• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utalii kuhusu mambo ya utamaduni katika mji mdogo wa Macau

    (GMT+08:00) 2010-01-11 16:56:16

    Ingawa mji wa Macau una eneo dogo, lakini una vitu vingi vyenye maana isiyo ya kawaida, hususan umaalumu wake wa maingiliano ya utamaduni wa aina nyingi unawapa watu kumbukumbu nyingi. Hayo ni maoni ya pamoja ya watu wengi waliowahi kufika Macau au wanaoifahamu vizuri Macau.

    Baada ya kufika katika mkoa wa utawala maalumu wa Macau, na kuingia kwenye mtaa wa mji wa kale kwa kufuata njia ya mawe, watu wanaweza kuona kanisa lenye mtindo wa kimagharibi, hekalu lenye mtindo wa kichina, muziki wa opera ya Guangdong inasikika kichochoroni, na kusikia harufu nzuri ya vitoweo vya kiguangdong, watu wanajisikia kama wameingia katika zama za kale zenye utamaduni tofauti. "Unaooneshwa kwenye upande wa kulia ni ustaarabu wa kichina, na unaooneshwa kwenye upande wa kushoto ni ustaarabu wa magharibi ikiwa ni pamoja na maandishi, fikra ya falsafa, dini, sayansi na teknolojia……."

    Mkuu wa jumba la makumbusho la Macau Bw Chen Yingxian alisema, Macau ni kama ujia unaoonesha maingiliano ya ustaarabu wa mashariki na wa magharibi: maneno yaliyochongwa kwenye magamba ya kobe na herufi za maneno ya kimagharibi, sanamu za askari na merikebu za Ureno za karne ya kati, fikra ya Laozi na falsafa ya Aristotle, ambavyo vinaoneshwa kwa mbalimbali kwenye pande mbili, vyote ni vivutio vya Macau kuhusu maingiliano ya utamaduni wa kichina na kimagharibi.

    Mbali na utamaduni, katika jumba la makumbusho watu wanaweza kuona sura ya jadi na utamaduni wa wakazi wa sehemu ya kusini mwa China, na ufahari wa makampuni ya wafanyabiashara wa kimataifa. Katika jumba la makumbusho kuna "mtaa wa Macau", nyumba za wakazi zenye umaalumu wa milango midogo na mapaa yaliyoezekwa kwa vigae vya rangi ya kijivu iliyokolea, na nyumba za wakazi zenye mtindo wa kireno za rangi ya manjano na buluu nyepesi, sauti za wachuuzi za kuita watu zinasikika kwenye mtaa wa Macau.

    Baada ya kutoka katika jumba la makumbusho, watu wanaona kuwa jumba la makumbusho la Macau liko ndani ya msingi wa jukwaa lenye mizinga. Jukwaa hili la mizinga likiwa pamoja na viwanja vinane na majengo 22 ya kihistoria ya lango kubwa la mawe la Dasanba, Kanisa la mama mwenye rozari, kiwanja cha mbele cha jengo, hekalu la Nezha, jengo kubwa la ukoo wa Lu, jengo kubwa la idara ya bandari na hekalu la Mage, vimekuwa majengo muhimu kwenye "sehemu ya mji wa kihistoria wa Macau".

    Mwezi Julai mwaka 2005, mkutano wa 29 wa kamati ya urithi wa utamaduni wa dunia ya Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa iliichagua sehemu ya mji wa kihistoria wa Macau" kuwa urithi wa utamaduni wa dunia ya 31 na kuiweka katika "orodha ya urithi wa dunia". Mkurugenzi wa idara ya utalii ya serikali ya Macau Bw An Dongliang alisema, "Urithi huu ni mabaki ya maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za magharibi ya miaka zaidi ya 400 iliyopita ya Macau yetu, ambao unaonesha umaalumu wa mji wetu."

    Mabaki ya utamaduni ya Macau yamekuwa vivutio kwa watalii. Majengo hayo ya kale ya mitindo ya kichina na ya kimagharibi yenye mazingira ya kihistoria na umaalumu tofauti, yanaonesha mtindo maalumu na vitu halisi kuhusu utamaduni wa Macau. Kutokana na majengo hayo yenye mchanganyiko wa mtindo wa Ulaya ya kusini na mtindo wa mashariki, watalii wanaweza kuona mgongano na mfanano wa mawazo, dini, biashara na mila na jadi ya kichina na kimagharibi wa miaka 400 iliyopita. Kwenye ardhi hiyo ndogo kuna aina nyingi za utamaduni na historia, ambazo hatimaye zinaingiliana na kupata maendeleo kwa pamoja, hii kabisa ni hali maalumu katika utamaduni.

    Kabla ya kurudi China, Macau haikuzingatia sana umuhimu wa utamaduni wake wa aina nyingi. Baada ya sehemu ya mji yenye historia ndefu ya Macau kuwekwa katika orodha ya urithi wa utamaduni wa dunia, wakazi wengi wa Macau walianza kutambua thamani ya mji huu wanaoishi. Bi He Lizuan wa idara ya utamaduni ya Macau alikuwa na hali kama hiyo, aliposoma katika shule ya Macau alitumia vitabu vya Hong Kong, ambavyo vinawafanya wakazi wengi wa Macau kutofahamu vizuri utamaduni wa China na Macau, kwa hiyo anaona maana ya kuomba kuiweka sehemu hiyo katika orodha ya urithi wa utamaduni wa dunia, na kuanzishwa shughuli nyingine za kiutamaduni imezidi wigo wa shughuli hizo zenyewe za kiutamaduni.

    Bi He Lizuan anafurahi sana kuweza kufanya kazi katika idara ya utamaduni baada ya Macau kurudi China, kwani uwekezaji wa serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Macau unawawezesha kufanya kazi bila vipingamizi, na wote wanafurahia maendeleo ya kazi zao. Bi He alisema "Kama tukisema kwa maneno machache kuhusu miaka kumi tangu Macau irudi China, tunaweza kusema tumehifadhi urithi mkubwa wa utamaduni wa dunia, tumejenga vituo viwili vya utamaduni vya kuhudumia Macau: kimoja ni kituo cha kuandaa wachezaji na wachezaji wa michezo ya sanaa cha Macau, yaani chuo cha michezo ya sanaa cha Macau, na kingine ni jumba la makumbusho la Macau; licha ya hayo tumeanzisha shughuli za tamasha ya muziki ya Macau, tamasha la michezo ya sanaa ya Macau, bendi ya Macau na bendi ya muziki wa kichina ya Macau."

    Macau ikiwa kama ni sehemu ya maingiliano ya utamaduni wa kichina na kimagharibi, watalii wanaoitembelea wanajionea kabisa vivutio vya kiutamaduni vya Macau. Katika tamasha la muziki wa Macau, watalii wanaweza kuburudishwa na maonesho ya wasanii wa Macau na waliotoka sehemu m mbalimbali nchini China na sehemu mbalimbali za dunia, wanamuziki wakishirikiana na wanamuziki wa sehemu mbalimbali za dunia, wanaonesha michezo ya opera, Simfoni, opera ya Beijing, opera ya Huagu ya mkoa wa Hunan, mchezo wa wanasesere wa mkoa wa Fujian, opera ya Bangzi ya mkoa wa Hebei, nyimbo za kienyeji na michezo ya kuigiza ya lugha ya Kireno ya Macau, kila mwaka inaoneshwa michezo kumi kadhaa, na katika bendi maalumu za Macau kuna wanamuziki na wawongozaji wa bendi na waimbaji kutoka sehemu mbalimbali nchini China.

    Hivi leo tamaduni za aina mbalimbali zinaonesha mivuto yao huko Macau, shughuli za maonesho za mwaka 2009 zilizotangazwa na idara ya utalii ya Macau zinaonesha kuwa, mbali na tamasha la michezo ya sanaa la Macau na tamasha la muziki la kimataifa la Macau, kuna shughuli nyingine nyingi za siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa ardhi, maonesho ya michoro ya Yesu mtakatifu, sikukuu ya Qingming, sikukuu ya Pasaka, siku ya kuzaliwa Budha, tamasha la utamaduni wa Mazu, tamasha la maua ya yungiyungi, maonesho ya michoro ya Madonna, siku ya kuzaliwa ya Guandi, Siku ya kuwaombea marehemu, sikukuu ya Chongyang, Tamasha la kireno, mbio za magari za Grand Prix, yote hayo yanaonesha umaalumu wa utamaduni wa aina nyingi.

    Mwanafunzi Xiao Men kutoka Macau anayesoma katika chuo kikuu cha mawasiliano ya habari cha China alisema kutokana na anavyoona, utamaduni wa aina nyingi wa Macau utakuwa kivutio kikubwa zaidi kwa watalii. Alisema

    "Mimi ni mwanafunzi wa kitivo cha mawasiliano ya muziki, lakini kitu ninachokipenda zaidi ni mawasiliano ya utamaduni. Utamaduni wa Macau unapendeza sana, na tunapaswa kuutambulisha kwa watu."

    Xiao Men alisema, nia yake ni kubadilisha wazo la makosa la watu kuhusu Macau kutokana na mawasiliano ya utamaduni, katika mji huo licha ya kuweko kwa shughuli za kasino, pia kuna dunia nyingine ya utamaduni murua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako