• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Profesa Liu Hongwu aliyetoa mchango zaidi kwa ajili ya kuongeza urafiki kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2009-11-27 14:32:01

    Profesa Liu Hongwu alizaliwa mwaka 1958 katika mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China. Yeye amefanya utafiti kuhusu Afrika kwa miaka 20. Katika muda huo ameandika vitabu zaidi ya 10 kuhusu Afrika, ambavyo vimechapishwa. Vitabu hivyo vinahusu mambo mbalimbali na sehemu mbalimbali za Afrika, kama vile utamaduni wa nchi zilizo kusini mwa Sahara, utamaduni wa Kiswahili, historia ya maendeleo ya Nigeria, ushirikiano kati ya China na Afrika, na suala la Darfur. Kutokana na mafanikio yake katika utafiti kuhusu Afrika, yeye amekuwa ni mmoja kati ya wataalam maarufu zaidi wanaofanya utafiti kuhusu Afrika nchini China. Akiwa mtafiti wa suala la Afrika, Profesa Liu ametembelea nchi zaidi ya 20 barani Afrika, na kati ya nchi hizo, ya kwanza ilikuwa ni Nigeria. Alisema:

    "Mwaka 1990 nilikwenda Afrika kwa mara ya kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Lagos nchini Nigeria. Katika wakati ule watu wachache walipenda kwenda kusoma katika nchi za Afrika, lakini niliona kuwa Afrika ina vivutio vingi, kwa hiyo niliamua kwenda. Uamuzi huo ulihusiana sana na tabia yangu na maisha niliyoishi, kwa sababu niliishi katika sehemu ya Xinjiang, ninapenda mazingira ya asili, utamaduni na sanaa za makabila madogomadogo nchini China, nadhani Afrika ni sehemu ambapo mazingira yake ya asili, utamaduni na sanaa zake zinanivutia sana, tena napenda kufanya utafiti kuhusu Afrika, naona ni lazima niende Afrika."

    Baada ya kusoma kwa mwaka mmoja nchini Nigeria, Profesa Liu Hongwu alirudi nyumbani mwaka 1991, alianzisha somo la utafiti kuhusu Afrika katika Chuo Kikuu cha Yunnan, sababu aliona kuwa wakati ule utafiti kuhusu Afrika nchini China bado ulikuwa wa kidhaifu. Amesema:

    "Viongozi wa China wametaja hali hii mara nyingi. Kwenye mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, mjumbe wa taifa wa China Bw. Tang Jiaxuan alisema utafiti kuhusu Afrika nchini China uko nyuma, ni lazima utiliwe mkazo, na mjumbe huyo alitaja hali hiyo tena baada ya miaka miwili kwenye mkutano mwingine."

    Ili kuharakisha kazi ya utafiti kuhusu Afrika nchini China na kuandaa wataalamu wa taaluma hiyo, Profesa Liu alianzisha taasisi ya kwanza ya utafiti kuhusu Afrika nchini China katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang mwezi Septemba mwaka 2007 kutokana na uungaji mkono wa wizara ya mambo ya nje na wizara ya elimu ya China. Baada ya kuendelezwa kwa miaka miwili, taasisi hiyo imekuwa idara kubwa zaidi na maarufu zaidi nchini China ya utafiti kuhusu Afrika, ambayo ina watafiti zaidi ya 20, vituo vinne vya utafiti, maktaba ya vitabu kuhusu Afrika na Jumba la sanaa za Afrika.

    Baada ya kusoma vitabu vya Profesa Liu, wasomaji wengi wa China wameifahamu zaidi na kuipenda zaidi Afrika. Profesa Liu anaona kuwa ni wajibu wake kutafuta na kugundua mambo mazuri ya Afrika, na kuwafahamisha wachina kuhusu mambo hayo. Alisema:

    "nikiwa mchina, nimewawakilisha vijana wasomi wa China wa kizazi baada ya kizazi katika miaka 30 iliyopita, ambao wameshinda shida za aina mbalimbali, kushikilia kutafuta na kugundua mambo mazuri ya Afrika, thamani ya Afrika, na mchango uliotolewa na utamaduni wa Afrika kwa utamaduni wa dunia, na kuwafahamisha wachina wa kawaida ustaarabu na utamaduni wa Afrika, vivyo hivyo mawasiliano kati ya utamaduni wa China na Afrika yakaongezeka."

    Pro. Liu amesema hivi sasa wachina hawana ufahamu wa kutosha kuhusu Afrika, na watu wa Afrika pia hawana ufahamu wa kutosha kuhusu China, kwa hivyo sio tu China inapaswa kufanya utafiti zaidi kuhusu Afrika, Afrika pia inatakiwa kufanya utafiti kuhusu China. Amesema:

    "Tunatetea kuwawezesha wanafunzi wengi waafrika waje hapa China, sio tu wangesomea sayansi ya maumbile, bali pia wangesoma masomo ya utamaduni, kama vile utamaduni wa jadi wa China, ili waafrika wengi zaidi wawe na ufahamu kuhusu China, huo ndio ushirikiano katika utamaduni uliotajwa kwenye Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. Tunasema mara kwa mara kwamba uzoefu wa China wa kujiendeleza una maana ya kuigwa kwa Afrika, lakini hakuna mwafrika anayefanya utafiti kuhusu njia ya kujiendeleza ya China, kwa hivyo tunatetea kuwaandaa watu wenye ujuzi mwingi kuhusu China barani Afrika."

    Profesa Liu ametembelea nchi za Afrika mara nyingi, na kuwa na urafiki na watu wengi wa Afrika. Amesema China na Afrika zina historia ya kufundishana tangu miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, na ni lazima kuenzi desturi hiyo. Amesema:

    "Mara yangu ya kwanza kwenda Afrika ilikuwa ni kwa ajili ya kusoma katika chuo kikuu barani Afrika. Mwalimu wangu Profesa Na Zhong pia alisoma nchini Misri kwa miaka minane katika miaka ya 40 ya karne iliyopita, baada ya kurudi nyumbani alianzisha somo la lugha ya kiarabu katika vyuo vikuu nchini China, tunaweza kusema sisi sote ni wanafunzi wa waafrika, sisi wachina tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa waafrika. Kwa upande mwingine, Mtume Muhammad alisema 'hata ujuzi ukiwa mbali kama iliko China, tunapaswa kuutafuta'. Msafiri maarufu wa Morocco Bw. Ibn Battuta aliwahi kuja China kufanya uchunguzi, kwa hiyo katika miaka zaidi ya elfu moja iliyopita, wachina na waafrika wamekuwa wanafundishana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako