili pia yanaongezeka bila kusita, Kenya imenufaika kutokana na maendeleo ya uchumi wa China. Alisema, wachina wanaowekeza au kutalii nchini Kenya wanaongezeka siku hadi siku, vilevile wanafunzi wa Kenya wanakwenda China ili kujifunza lugha ya kichina na kujifunza uzoefu wa maendeleo ya jamii na uchumi. Uhusiano kati ya Kenya na China hakika utakuwa karibu zaidi.
Mwalimu wa idara ya lugha ya chuo kikuu cha Nairobi ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu cha ualimu cha Tianjin China Bw. Tom Aurarri anasema, misaada iliyotolewa na China kwa Kenya ni dhati na wala haina maslahi binafsi, vilevile haina masharti ya kisiasa. Na China haiingii mambo ya ndani ya nchi nyingine.
Bw. Aurarri alisema, China inasonga mbele kufuata njia sahihi ya kujiendeleza, anaamini kuwa, China bila shaka itapata maendeleo makubwa zaidi katika siku za baadaye.
Maofisa wa wizara ya mambo ya nje ya Cote D'ivoire: China imetoa uzoefu na fursa kwa maendeleo ya nchi za Afrika
Mkurugenzi wa idara ya Asia na Mashariki ya Kati ya wizara ya mambo ya nje ya Cote D'ivoire Bw. Yakba Atta hivi karibuni alisema, maendeleo ya China yametoa uzoefu kwa nchi za Afrika. Vilevile misaada iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na miradi ya uwekezaji imeleta fursa nzuri kwa maendeleo ya nchi za Afrika.
Bw. Atta alitoa pongezi kwa China kuadhimisha miaka 60 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe. Alisema, katika miaka 60 iliyopita, mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za siasa, uchumi na jamii nchini China, kiwango cha mashisha ya wananchi wa China kimeinuka sana. Uzoefu wa China unastahili kuigwa na nchi nyingine.
Katibu mkuu wa chama tawala cha Togo asifu sana maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini China katika miaka 60 iliyopita
Katibu mkuu wa chama tawala cha Togo RTP Bw. Esso alisema, katika miaka 60 iliyopita tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe, hasa miaka 30 iliyopita tangu China ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, China imepata maendeleo makubwa. Nchi zinazoendelea ikiwemo Togo zinafurahia maendeleo ya China, kwa sababu nchi za Afrika si kama tu zinaweza kunufaishwa na msaada wa China, bali pia zilipata uzoefu wa maendeleo ya China na kuhimiza maendeleo ya nchi zao.
Bw. Esso amesema, tangu uhusiano wa kibalozi kati ya Togo na China uanzishwe tarehe 19 Septemba mwaka 1972, maofisa wa pande hizo mbili wanatembeleana mara kwa mara, China imetoa msaada mkubwa kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa Togo, uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili unaendelezwa na kuimarishwa mwaka hadi mwaka..
Ofisa wa Zimbabwe : China imeonesha mfano mzuri wakuigwa katika kuboresha maisha ya wananchi wake
Waziri wa elimu wa Zimbabwe Bw Stan Mutenge hivi karibuni alisifu mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uchumi na jamii tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe miaka 60 iliyopita. Alisema China imeonesha mfano mzuri wa kuingwa katika kuboresha maisha ya wananchi wake.
Bw. Mutenge alipohudhuria tafrija ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China iliyofanyika katika ubalozi wa China nchini Zimbabwe alisema, katika miaka 60 iliyopita, China imeendelezwa kuwa nchi kubwa ya kiuchumi duniani kutoka nchi iliyokuwa nyuma kimaendeleo. Bw. Mutenge alisema, katika miaka ya 70 ya karne iliyopita, China iliwaunga mkono watu wa Zimbabwe kwenye mapambano ya kujipatia uhuru, wakati ule urafiki mkubwa kati ya nchi hizo mbili ulianzishwa, na sasa urafiki huo unazidi kuimarishwa.
Balozi wa China nchini Zimbawe Bw. Xin Shunkang alisema, katika miaka 29 iliyopita tangu China na Zimbabwe zianzishe uhusiano wa kibalozi kati ya, maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili yalileta maslahi makubwa kwa wananchi wake. China itaendelea kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na kuendelea kuhimiza amani na maendeleo barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |