• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 1020

    (GMT+08:00) 2009-10-20 16:35:25

    Wasikilizaji wapendwa, karibuni katika kipindi hiki cha sanduku la barua. Leo kwanza tunawaletea barua tulizotumiwa kutoka kwa wasikilizaji wetu.

    Msikilizaji wetu Mbarouk Msabah wa Sanduku la posta 52483 Dubai United Arab Emirates ametuletea barua akisema, Ndugu watangazaji, kwanza kabisa ningependa kupongeza ziara ya tarehe 12 October mwaka huu iliyofanywa na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania TBC Bw. Tido Mhando mjini Beijing pamoja na kuwa na mazungumzo na Naibu Mkuu wa Redio China Kimataifa Bw.Wang Yunpeng. Kwa maoni yangu binafsi ziara hiyo itaweza kufunguwa njia muwafaka juu ya ushirikiano wa habari baina ya pande mbili pamoja na kuweka matumaini zaidi juu ya uwezekano wa kurusha matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimatifa kupitia mitambo iliyopo nchini Tanzania , ili matangazo hayo yaweze kuwafikia wasikilizaji wenu kwa njia ya urahisi zaidi ikilinganishwa na hivi sasa.

    Bila shaka sisi wasikilizaji wenu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa tunaelewa wazi juu ya hatua ambazo hazina budi kuchukuliwa kwanza kuhusu urushaji wa matangazo hayo , lakini bila shaka ziara ya Bw. Tido Mhando itakuwa ni ishara nzuri kabisa ya kufanikisha malengo hayo kwani hata Wahenga walisema " penye nia pana njia ".

    Mimi kama msikilizaji wenu nawatakieni kila la kheri na mafanikio katika mpango wa kuanzisha urushaji wa vipindi vya Redio China Kimataifa huko kwetu nchini Tanzania. Asanteni.

    Tunakushukuru sana Bw Mbarouk Msabah kwa barua yako, ni kweli hata sisi pia tunatumai kuwa mazungumzo yaliyofikiwa yataleta matunda mazuri na hatimaye tutaweza kufanikisha lile lengo tuliloliweka la kuwaridhisha zaidi wasikilizaji wetu wote wa maeneo hasa yale yasiyosikika vizuri matangazo yetu, kwani CRI inapenda wasikilizaji wake wote hasa wa Tanzania wafaidike na matangazo ya kila siku.

    Msikilizaji wetu Mutanda Ayub ambaye barua yake pepe ni ayub06@yahoo.com ametuletea barua akisema, akiwa kwa niaba ya mashabiki wa Bungoma na vitongoji vyake pokeeni salamu zisizo na hesabu mara kwa mara nyingine. Mbali na salamu nashukuru Mola kwa kunipa fursa hii iliyo bora zaidi niweze kuwafahamisha kuwa ninaendelea kufatilia vipindi hata zaidi.

    Kwa kipindi kilichomalizika cha Sanduku la Barua kweli niliweza kufuatilia maelezo ya mama chen na kwa kinagaubaga nilihisi kama niko kwenye studio kule Beijing kwenyewe. Nilipata kuelewa na kufahamu jinsi mambo Yalivyo na ndipo sasa ninamatumaini kuwa upendo tulionao na CRI bila shaka nitapata nafasi nyingini hata kama ni kujigharamia nauli ya ndege ni sharti nirudi CRI kabla ya miaka kumi sasa.Vilevile barua ambayo nimepokea inathibitisha vile ambavyo mnajali wasikilizaji wote bila ubaguzi wowote.

    Juzi niliongea kuhusu maoni ya kuhusisha kipindi kama vile Sauti ya Wasikilizaji, nitajaribu kueleza hii. Ingawa ni vigumu kujieleza hapa lakini hivi ndivyo mawazo yangu pamoja na washiriki tunaonelea; Ili vipindi viweze kuboreshwa zaidi tuwe na kipindi cha majadiliano na mahojiano kati ya watangazaji na wasikilizaji wa CRI kwa njia ya ujumbe mfupi, Barua pepe, na hata kupiga simu moja kwa moja ambapo wasikilizaji wataweza kupata fursa ya kutoa maoni yao bila kukawia. Ndipo kipindi hiki kitaweza kujulikakana kama Sauti ya Wasikilizaji.

    Vilevile katika kuwepo kwa kipindi hiki wasikilizaji waweze kupewa nafasi ya kutuma salamu au kutoa anwani zao kwa wale wanaohitaji mawasiliano haswa kwa marafiki. Jamaa zao kujuliana hali na fursa hii itawezesha Vilabu vya wasikilizaji kutoka pande zote za dunia kubadilishana maoni jinsi wanavyoendelea.

    Jambo lingine ni kuwa kuwe na angalau uwezekano wa wahariri au waandishi wa CRI kutembelea wasikilizaji hata ni kama mara moja kwa mwaka.Hii itakuwa njia moja ya kuleta ushirikiano na maelewano zaidi na ya kipekee. Kati ya wasikilizaji kutoka Kenya, Tanzania, Uganda , Rwanda, Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na Afrika kwa jumla.

    Kutembeleana huku kutakuwa na mwelekeo mzuri wa kuhakikisha uhusiano unadumu milele.Kwa mfano mimi nimejitolea kutoa shamba ili tuweze kupanda maua na miti tafauti tafauti na wasikilizaji wengine ili tuwe na Mandhari nzuri ya Radio China Kimataifa, ambayo tutawakaribisha mje mjionee na mule matunda ya Afrika palepale.kwani naamini kuwa sisi ni watu wa jamii moja yenye upendo wa kuigwa na wengi.

    Na Mutanda Ayub Shariff anasema katika barua yake nyingine kuwa, ni muda mrefu sijawaandikia barua ijapokuwa mimi ni mzima sasa baada ya kuwa na maumivu na shida hapa na pale. Jambo jema ni kuwa sijawahi kukosa kusikiliza matangazao ya CRI.

    Ni fursa nyingene nzuri ambayo nimetunukiwa na mwenye kuumba ardhi na mbingu kuweza kuwajulia hali wote katika idhaa ya kiswahili. Nina imani kuwa wote mu wazima na kazi yachapwa vilivyo.

    Nimekuwa mnyonge kidogo Afya yangu haijakuwa nzuri kwa siku kadhaa bali kwa sasa nahisi nafuu kidogo ingawa sijawa na uwezo wa kutuma maoni mara kwa mara hata hivyo nimekuwa nikitegea idhaa sikio kitandani mwangu.

    Kwa sasa nina furaha kwa yafuatayo kulingana na barua mwanzoni mwa mwaka tulikuwa na shughuli ya kuwa na uwezekano ya kurusha hewani matangazo ya CRI kupitia vituo vya utangazaji kama vile TBC. sijui juhudi hizo Zilifika wapi?lakini furaha yangu nikufahamu kuwa kwa sasa kuna mipango inayoendelea kuhakikisha kuwa wenzetu wa Nchi jirani wa Uganda wana matumaini ya kuweza kuisikia vizuri CRI hii inafuatana mkuu wa kituo cha habari na matangazo cha Unganda alivyo tembelea nchini china pamoja na kukutana na wasimamizi na watangazaji wa Radio China kimataifa. Hii sio juhudi ndogo kulingana na vile nilivyo pokea Moja kwa moja kwa Radio china tulikuwa na maelewano ya ushirikiano kuwepo karibuni.

    Jambo lingine kutangaza kwa mashindano ya chemsha bongo mwakani mapema ni jambo ambalo wasikilizaji wote wa Bungoma wamefurahia sana.Hata hivyo jambo linalo nitia baridi ni kusitaafu kwa mama Chen mwaka huu. Ombi langu Tunamkaribisha Bungoma Karamu ya Kustaafu kwake.

    Bw. Shariff anasema, nimeendelea kuburudika vilevile na nyimbo zilizo nziru kati ya vipindi haswa kwa kipindi cha salamu zenu. Kwa wakati huu natuma salamu zangu kwa wafuatao:

    Jendeka Goldah wa Nambuku Estate, Richard Mutanda wa Mahuma. David Wekesa wa Nalondo,Wycliffe Mulunda Khaoya wa Ruwanda, Pilot Moses Wanjala wa Sang'alo, Mbarouk Msabah Mbarouk wa Dubai Emirates, Mogire Machuki wa Kisii Kenya, Stephen Makoye Kumalija wa Tanzania, Xavier Telly Wambwa wa Bongoma Kenya, Jennifer Wafula wa Khaoya Primary, Elizabeth Wafula wa Sianda

    Ujumbe wake unasema, Madam Jennifer na Bi. Elizabeth Wafula poleni kwa shida mlizopata na msisahau kusikiliza CRI kila siku.

    Shukurani msikilizaji wetu Mutanda Ayub kwa maoni yako ambayo umeyatoa, na kubwa ni kukwambia tu tutayafanyia kazi kwa yale ambayo yapo kwenye uwezo wetu na kwa yale ambayo yako nje ya uwezo wetu au utekelezaji wake unahitaji muda tunaomba utuwie radhi.Aidha tunapenda kukuambia kuwa juhudi za kurusha matangazo ya CRI zimefikia pazuri kwani mazungumzo yaliyofikiwa wakati mkuu wa TBC alipotembelea CRI yanatia matumaini mazuri hivyo usiwe na hofu kwa hilo, Pia napenda kukutoa wasiwasi kwamba muda wangu wa kustaafu bado haujafika na ninaendelea kuchapa kazi kama kawaida kwahiyo usitie shaka wala usiwe na baridi kwa hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako