Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao anayehudhuria mkutano wa viongozi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, tarehe 17 alikutana na rais Mohammed Nasheed wa Maldives, waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Meles Zenawi, waziri mkuu wa Bangladesh Bibi Sheikh Hasina Wajed, waziri mkuu wa Grenada Bw. Tillman Thomas na msaidizi wa rais wa Sudan Bw. Nafie Ali Nafie.
Bw. Wen Jiabao alisema China na nchi zilizokuwa nyuma kimaendeleo, nchi za visiwa, na nchi za Afrika zote ni nchi zinazoendelea, ambazo zinaathiriwa vibaya na mabadiliko ya hali ya hewa, na zina maslahi ya pamoja katika kukabiliana na changamoto hiyo ya kimataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |