• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha ya Bw. Yunus wa kabila la Wauyghur katika mwaka 2009

    (GMT+08:00) 2010-01-07 15:00:07
    Bw. Yunus mwenye umri wa miaka 33 ni mkurugenzi wa ofisi inayoshughulikia mambo ya mtaa wa wakazi wa Heijiashan ya serikali ya mji wa Urumuqi ulioko katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur. Kwa Bw. Yunus mwaka 2009 uliomalizika hivi karibuni ni mwaka utakaomwachia kumbukumbu kubwa. Kwani ingawa amekuwa ofisa wa mtaa huo kwa miaka 8, lakini mambo yaliyotokea mwaka 2009 yanamfanya ajivunia sana kuhusu mshikamano kati ya watu wa makabila totauti.

    Katika mtaa wa Heijiashan, kuna wakazi zaidi ya 8,900 kutoka makabila 10 yakiwemo Wauyghur, Wahan, Wahui na Wakazakh. Kila asubuhi, Bw. Yunus anaanza kazi zake mapema, na kazi yake ya kwanza ni kuwapokea wakazi wanaokwenda kwake kuomba msaada.

    Siku hiyo mkazi aliyemwendea Bw. Yunus anaitwa Pu Hongyuan. Mzee huyo wa kabila la Wahan ana umri wa miaka 71, na mke wake anatoka kabila la Wauyghur. Walikuwa wakizozana kuhusu jambo fulani la kawaida, hivyo walimwendea Bw. Yunus ili awasuluhishe. Bw. Yunus alimshawishi Bw. Pu Hongyuan kuthamini masikilizano ya familia, na kutoa njia ya kumaliza mzozo kati yao. Baada ya usuluhishi wa Bw. Yunus, hasira ya Bw. Pu Hongyuan ilitoweka kabisa. Alisema,

    "Huyu ni mtu mwema. Kila ninapokutana naye ananiuliza kuhusu mambo ya familia yangu yanavyokwenda. Aidha anakuja nyumbani kwangu mara kwa mara, na kunipa misaada mingi."

    Bw. Yunus alizaliwa katika sehemu ya Kashi iliyoko kusini mwa mkoa wa Xinjiang. Baada ya kuhitimu masomo katika chuo kikuu mwaka 1999, alifaulu mtihani wa kuchagua watumishi wa serikali, na akawa ofisa wa serikali ya mji wa Urumuqi, na kuanza kufanya kazi katika ofisi ya serikali katika mtaa wa wakazi wa Heijiashan. Bw. Yunus alisema,

    "Wakati huo, sikujua kuwa nitafanya kazi gani. Kiongozi wangu aliniambia kuwa kazi ya ofisi yetu ni kutoa huduma kwa wakazi wa mtaa wa Heijiashan, na kutoa misaada mbalimbali kwa watu kutoka makabila mbalimbali kwa niaba ya serikali. Nilimjibu kuwa serikali ilinipa elimu ya juu, na kuniandaa kuwa ofisa wa serikali kutoka mtoto wa mkulima, hivyo wajibu wangu ni kuwahudumia watu wa makabila mbalimbali."

    Bw. Zeng Ying mwenye umri wa miaka 68 anatoka kabila la Wahan, na ameishi katika mtaa wa Heijiashan kwa zaidi ya miaka 30. Zamani alikuwa mfanyabiashara mdogo, lakini sasa amezeeka na hawezi kujitegemea. Kwa bahati mbaya, mke wake hana afya njema, na mtoto wake mmoja ni mlemavu. Hivyo familia ya Bw. Zeng Ying inaishi maisha magumu. Baada ya kujua hali hii, Bw. Yunus aliisaidia familia hiyo kupata ruzuku inayotolewa na serikali kwa wakazi wa mijini wenye matatizo ya kiuchumi. Hivi sasa familia ya Bw. Zeng Ying inapewa msaada wa fedha kutoka serikalini, haina wasiwasi tena juu ya maisha. Bw. Zeng Ying alisema,

    "Baada ya kujua kuwa familia yangu ina matatizo ya kiuchumi, Bw. Yunus anatembelea nyumbani kwangu mara kwa mara. Mbali ya kutuletea misaada mbalimbali, pia anatusaidia kusafisha nyumba. Ninamshukuru sana."

    Tarehe 5 mwezi Julai mwaka huu, wafarakanisha walizusha tukio la kimabavu mjini Urumuqi. Ili kulinda usalama wa familia ya Bw. Zeng Ying wa kabila la Wahan, Bw. Yunus aliwataka wajifiche katika ofisi yake. Lakini Bw. Zeng Ying alikataa akiwa na tabasamu. Alisema anaishi pamoja na wakazi wa makabila mengine kwa mshikamano, wao wote watamlinda, na alisema wahalifu wachache hawataweza kutishia usalama wake.

    Kutokana na tukio la tarehe 5, Julai, mtaa wa Heijiashan ulikumbwa na hasara kubwa, ambapo shughuli za uzalishaji, na maisha yaliathiriwa vibaya, na wakazi wa mtaa huo walidhuriwa kiroho . Ili kuhakikisha usalama na utulivu wa mtaa huo, Bw. Yunus aliongeza nguvu ya kufanya doria wakati wa usiku. Mchana alitembelea familia za wakazi ili kueneza sera ya serikali kuu kuhusu mambo ya makabila madogo madogo na kutuliza moyo wa watu, na usiku aliongoza watu wa kulinda usalama kufanya doria.

    Bw. Yunus alisema mkoa wa Xinjiang ni kama familia kubwa ya watu kutoka makabila mbalimbali wanaoishi pamoja kwa mshikamano. Hivi sasa utulivu na usalama mkoani Xinjiang umerudi, na watu wote wamerejea maisha ya kawaida. Wakazi wote wa mtaa wa Heijiashan akiwemo Bw. Zeng Ying waliridhika sana na kazi ya Bw. Yunus katika tukio hilo. Bw. Zeng Ying alisema,

    "Wakati wa tukio la tarehe 5, Julai, Bw. Yunus alifikiria sana usalama wa familia yangu. Ninamshukuru sana kwa wema wake."

    Katika majira ya baridi ya mwaka huu, mji wa Urumuqi umekuwa na baridi ya mzizimo zaidi kuliko zamani. Bw. Yunus alitembelea familia zote za mtaa wa Heijiashan ili kuona kama wana matatizo yoyote.

    "Kazi zangu ni za aina mbalimbali. Lakini huu ni wajibu wangu, ni lazima nizifanye vizuri."

    Bw. Yunus anajishughulisha vizuri na kazi hizo za mtaa wa wakazi, lakini jambo linalojulikana na watu wachache sana ni kuwa ana mzigo mzito wa familia. Mke wa Bw. Yunus hana kazi, na mtoto wao ana umri wa mwaka mmoja tu, maisha ya familia yake yanategemea mshahara wa Bw. Yunus tu. Mbali na hayo, mara kwa mara analipa matibabu kwa ajili ya wazazi wake wasio na afya njema. Hata hivyo Bw. Yunus anapenda sana kuwasaidia watu wengine wenye matatizo ya kiuchumi. Katika miaka 8 iliyopita tangu aanze kazi katika mtaa wa Heijiashan, amechangia fedha nyingi kwa wakazi wa mtaa huo.

    Baada ya tukio la tarehe 5, Julai la Urumuqi, baadhi ya watu walidhani kuwa tukio hilo lingeweza kusababisha kutoelewana kati ya watu wa makabila tofauti mkoani Xinjiang. Lakini Bw. Yunus anaona kuwa watu wa makabila mbalimbali mkoani humo wameishi na kufanya kazi kwa pamoja kwa miaka mingi, hivyo hawawezi kutengana. Alisema,

    "Katika siku za baadaye nitafanya kazi kwa bidii zaidi, ili kujenga mtaa wetu kuwa familia kubwa ya watu kutoka makabila tofauti wenye mshikamano. Nina imani kuwa tutakuwa na mustakabali mzuri zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako