• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Urithi wa Utamaduni Usioonekana wa China" Nyimbo za Jadi katika Kijiji cha Lujiahe

    (GMT+08:00) 2009-10-19 16:47:02

    Kijiji cha Lujiahe mkoani Hubei kinasifiwa kuwa ni "kijiji cha kwanza cha nyimbo za jadi za kabila la Wahan" nchini China. Kutokana na kufundishana nyimbo hizo wenyewe kwa wenyewe, wenyeji wa kijiji hicho wamehifadhi nyimbo za jadi zaidi ya elfu tano, sauti mbalimbali za nyimbo hizo zinafika 79. Mwezi Juni mwaka 2008 serikali iliziweka nyimbo za jadi za kijiji hicho katika orodha ya urithi wa utamaduni usioonekana nchini China.

    Jina la kijiji hicho lilitokana na jina la mto mdogo unaopita kwenye upande wa kusini mwa Mlima Wudang, kwenye kando mbili za mto huo kuna vijiji vitatu vyenye wakazi zaidi ya elfu mbili, moja kati ya vijiji hivyo ni kijiji cha Lujiahe. Kijiji cha Lujiahe kiko katikati ya mlima, mtu anapokuwa nje ya mlango anaweza kuona wazi vijiji, mashamba ya mpunga na mto unaopindapinda. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utamaduni ya mji wa Danjiangkou Bw. Chen Zhizhong alituambia akisema

    "Kijiji cha Liujiahe kina historia ndefu, kimehifadhi fasihi simulizi na mashairi ya kutoka Enzi ya Zhou Magharibi iliyoanzia mwaka 771 K.K hadi mwaka 1046. Nyimbo za jadi za Lujiahe zilienea kutokana na mahitaji ya kisiasa, kijeshi na kiuchumi, ambapo utamaduni wa dini ya Kidao ulichangia kuibuka kwa nyimbo hizo. Na kutokana na sehemu kilipo kijiji hicho, wakazi wake wameweza kupokea utamaduni kutoka maeneo ya mito ya Huanghe na Changjiang."

    Bw. Yao Qihua mwenye umri wa miaka 72 anasifiwa kuwa ni "mfuko wa nyimbo", kwani alikuwa anaweza kuimba nyimbo za jadi zaidi ya elfu moja. Alipokuwa katika ua nyumbani kwake, bwana huyo alianza kuimba.

    Ni kweli bwana huyo anastahili kusifiwa kuwa ni "mfuko wa nyimbo", kwani aliimba nyimbo mmoja baada ya mwingine kwa mfululizo hata kwa asubuhi nzima, kati ya nyimbo alizoimba kuna nyimbo zinazohusu hadithi za enzi za kifalme, kuna nyimbo za mapenzi zilizopinga mfumo wa kikabaila wa ndoa za lazima, kuna nyimbo zinazohusu maisha na pia kuna nyimbo walizoimba wenyeji walipokuwa wakifanya kazi nzito.

    Bw. Yao ni mtu mchangamfu, yeye anasema anapenda kujiburudisha kwa kuimba. Katika sikukuu fulani, au katika sherehe nyingine anapenda kuchangia shamrashamra kwa nyimbo zake, alijifunza kuimba nyimbo hizo kutoka kwa walimu wake wengi.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako