• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia yenye furaha inayoundwa na mke na mume kutoka nchi mbili tofauti

    (GMT+08:00) 2009-11-05 15:07:44

    Kadiri uhusiano wa kirafiki kati ya China na Laos unavyoendelezwa siku hadi siku, ndivyo ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni unavyoimarishwa, na ndivyo mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili yanavyokuwa ya karibu siku hadi siku. Wachina na Walaos wengi zaidi wanafahamiana, hata wanaoana na kuunda familia zenye furaha.

    Mliosikia ni wimbo ulioimbwa na msichana Jingjing, ambao ni wimbo wa kabila la Wadai la China uitwao "Tausi wa dhahabu anayeruka ruka". Msichana huyo anaimba vizuri, na anatamka vizuri maneno ya Kichina kwenye wimbo huo. Lakini mama yake ni Mlaos halisi, anaitwa Phukham Ongvichit.

    Bibi Phukham alizaliwa nchini Laos, ni Mlaos halisi. Mwaka 1996 ulikuwa na mradi wa ushirikiano kati ya China na Laos, Bw. Cheng Xiaoyang akiwa mtaalam wa China alitumwa nchini Laos, ambapo alikuwa na mawasiliano na mama wa Phukham katika shughuli za mradi huo. Bw. Cheng Xiaoyang na Phukham walifahamiana kupitia kufahamishwa na rafiki wa mama wa Phukham. Baadaye Bw. Cheng Xiaoyang alirudi nchini China, ingawa walikuwa mbali sana, lakini waliwasiliana kwa barua kwa miaka miwili. Mwaka 1999 Bw. Cheng Xiaoyang alikwenda tena Laos na kuomba kufunga ndoa na Phukham. Alipokumbuka hali ya wakati ule, Bibi Phukham bado alikuwa na furaha kubwa. Alisema,

    "Mwaka 1999 aliporudi tena nchini Laos, aliniomba tuoane. Kufunga ndoa ni jambo kubwa, mimi ni binti pekee katika familia yangu, na nina kaka wawili wadogo, ambao bado wanasoma. Wakati ule nilikuwa na furaha kubwa, lakini ili kufunga ndoa ilikuwa ni lazima nipate idhini ya mama yangu. Hatimaye nilikubali, kwa kuwa naona yeye ni mtu mwema anayeweza kubeba wajibu. Pia aliwahi kumwambia mama yangu kuwa, atabeba wajibu na kunilinda vizuri."

    Bw. Cheng Xiaoyang hakujifunza rasmi lugha ya Kilaos chuoni, lakini alipozungumza na mwandishi wetu wa habari, anajua kuongea lugha ya Kilaos. Alisema katika miaka ile aliyofanya kazi nchini Laos, alikuwa na hamu kubwa ya kujifunza lugha ya Kilaos, alisema,

    "Kilaos ninachoongea nilijifunza nchini Laos. Wakati ule nilitumia zaidi lugha za Kichina na Kiingereza, lakini kutokana na kufahamiana na Phukham, nilianza kujifunza lugha ya Kilaos kwa bidii, la sivyo nisingeweza kumwoa."

    Mwaka 1999 Bw. Cheng Xiaoyang na Bibi Phukham walirudi mjini Beijing baada ya kuoana. Akilinganisha hali ya maisha nchini Laos, mji mkubwa wa Beijing ulimpa Bibi Phukham hisia tofauti, alisema,

    "Bado ninakumbuka kuwa siku moja baada ya kuja hapa, nilikwenda kutembelea bustani, kulikuwa na watu wengi, na nilitumia zaidi ya saa moja kutembea kutoka mlango wa mbele hadi mlango wa nyuma. Nchini Laos watu wengi wanakusanyika wakati wa sikukuu tu, lakini mjini Beijing, naona kila siku kuna watu wengi. Hisia hiyo sitasahau."

    Kuanzia mwaka 1999 hadi 2009, Bibi Phukham pia ameshuhudia mabadiliko mapya ya Beijing. Yeye pia amenunua gari. Alisema,

    "Nilikuja hapa Beijing mwaka 1999, hadi leo miaka 10 imepita, na mji wa Beijing una mabadiliko makubwa. Ujenzi wa mji na mawasiliano ya barabarani vimepata maendeleo makubwa, na uchumi wake unastawisha. Majengo marefu yanajengwa. Kutokana na maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing, kazi ya ujenzi wa mji wa Beijing imepata maendeleo makubwa zaidi. Mazingira ya maisha pia yameboreshwa sana. Kwa mfano, miaka 10 iliyopita, mabasi yalitumia mafuta, lakini hivi leo mengi yanatumia nishati ya mseto wa umeme na petroli. Kama usipotembelee sehemu moja kwa miaka miwili au mitatu, ukienda unaweza kupotea njia, kwani kuna mabadiliko makubwa. Magari binafsi pia yameongezeka, na mawasiliano ya umma pia ni rahisi."

    Miaka 10 imepita, Bibi Phukham sasa ana mabinti wawili. Mwanzo mwa kipindi hiki, ulisikia sauti ya msichana mmoja aliimba, msichana huyo ni binti mkubwa wa Bibi Phukham Jingjing. Ana umri wa miaka 8, na anasoma katika shule ya msingi ya Wuyi mjini Beijing. Binti mdogo Jiajia ana umri wa miaka zaidi ya mitano, anasoma katika shule ya chekechea mjini Beijing. Wasichana hao wawili wanapendeza sana kama malaika. Licha ya kusoma, vilevile wanajifunza kupiga kinanda, kuimba na kuandika.

    Ingawa sasa wanaishi hapa Beijing, lakini kila mwaka, Bw. Cheng Xiaoyang na Bibi Phukham wanatumia mapumziko marefu ya shule kwenda nchini Laos, na kukutana na jamaa za huko.

    Wasichana hao pia wana hisia maalum na maskani ya mama yao, katika mioyo yao, wana picha ya kupendeza kwa Laos. Jingjing alisema,

    "Nimekwenda Laos mara nyingi, naipenda Laos, huko kuna watawa wengi na mahekalu mengi, kila familia ina vila, hakuna mitaa, ni tofauti na Beijing."

    Jiajia alisema,

    "Nampenda tembo wa Laos, ana tumbo kubwa na mnene, pia anaweza kusafirisha magogo."

    Bw. Cheng Xiaoyang ana matumaini kuwa, mabinti zake watakwenda Laos mara kwa mara, wakati wanapojifunza ujuzi nchini China, pia wanafahamu utamaduni wa Laos, ili kutoa mchango zaidi na kuzidisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

    Kadiri uhusiano kati ya China na Laos unavyoendelezwa siku hadi siku, ndivyo mawasiliano ya watu wa nchi hizo mbili yanavyokuwa karibu siku hadi siku, na familia kama ya Bw. Cheng Xiaoyang na Bibi Phukham pia zitazidi kuongezeka siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako