• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shamba la ukoo wa Mou, mkoani Shandong

    (GMT+08:00) 2009-10-26 21:16:16

    Kundi kubwa la majengo ya ukoo wa Mou liko kwenye sehemu ya kaskazini ya mji wa Qixia, majengo hayo yalianza kujengwa katika enzi ya mfalme Yong Zheng ya Qing (mwaka 1723-mwaka 1735), na ujenzi wake ulikamilika katika miaka ya 30 ya karne iliyopita. Majengo hayo ni makazi binafsi yaliyojengwa na ofisa Mou wa huko. Shamba zima lina eneo la mita za mraba zaidi ya elfu 20, makazi hayo yana sehemu tatu zenye nyua 6 na nyumba zaidi ya 480, ambazo ziko hadi hivi sasa. Nyumba hizi zilijengwa kwenye mstari wa katikati ya shamba, na nyumba zilizoko upande wa kushoto wa mstari zinafanana na nyumba zilizoko upande wa kulia, mtindo wake ni sawasawa na majumba ya zamani ya mfalme ya Beijing, hivyo yanaitwa "majumba madogo ya mfalme ya kienyeji".

    Mji Qixia uko kwenye sehemu ya bara, huko kuna milima na mawe mengi, kwa hiyo vinyago na sanamu za mawe zilizotengenezwa na mafundi stadi zinaonesha zaidi umaalumu wa shamba la ukoo wa Mou. Ngoma mbili za mawe zilizoko kwenye kando mbili za lango la shamba hilo ni mfano wa vinyago vya mawe vya shamba la Mou. Ngoma hizi zilitengenezwa na mafundi wanne kwa miaka 3. Kila ngoma ina kimo cha mita 1.5 na uzito wa kiasi cha tani 1, juu ya ngoma hizo imechongwa michoro ya jadi ya China ya kuomba baraka.

    Vinyago na sanamu karibu zote zilizoko kwenye shamba la Mou zilitengenezwa na mafundi kwa umakini sana, na kugharimu fedha nyingi. Mwanachama wa taasisi ya mila na jadi za watu ya China Bi Xu Xiaobin alieleza.

    "Kipande hiki cha ukuta ni maarufu sana, mwenye shamba wa kizazi cha pili Mou Zuo alikubali kutumia fedha nyingi kutengeneza mawe yaliyotumika kujenga ukuta huu. Mawe zaidi ya 660 ya kujenga ukuta yaligharimu mchele zaidi ya kilo 16,500. Kila jiwe lilikatwa barabara kwa kufuata vipimo, kisha lilinolewa kwa maji, hivyo mawe yote ni laini sana, na ukuta huu unaonekana ni kama ukuta mzima usio na ufa."

    Kila jiwe, tofali na mbao kwenye shamba la Mou vilisanifiwa kwa makini, na kuonesha mtazamo na matarajio ya mwenyewe. Mwongoza watalii Bi Sun Jia alisema,

    "Tunachoona sasa ni sehemu ya nje ya ukuta wa ghala moja la kawaida la shamba hilo, kuta za ghala hili zilizojengwa na mafundi kwa vipande vya mawe, zina michoro 145 ya maua yanayochukuliwa kama ni vitu vya baraka katika jadi ya China, hata mawe hayo baridi na magumu yamekuwa ya vitu vya sanaa."

    Shamba la ukoo wa Mou lina maajabu 9 kwenye historia ya ujenzi wa majengo, mbali na ngoma za mawe, maajabu mengine mawili ni matofali ya rangi ya kijivu na vigae vya kuezekea mapaa ya nyumba vilivyotiwa rojo ya maharage yaliyosagwa pamoja na kuta zilizotiwa misumari mikubwa ya mawe magumu ya granite. Kabla ya kujenga, matofali na vigae vyote vinavyotumiwa kwa shamba hilo vilitiwa katika rojo ya maharage yaliyosagwa, ili kufanya kuta za nyumba zisifyonze maji ya mvua na kuwa imara na kudumu kwa miaka mingi. Kutiwa misumari mikubwa ya mawe kwenye kuta, kulikuwa na lengo la kufanya kuta nene na zenye kimo kikubwa ziwe imara zaidi.

    Maskani ya asili ya ukoo wa Mou yako katika mkoa wa Hubei, kwa hiyo kwa jumla majengo ya shamba ya ukoo wa Mou licha ya kuwa na taadhima na ufahari, yalijengwa na kupambwa kwa makini. Wakati shamba la ukoo wa Mou lilipokuwa likijengwa, ukoo huo ulituma kwa mara nyingi maseremala na waashi waende kufanya uchunguzi na kujifunza kwenye sehemu ya kusini, hivyo sanaa za majengo za sehemu za kusini na kaskazini zimeunganishwa vizuri kwenye majengo ya shamba la ukoo wa Mou.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako