• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matairi ya magari yaliyotumika yanachangia kuwepo kwa 'uchumi usio na uchafuzi'

    (GMT+08:00) 2009-11-03 15:55:05

    Matairi ya magari yaliyotumika yanajulikana kuwa ni 'uchafuzi mweusi' kote duniani, ambao unasababisha uharibifu wa ardhi na kukua kwa vijidudu. Kampuni ya sayansi na teknolojia ya Haitai ya Tianjin ilianza kufanya utafiti kuhusu matumizi ya matairi yaliyotumika katika miaka mitano iliyopita, hivi sasa kampuni hiyo imefanyikiwa kubadilisha matairi yaliyotumika kuwa raslimali za aina mpya za kutandika barabara, mpaka sasa matairi milioni 3 yaliyotumika yametumiwa tena, na kupunguza matumizi ya tani elfu 30 za mafuta ghafi. Sasa tunawaelezeni kuhusu namna kampuni hiyo ilivyoweza kubadilisha 'uchafuzi mweusi' na kuchangia 'uchumi usio na uchafuzi'.

    "katika chumba kile kidogo kweli kila mahali kulikuwa kumejaa makarai yenye lami, wakati nilipowaita wanifungilie mlango, nilijiuliza ni vipi utafiti wa kuhimiza uchumi usio na uchafuzi unafanyika katika chumba kidogo namna hii? Lakini baada ya viongozi kutoka, waliniambia kwamba, 'tunajua hutaki kuja kufanya utafiti katika maabara hii, kwa sababu hakuna vifaa vya kisasa na mazingira sio mazuri, lakini tuna imani kwamba tutaweza kupata mafanikio makubwa katika maabara hii."

    Aliyesema hayo ni maneja mkuu wa kampuni ya sayansi na teknolojia ya Haitai ya Tianjin Bw. Yu Qiang, yeye ni mmoja kati ya watu waliojitahidi kufanya utafiti na kueneza teknolojia za kutandika barabara kwa kutumia matairi yaliyotumika. Kampuni yake ina vifaa na teknolojia za kisasa zinazoongoza katika eneo hilo duniani ambavyo vyote vilisanifiwa katika chumba hicho kidogo. Kutandika barabra kwa matairi yaliyotumika, ni kuyasaga matairi hayo, na kuchanganywa na lami na kokoto na kushughulikiwa kwa njia ya kikemikali na kifizikia, mwishoni mchanganyiko huo unatumika kutandika barabara.

    Kutoka mji wa Tianjin kwenda kaskazini hadi kwenye barabara ya mwendo kasi ya Tianjin hadi Tangshan, sehemu moja ya barabara ambayo ina rangi ya nyeusi zaidi na ni laini zaidi ndiyo ilitengenezwa kwa kutumia matairi yaliyotumika. Msimamizi wa sifa ya mradi wa ujenzi wa barabara Bw. Zhou alisema:

    "tunatia unga la matairi yaliyotumika kwenye lami, kufanya hivyo tunaboresha kwa ufanisi uwezo wa lami, kuimarisha nguvu ya mchanganyiko wa lami, kwa njia hii inaweza kupunguza unene wa lami inayotandikwa barabarani na kupunguza gharama."

    Kwenye barabara iliyotengenezwa kwa njia hiyo magari yanatoa kelele ndogo zaidi ikilinganishwa na kwenye barabara ya kawaida; Aidha uwezo wa barabara ya aina hiyo wa kuhimili joto na baridi umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 20 kuliko ule wa barabara ya kawaida, pia inaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi. Mbali na hayo, kutandika kilomita moja ya barabara kwa njia hiyo kunatumia matairi 6000 yaliyotumika na kupunguza gharama kwa zaidi ya yuan laki tatu. Maneja mkuu wa kampuni ya sayansi na teknolojia ya Haitai ya Tianjin Bw. Yu Qiang alisema:

    "matairi yaliyotumika haziwezi kutumiwa tena kwenye magari, lakini vitu vingi vya matairi hayo vinaweza kutumika, muda wa matumizi ya matairi ni miaka 50 hadi karne moja, na matiari yana vitu vingi vinavyoweza kutumika, ukiwemo mpira wa asili, kaboni na kemikali ya Permanax CD, ambavyo vyote ni rasilmali muhimu kwa uzalishaji."

    Bw. Yu Qiang alikuwa hana ufahamu hata kidogo kuhusu matairi yaliyotumika. Kampuni ya biashara na nje ambayo aliyofanya kazi iliwahi kushinda mara tatu zabuni za miradi ya kushughulikia matairi yaliyotumika kwenye sehemu kadhaa ikiwemo Macau, ambayo ilimfungulia Bw. Yu Qiang mlango wa ghala kubwa la matairi yaliyotumika. Mwaka 2003 Bw. Yu Qiang aliunda kikundi chake na kuanza utafiti wa shughuli hiyo. Lakini alikumbwa na taabu kubwa zaidi kuliko alivyodhani mwanzoni.

    Matairi yaliyotumika yanaweza kutumika kwa njia mbalimbali. Katika miaka ya 80 China ilianzisha shirikisho la kutengeneza upya matairi yaliyotumika, lakini mwanzoni njia za kutumia matairi hayo ilikuwa ni kuyatengeneza upya, au kuyayeyusha na kutengeneza bidhaa ndogo za mpira. Mkurugenzi wa taasisi ya sayansi ya vichocheo katika chuo kikuu cha Nankai cha China Prof. Liu Shuangxi alisema:

    "matairi yaliyotumika ni suala gumu duniani, ambalo bado lipo katika nchi zilizoendelea kabisa kichumi ikiwemo Marekani, matairi hayo yanaweza kusababisha ajali ya moto au kuwa mazalia ya mbu na inzi, jambo ambalo ni baya kwa maisha ya wakazi wanaoishi sehemu za karibu. Kwa mfano wa kampuni zetu za kuyeyusha matairi yaliyotumika kuwa raba, hasa kwa njia zile za zamani, pia zinaweza kutoa kiasi fulani cha uchafuzi."

    Kwa muda mfupi tu, kikundi cha Yu Qiang kilisanifu vifaa vya kwanza vya kutengeneza lami inayochanganywa na vipande vya matairi yaliyotumika. Lakini suala la pili linalowakabili ambalo ni muhimu kabisa ni ustadi wa kiteknolojia. raslimali ya kutandika barabara inaweza kutumika ndani ya saa 48 tu, ama sivyo itakauka na kutoweza kutumika tena. Kama raslimali hiyo ikitengenezwa viwandani na kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara kote nchini, basi zitakauka kabla haijafika kwenye sehemu ambako itatumika. Kutokana na hali hiyo, Bw. Yu Qiang alifikisha suala hilo la kiteknolojia kwa watafiti wa vyuo vikuu mbalimbali.

    Baada ya kufanya utafiti wa zaidi ya miezi 5, muda wa kuhifadhia raslimali za mchanganyiko wa lami umeongezeka kwa sasa ambao ni kutoka saa 48 hadi kufikia mwezi mmoja wa sasa, viwango vingine vya lami ya aina hiyo vyote vimeinuka kwa kiasi kikubwa.

    Hivi sasa barabara na madaraja ya ngazi ya juu yaliyojengwa kwa kutumia matairi yaliyotumika yanaonekana kwenye sehemu nyingi nchini China, na kampuni ya sayansi na teknolojia ya Haitai ya Tianjin iliyowekeza mapema katika utafiti wa teknolojia hiyo imeendelea kuwa na mitaji ya zaidi ya yuan milioni 100 katika muda wa miaka mitano, na mpaka sasa barabara yenye urefu wa kilomita 400 zilijengwa kwa kutumia matairi milioni 3 yaliyotumika, ambayo ni sawa na kupunguza matumizi ya tani elfu 30 za mafuta ghafi na kubana matumizi ya zaidi ya yuan milioni 100. prof. Liu Shuangxi alisema:

    "mifuko ya plastiki ni uchafuzi mweupe, kwa hiyo matairi yanayotumika ni uchafuzi mweusi, kama tunaweza kuzitumia kihalisi, basi matairi hayo hayatakuwa tena uchafuzi bali yatakuwa ni ghala kubwa la raslimali. Kwa hiyo kwa upande huu, matumizi ya matairi hayo pia ni uchumi usio na uchafuzi.'

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako