• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2009-12-08 17:45:04

    Baada ya kutangazwa kwa vipindi vya Tamasha la utamaduni la Lamu, wasikilizaji wetu wengi nchini Kenya wametutumia ujumbe mfupi kwa kupitia simu wakitoa maoni yao.

    Msikilizaji Johnston Ambale, wa Mombasa anasema kipindi kilikuwa cha kuvutia kwani kilieleza kwa kina jinsi Punda anathaminiwa katika kisiwa cha Lamu. Mtangazaji alieleza kwa msisimko mkubwa sana na kutuwezesha kutaka kujua mengi zaidi kuhusu Lamu na maeneo mengine. Ningependa Radio China kimataifa itembelee maeneo mengine ambayo yatasaidia kuelezea uzuri wa taifa la Kenya.

    Msikilizaji mwingine Odengo Dorris wa Kajiado anasema kwa kweli kipindi kilikuwa ni cha kusisimua sana. Lakini anasema ingekuwa bora kama tungetembelea maeneo ya Kajiado kujua utamaduni wa jamii ya wamasai na kulinganisha na ule wa China. Amesema amefurahia sana msururu huo wa safari ya mwandishi kisiwani Lamu.

    Msikilizaji Richard Likhakhasi wa Khayega, kwanza kabisa anasema sauti iliyotumiwa ilikuwa tamu sana na mada ya kusomwa kwa shairi pia ilivutia sana. Hata hivyo huko Khayega kuna crying stone, yaani jiwe linalolia na jingine lililo na alama za wayo. Kuna watu ambao wanaamini kuwa alama hiyo ni ya mungu na kila wiki watu hutembelea eneo hilo kufanya maombi. Anatuhimiza watu tufanye hima kuujulisha ulimwengu kuhusu maajabu haya, na anawapongeza watangazaji Mogoa na Zakia, anasema hongera tena sana.

    Msikilizaji Moses Mogaka, akiwa Nairobi yeye anasema alifurahia sana kusikia kipindi kinachoeleza uzuri wa mandhari ya Kenya. Anaona kuwa Radio China Kimataifa inastahili pongezi na iendelee na moyo huo huo. Alifurahia jinsi shairi lilivyoimbwa, na bado anasubiri sehemu ya mwisho ya safari ya waandishi wetu kisiwani Lamu.

    Msikilizaji wetu mwingine wa Nairobi, Bi Diana Mjeni anasema hongera Radio China Kimataifa kwa makala mazuri kuhusu Lamu. Kilichomfurahisha zaidi ni jinsi utamaduni unavyodumishwa bila kuchanganywa na vitu vya kigeni. Anasema hakujua kuhusu uhusiano uliopo kati ya baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho na Lamu. Anasema anaomba tuendelee na kazi nzuri na moyo huo huo.

    Mwalimu Kofa wa Lamu, yeye anasema ama kweli hadi leo anazidi kukumbuka kipindi cha kwanza kuhusu umuhimu wa Punda kisiwani Lamu. Vituo vingi vya habari vimekuwa vikizungumzia sana utamaduni pekee, lakini mwandishi ameeleza kwa undani kuhusu Punda na kunasa taswira ya mji wa Lamu. Anamaliza kwa kusema Radio China hoyeeee!

    Gabriel Agoro Simba akiwa Kisumu anasema, Kisumu pia kuna mambo mazuri kwa hiyo anaomba waandishi wetu wa habari watembelee huko. Huko kuna ziwa Victoria na jinsi linavyowawezesha wakazi kujikimu kimaisha. Anasema tafadhari tusikose kutembelea mji wa Kisumu na kujionea jinsi wajaluo wanavyohifadhi utamaduni wao pamoja na biashara inavyonoga katika ziwa Victoria. Hata hivyo anasema kipindi cha Lamu kilivutia wasikilizaji wengi sana huko Kisumu.

    Samson Amukubwa akiwa Nairobi anasema amefurahishwa sana kwa hajawahi kusikiliza kipindi kinachoeleza uzuri wa maeneo huko nchini Kenya kama safari ya mwandishi kisiwani Lamu ilivyoeleza. Hivyo ndivyo wasikilizaji kama yeye wanavyopenda na watazidi kusikiliza Radio China kimataifa. Anasema hongera Mogoa na Zakia kwa kazi hiyo nzuri.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako