• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msomi wa kabila la Wamongolia Bw. Batu

    (GMT+08:00) 2009-11-26 16:29:32

    Bw. Batu alizaliwa mwaka 1952 katika familia moja ya wafugaji mkoani Xinjiang. Baada ya kuhitimu masomo kwenye chuo kikuu, kwa nyakati tofauti alikuwa mwalimu, mwanariadha na mkalimani. Bw. Batu alisema kazi ya ualimu ilimsaidia kuinua sana kiwango chake wa lugha za kihan na kiuyghur. Alisema,

    "Sikuwafundisha wanafunzi wa kabila la Wamongolia tu, bali pia niliwafundisha wanafunzi wa kabila la Wahan lugha ya kiuyghur, na kuwafundisha wanafunzi wa Wauyghuur lugha ya kihan. Wakati huo huo kiwango changu cha lugha za kihan na kiuyghur pia kiliinuka sana."

    Kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kuwa na uwezo mkubwa wa lugha, Bw. Batu aliajiriwa na ofisi ya mabaki ya kale ya kamati ya makabila na dini ya mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur, na kuanza kushughulikia kazi ya kutafuta, kurekebisha na kuchapisha vitabu kuhusu mabaki ya kale ya makabila madogo madogo mkoani Xinjiang. Kazi hiyo ilimfanya Bw. Batu awe mpenzi wa utamaduni wa kabila la Wamongolia. Alisema,

    "Baada ya China kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, shughuli za utamaduni pia zimeendelezwa kwa kasi, na watafiti wa utamaduni wanaongezeka siku hadi siku. Mwaka 1989, tuliandaa maonesho ya matokeo ya utafiti wa Utenzi la Jiangger ambalo ni utenzi maarufu la kihistoria la kabila la Wamongolia."

    Utafiti wa lugha ni kazi ya kuchosha ambayo inahitaji ujuzi wa matawi mbalimbali ya sayansi, na utafiti wa lugha za makabila madogo madogo ni mgumu zaidi kutokana na uchache wa watu wanaoitumia na upungufu wa data zinazohusika. Mkoani Xinjiang kuna wamongolia karibu laki 1.8 tu, na wengi kati yo wanaishi milimani, hivyo kufanya utafiti wa lugha ya kimongolia mkoani humo kweli ni kazi ngumu sana.

    Bw. Batu alisema ili kuthibitisha hadithi au setensi moja ya kimongolia, mara kwa mara anakwenda milimani kutafuta wazee wa kabila la Wamongolia ili kuwauliza. Bw. Batu alisema anapokuwa na mradi wa utafiti, kwa kawaida analala kwa saa tano tu kila siku. Lakini anapenda sana kazi hiyo, kwani anaona kazi hiyo ni muhimu sana, inaweza kuwasaidia wamongolia kufahamu historia yao.

    Mwaka 1985, Shirika la Oirats linaloshughulikia utafiti wa elimu za kabila la Wamongolia lilianzishwa mkoani Xinjiang, na mwaka 1999, Shirika la kitaifa la Utafiti wa Jiangger lilianzishwa. Mashirika hayo yaliweka msingi imara kwa maendeleo ya utamaduni wa kimongolia mkoani Xinjiang. Bw. Batu alisema,

    "Zamani mkoani Xinjiang hakuwa na shirika linalojiendesha la utafiti wa elimu za kimogolia. Kuanzishwa kwa mashirika hayo pia kumeonesha maendeleo ya utafiti wa utamaduni wa kabila letu."

    Bw. Batu sasa ni mkurugenzi wa ofisi ya pili inayoshughulikia mambo ya kidini ya kamati ya mambo ya makabila na dini ya mkoa wa Xinjiang, na kila siku ana shughuli nyingi ofisini. Bw. Batu pia ni naibu mkuu wa Shirika la kitaifa la Utafiti wa Jiangger na Shirika la Oirats ambalo linashughulikia utafiti wa elimu za kabila la Wamongolia. Baada ya kuondoka kazini, anapenda kutumia wakati wake katika kusoma na kutafsiri data kuhusu historia na utamaduni wa kabila la Mongolia, kwani anaona kuwa kurithi na kuendeleza utamaduni wa kabila la Wamongolia ni wajibu wake. Alisema,

    "Kwa kupitia mashirika hayo, shughuli za utamaduni wa kabila la Wamongolia mkoani Xinjiang zinaendelezwa siku hadi siku. Hivi sasa mageziti na majarida mengi yanatumia lugha ya kimongolia, na shule za kabila letu zinawafundisha wanafunzi kwa lugha mbili za kihan na kimongolia. Hali hiyo inaonesha kuwa utamaduni wetu unaendelezwa vizuri."

    Wakati waandishi wetu wa habari walipowahoji wataalamu wengine wa Shirika la kitaifa la Utafiti wa Jiangger na Shirika la Oirats, walisema Bw. Batu ni msomi mwadilifu katika utafiti wa lugha, pia anaheshimu sana maoni tofauti ya watu wengine. Mfanyakazi wa Shirika la Oirats Bi Li Li alisema,

    "Nilijiunga na shirika hilo miaka miwili iliyopita. Bw. Batu anawatenda vizuri wafanyakazi wapya, na kutusaidia mara kwa mara katika maisha na kazi. Anafanya kazi kwa bidii na kupenda kuwasaidia watu wengine, yeye ni mfano mzuri wa kuigwa kwa sisi vijana."

    Bw. Batu anaona kuwa mustakabali wa maendeleo ya utamaduni wa kabila la Wamongolia hasa unategemea juhudi za mashirika mbalimbali ya utafiti. Alisema mashirika hayo yanaweza kuunganisha nguvu mbalimbali, na anawataka vijana wengi zaidi kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya utamaduni wa kimongolia kwa kupitia mashirika hayo. Alisema,

    "Hivi sasa nataka kuwasaidia vijana na kuwawezesha wafanye kazi nyingi zaidi za utafiti. Tunajitahidi kuhimiza utamaduni wa kabila la kimongolia uendelezwe zaidi kwa kupitia mashirika ya utafiti, kwa kuwa mashirika hayo yamekusanya wasomi wengi wanaoweza kufanya utafiti kuhusu mambo mbalimbali. Hivyo tukiendesha vizuri mashirika hayo, tutasukuma mbele utamaduni wa kimongolia mkoani Xinjiang. Aidha kutumia vizuri utamaduni bora wa makabila mengine katika kuendeleza utamaduni wa kabila letu pia ni jambo muhimu sana. Kwa mfano lugha ya kimongolia haitoshi katika kuendeleza utamaduni wa kabila la Wamongolia, mara kwa mara tunatafsiri matokeo ya utafiti wa utamaduni wetu kuwa lugha za makabila mengine hasa lugha ya kabila la Wahan, ili utafiti wetu upate nguvu mpya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako