• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziwa Qinghai

    (GMT+08:00) 2009-12-28 17:01:50

     

    Ziwa Qinghai ni sehemu yenye mandhari nzuri ya ngazi ya 4A ya taifa, liko kwenye sehemu iliyoinama, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Qinghai, umbali wa kilomita 151 kutoka Xining, mji mkuu wa mkoa wa Qinghai, watu wanaweza kufika huko kwa kutumia barabara NO. 109 ya ngazi ya taifa au kwa gari-moshi. Ziwa Qinghai ni ziwa la kwanza kwa ukubwa kwenye sehemu ya ardhi ya China, vilevile ni ziwa la kwanza kwa ukubwa lenye maji ya chumvi nchini China. Ziwa hilo likiwa na sifa ya "ziwa zuri kabisa la China" limewekwa katika "orodha ya ardhi oevu muhimu ya dunia", na limejiunga na "mapatano ya radhi oevu muhimu ya dunia kwa ndege wa majini". Sehemu hii inafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, na ni moja ya sehemu maalumu ya utalii mkoani Qinghai.

    Jina la Ziwa Qinghai katika lugha ya Kitibet ni "Cuowenbo" na ni "Kukuzhuoer" katika lugha ya Kimongolia, yote yakiwa na maana ya "bahari ya buluu". Mwongoza watalii wa huko Li Yucai alisema, kwa kuwa zamani wakazi wa huko walikuwa hawajawahi kuona bahari, walidhani kuwa Ziwa Qinghai ni ziwa kubwa kama bahari, hivyo wakaliita "bahari ya magharibi". Alisema,

    "Ziwa Qinghai lilisifiwa kuwa ziwa zuri kabisa katika China, na linachukua nafasi ya kwanza kati ya maziwa makubwa nchini China, na ni ziwa kubwa kabisa lenye maji ya chumvi nchini China, kwa kuwa ziwa hilo liko kwenye sehemu iliyoinama, hivyo maji yanapoingia kwenye ziwa hilo hayaendi mahali pengine tena. Eneo la ziwa hilo ni kilomita 4,500 za mraba, urefu wa kutoka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi ni kilomita 106, na ni kilomita 63 kutoka upande wa kusini hadi upande wa kaskazini. Ziwa hilo limezungukwa na milima, mzingo wa ziwa hilo ni kilomita 360, wastani wa kina chake ni mita 19, na sehemu yenye kina kirefu zaidi ni mita 39."

    Ziwa Qinghai liko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet, kwenye kando zake kuna mbuga tambarare, hali ya hewa ya huko si baridi wala joto, na ni sehemu nzuri kwa malisho ya mifugo. Mtu akisimama kwenye kando ya ziwa hili na kutizama mbali, ataweza kuona kuwa ziwa limezungukwa na milima, maji ya ziwa ni maangavu, na kwenye kando zake kuna malisho yenye majani mazuri, ambapo kuna makundi mengi ya kondoo jinsi ilivyo ni kama mawingu meupe kwenye anga. Kwenye upeo wa macho, maji ya ziwa kama yameungana na mbingu, vivuli vya milima yenye theluji vinaonekana kwenye maji ya ziwa, ambapo unaweza kuona samaki wakiogelea, na ndege wanaruka na kuzunguka kwenye ziwa.

    Kwa kuwa maji ya ziwa yenye kina tofauti pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa katika majira mbalimbali, hivyo rangi ya maji ya ziwa yanabadilika asubuhi, mchana na jioni katika siku moja, mwongoza watalii Li Yucai alisema,

    "wakatai wa hali ya hewa ya kawaida, maji ya ziwa yanakuwa na rangi 7, kwa hiyo wakazi wa kabila la Watibet wa eneo hili wanaliita kuwa ni ziwa lenye rangi 7, na ni ziwa takatifu. Mwezi Julai kila mwaka mandhari ya Ziwa Qinghai ni nzuri zaidi, katika wakati huu mimea ya rapa inachanua maua kwenye eneo kubwa, anga inaonekana kuwa ya buluu, mawingu yanakuwa meupe na maua ya rapa ya rangi ya manjano yanapendeza sana."

    Mandhari ya sehemu ya Ziwa Qinghai ni tofauti sana katika majira mbalimbali. Katika majira ya joto na majira ya mpukutiko wa majani, milima na mbuga zinapokuwa na rangi ya kijani, mandhari ya sehemu ya Ziwa Qinghai inapendeza sana, maji ya ziwa ni maangavu na hali ya hewa pia ni nzuri sana. Mbuga kubwa inaonekana kama imetandikwa zulia kubwa la rangi ya kijani, maua ya mwitu ya rangi mbalimbali yanachanua vizuri, hali hii inafanya mbuga ya rangi ya kijani ipendeze zaidi, makundi mengi ya mifugo yanaenea kwenye mbuga ya malisho; mashamba ya ngano na mimea ya rapa inayochanua maua ya rangi ya manjano na kutoa harufu ya kunukia; maji ya ziwa yanaonekana yameungana na anga ya buluu. Katika majira ya baridi, majani ya miti ya milimani na majani yaliyoko kwenye mbuga yanakauka na kuwa ya rangi manjano iliyochujuka, na wakati theluji inapoanguka sehemu yote inaonekana nyeupe. Maji ya Ziwa Qinghai yanaanza kuganda kuwa barafu, ziwa kubwa linaonekana kama kioo kikubwa, na linaangaza macho katika mwanga wa jua.

    Majira ya joto ni majira mazuri zaidi kwa watalii, Bw Wang Feng kutoka mkoa wa Shanxi alisema, ni tarajio lake la siku nyingi kulitembelea Ziwa Qinghai, alisema,

    "Nilisikia kuwa hapa Qinghai kuna mandhari nzuri sana, kuna ziwa zuri la Qinghai na hekalu la Taer, nimefurahi baada ya kufika hapa na nimeburudika sana, anga ni ya buluu, ziwa lina maji maangavu, milima yenye miti ya rangi ya kijani, baada ya kuona yote hayo nimefurahi zaidi. Wakazi wa sehemu ya Qinghai ni wachangamfu sana, vilevile ninaona kuwa mazingira ya hapa ni safi sana na yanapendeza kweli, wenyeji ni wakarimu, mandhari inanivutia, hewa ni safi mno, kweli ni mahali pazuri kutalii na kuishi."

    Kwenye Ziwa Qinghai, kuna visiwa vitano ambavyo vinaonekana kama ni mashua tano zenye maumbo mbalimbali. Kati ya visiwa hivyo kisiwa maarufu zaidi ni kisiwa cha ndege, kisiwa hicho kina eneo la kilomita za mraba 0.5, katika majira ya Spring na majira ya joto kuna ndege zaidi ya laki moja wanaoishi hapa, hali ya huko inapendeza zaidi wakati wanaporuka kwa pamoja.

    Ziwa Qinghai licha ya kuwa ni mahali pazuri kwa ajili ya utalii, vilevile ni ziwa lenye rasilimali kubwa linalofuatiliwa na wanasayansi duniani. Serikali ya China iliwahi kutuma watu kufanya uchunguzi mara kadhaa, na waligundua kuwa kuna rasilimali nyingi za madini. Tena ziwa hilo lina samaki wengi aina ya Huang, na linaonekana kama ni ghala kubwa la samaki la wakazi wanaoishi kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya China.

    Wakazi wanaoishi kwenye sehemu hii ni pamoja na watu wa makabila ya Wahan, Watibet na Wamongolia, ambao wanaishi pamoja kwa masikilizano, wanahifadhi na kuendeleza pamoja ziwa hilo lenye utajiri mwingi. Mandhari nzuri ya Ziwa Qinghai inavutia maelfu kwa mia ya watalii wa nchini na wa nchi za nje. Ili kuendeleza shughuli za utalii zinazostawi hivi sasa kwenye uwanda wa juu, idara ya utalii ya mkoa wa Qinghai imejenga vituo vya utalii, ambapo watalii wanaofika huko licha ya kuweza kujiburudisha kwa mandhari nzuri ya sehemu ya malisho ya uwanda wa juu, vilevile wanaweza kufanya matembezi kwenye mbuga kwa kupanda farasi na ng'ombe wa aina ya Tibet, au kutembelea kwenye kambi za watu wanaochunga mifugo mbugani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako