• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Singapore-Rais Hu Jintao akutana na ofisa mkuu wa mkoa wa utawala maalum wa Hongkong Bw. Donald Tsang Yam Kuen

  (GMT+08:00) 2009-11-14 15:42:28
  Rais wa China Hu Jintao na mkewe Liu Yongqing tarehe 14 huko Singapore wamekutana na ofisa mkuu wa mkoa wa utawala maalum wa Hongkong Bw. Donald Tsang Yam Kuen na mkewe ambao wako huko kuhudhuria mkutano wa 17 usio rasmi wa Jumuia ya APEC, na walikula chakula cha asubuhi kwa pamoja. Bw. Tsang Yam Kuen ametoa ripoti kwa rais Hu kuhusu hali ya hivi sasa ya Hongkong, akishukuru serikali kuu ya China juu ya ufuatiliaji na uungaji mkono wake kwa Hongkong katika kukabiliana na msukosuko wa fedha wa kimataifa. Rais Hu Jintao amesifu sana juhudi za serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hongkong kwa ajili ya kulinda utulivu wa mambo ya fedha ya Hongkong na mwelekeo wa utawala wake katika siku zijazo. Na ameitaka serikali ya mkoa wa Hongkong iendelee kufuatililia zaidi hali ya mambo ya uchumi na fedha duniani, ili kufanya vizuri kazi ya kuikabili, kuhimiza zaidi maendeleo ya uchumi wa Hongkong na kuboresha maisha ya wakazi, na kusukuma mbele usitawi na utulivu wa Hongkong.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako