• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuala Lumpur-Rais Hu Jintao wa China awasil Kuala Lumpur, Malaysia

    (GMT+08:00) 2009-11-10 16:03:22
    Kutokana na mwaliko wa kiongozi mkuu wa Malaysia, rais Hu Jintao wa China tarehe 10 amewasili Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia kuanza ziara yake nchini humo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Bw. Anifah Aman, waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Ong Tee Keat na maofisa wengine wa Malaysia, maofisa wa ubalozi wa China nchini humo na wajumbe wa wachina wanaoishi nchini humo walikwenda uwanja wa ndege kumlaki rais Hu Jintao.

    Alipowasili uwanja wa ndege Rais Hu Jintao ametoa hotuba ya maandishi akipongeza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Malaysia. Amesema China na Malaysia ni nchi zinazoendelea zilizoko sehemu ya Asia na Pasifiki, zina maslahi mengi ya pamoja. Ameeleza matumaini kuwa ziara yake hiyo inaweza kuongeza maelewano na urafiki kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili na kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili uinuke kwenye kiwango kipya.

      

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako