• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Singapore-Rais Hu Jitnao akutana na mwenyekiti wa heshima wa Chama cha Kuomintang cha China Bw. Lian Zhan

  (GMT+08:00) 2009-11-14 15:43:31
  Katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China Bw. Hu Jintao tarehe 14 huko Singapore alipokutana na mwenyekiti wa heshima wa Chama cha Kuomintang cha China Bw. Lian Zhan, alieleza matumaini yake kuwa vyama hivyo viwili na pande mbili za China bara na Taiwan zitaimarisha mawasiliano na mazungumzo, kuongeza uaminifu wa kisiasa, kuwa na imani imara, kufanya mambo mengi halisi, na kuhimiza uhusiano kati ya China bara na Taiwan upate maendeleo mapya. Amesisitiza kuwa pande mbili zingejitahidi kuanzisha mchakato wa kufikia makubaliano ya jumla kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya China bara na Taiwan, wakati huo huo pande mbili zingefanya juhudi kwa pamoja ili kutatua matatizo ya kisiasa katika siku zijazo. Bw. Lian Zhan amekubaliana na Bw. Hu Jintao, akisema tokea mwaka jana uhusiano kati ya Taiwan na China bara unaendelezwa kwa hatua madhubuti, na umepata mafanikio ya kufurahisha. Ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande mbili unapanuliwa na kuendelezwa kwa kina siku hadi siku, ana matumaini kuwa pande hizo mbili zitapiga hatua ijayo ya kuharakisha mchakato wa kufikia makubaliano ya jumla ya ushirikiano wa kiuchumi.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako