• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wanaojitolea waimarisha urafiki kati ya China na Laos kwa moyo wa upendo

    (GMT+08:00) 2009-10-30 14:58:06

    Mpango wa utoaji huduma za kujitolea kwa vijana wa China katika nchi ya Laos unaandaliwa na kamati kuu ya Umoja wa vijana wa China na wizara ya biashara kwa ajili ya kuongeza maingiliano kati ya China na Laos. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2008, shirikisho la vijana wanaojitolea la Shanghai lilituma vikundi 7 vyenye vijana 81 wanaojitolea, ambao walitoa huduma za matibabu, elimu, usimamizi wa makampuni, sayansi na teknolojia za kilimo na nyinginezo.

    Yu Lei ni kijana mwenye umri wa miaka 30 hivi, anafanya kazi katika idara inayoshughulikia mambo ya vijana ya Umoja wa vijana wa China mjini Shanghai. Mwezi Januari hadi Julai mwaka 2008 alikuwa mkuu wa kikundi cha 7 cha vijana wanaojitolea wa Shanghai cha kutoa huduma nchini Laos, na kufundisha lugha ya Kichina katika kituo cha utoaji mafunzo kwa vijana huko Vientiane nchini Laos. Alisema,

    "Bado ninakumbuka siku nilizokuwepo nchini Laos, zilikuwa siku zenye furaha kubwa."

    Kwenye blog ya Bw. Yu Lei, aliandika hivi: Laos ni nchi yenye furaha, Walaos si wagumu wa kuonesha tabasamu zao. Barabarani unaweza kusikia salamu kila mahali, na tabasamu zao zinaweza kukuondoa wasiwasi wa watu mara moja. Bila kujali kama ni watu wanaokufahamu au la, walikutana na wewe watakusalimia. Na vijana wetu wameleta desturi hii nchini China.

    Hivi sasa, baada ya kurudi kutoka Laos, Bw. Yu Lei anaishi kama kawaida mjini Shanghai kama alivyoishi zamani, pia anafuatilia habari kutoka Laos. Alisema,

    "Sasa mtandao wa internet umeendelezwa sana, ninawasiliana na wanafunzi na marafiki zangu wa Laos kwa barua pepe na kwenye MSN. Kila mara wananiuliza kama nina pilikapilika au la, na kuuliza hali ya maisha yangu. Mimi pia ninawauliza kama wanaendelea kujifunza lugha ya Kichina mara kwa mara au la."

    Bw. Yu Lei alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, alipokuwa Laos alijifunza maneno karibu 100 ya Kilaos. Sasa amerudi mjini Shanghai, lakini baadhi ya wakati alipozungumza na jamaa zake, anatumia maneno machache ya Kilaos, kwani Laos imemwachia kumbukumbu nyingi nzuri. Alisema,

    " Nawapenda watu wa Laos, na naipenda Laos."

    "Mimi naitwa Gu Junqing, ni mmoja wa kikundi cha 6 cha utoaji huduma cha vijana wanaojitolea wa Shanghai, China, nilishughulikia kazi ya akyupancha na usingaji katika hospitali ya 109 ya Laos. Muda wangu wa nusu mwaka nchini Laos sitausahau katika maisha yangu."

    Bw. Gu Junqing anafanya kazi ya kutoa tiba ya kichina katika kitengo cha magonjwa ya mifupa cha hospitali ya Guanghua mjini Shanghai. Alisema ingawa Kiingereza chake sio kizuri, lakini kilimsaidia aliyokuwa nchini Laos, kwani aliweza kujitumbukiza kabisa katika lugha ya Kilaos, na kuifahamu Laos zaidi. Alisema,

    "Nilikuwa na marafiki wawili wa Laos katika hospitali, mmoja anafahamu Kichina, na mwingine anafahamu Kiingereza, lakini katika muda ambao sikuwa nao, nilikuwa peke yangu kuwatibu wagonjwa. Nchini Laos watu wengi huwa wanaumwa shingo na kiuno, hivyo wagonjwa hao wa Laos wakija walikuwa wanaweza kunionesha sehemu zenye maumivu, bila haja kusema maneno."

    Muziki mzuri wa Laos uitwao Mkulima mwenye furaha, ni mlio wa simu ya mkononi ya Bw. Gu Junqing. Si rahisi kusikia mlio kama huu mjini Shanghai. Bw. Gu Junqing alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, baada ya kurudi Shanghai, kama akijisikia kutokuwa na furaha alikuwa anasikiliza nyimbo za Laos. Hivi sasa, kuna nyimbo nyingi kutoka Laos kwenye simu yake ya mkononi, ingawa hajui kuimba, lakini anaona ni nyimbo nzuri. Alisema,

    "Nilitengeneza maonesho ya kompyuta ya PPT kuhusu Laos, niliona kuwa PPT hii ina thamani zaidi, kwa sababu niliitumia kutoa mihadhara kumi kadhaa kwa vijana, ambayo inafahamisha kazi na maisha yetu nchini Laos."

    Xu Jin ni katibu wa kamati ya Umoja wa vijana ya Chuo kikuu cha Donghua mjini Shanghai, pia ni mkurugenzi wa kituo cha elimu ya sanaa cha chuo hicho. Mwaka 2006 aliwahi kuwa mmoja wa kikundi cha 5 cha vijana wanaojitolea wa Shanghai kwenda Laos, na kufundisha kompyuta nchini Laos. Alisema,

    "Niliamka saa kumi na mbili na nusu asubuhi, na kuondoka saa moja, halafu nilitumia muda wa nusu saa kwenda shuleni kwa baiskeli, saa mbili na nusu hadi saa sita asubuhi niliwafundisha ujuzi rahisi wa kompyuta, alasiri niliwafundisha watoto lugha ya Kichina, au nilisoma vitabu, halafu nilirudi kwenye hoteli ya vijana niliyofikia."

    Alipozungumzia maisha yake nchini Laos katika miaka mitatu iliyopita, Xu Jin alisema, wanafunzi walijiandikisha kutoa huduma za kujitolea kwa hiari, miongoni mwa walikuwepo watawa, wanafunzi wa vyuo vikuu na maofisa wa serikali darasani. Lugha za Kichina, Kiingereza na Kilaos huchanganywa katika mafunzo darasani, kweli ni hali ya kufurahisha. Alisema,

    "Alikuwepo mwanafunzi wa kike wa chuo kikuu, ambaye anajua kuongea Kiingereza tu. Siku moja katika darasa la kupiga taibu kwa kompyuta, aliniuliza namna ya kusema 'nakupenda' kwa Kichina, alikuwa hajui kuandika maneno hayo ya kichina kwenye kompyuta, hivyo nilimwambia matamshi ya maneno hayo. Darasa lilikuwa karibu kumalizika, aliniita nikaona maneno ya Kiingereza I LOVE YOU kwenye kompyuta yake, pia kwa maneno ya Kilaos chini ya yale ya Kiingereza, halafu aliniambia kwa Kichina nakupenda."

    Baada ya kumaliza kazi ya kujitolea nje ya nchi na kurudi mjini Shanghai, hivi sasa Xu Jin anatumia muda mwingi zaidi katika usimamizi wa watu wanaojitolea wa chuoni kwa sehemu za magharibi za China. Uzoefu wake nchini Laos umemfanya awe na uelewa mpya. Alisema,

    "Ni lazima kuwa na moyo huo katika kazi za kila siku, ambao ni kupenda kuwasaidia wengine. Sasa nina matakwa ya hali ya juu zaidi kwa wanafunzi hawa wanaojitolea, naona kuwa haitoshi kukamilisha majukumu yao katika sehemu wanazokwenda kutoa huduma, nawataka waweze kufikiri kuwa, wanaweza kufanya nini zaidi?"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako