• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msanii Mashuhuri Bw. Jin Lisheng wa mchezo wa sanaa wa Pingtan

    (GMT+08:00) 2010-01-11 16:54:05

    Pingtan ni aina ya usanii wa kusimulia hadithi kwa kuimba na kuongea kwa lahaja ya mji wa Suzhou, usanii huu umeenea katika mikoa ya Jiangsu na Zhejiang, kusini mwa China. Usanii huo umewekwa na serikali katika orodha ya urithi wa utamaduni usioonekana wa China. Bw. Jin Lisheng ni msanii mkubwa wa mchezo huo, na michezo iliyoonesha uwezo wake mkubwa ni "Kesi ya Mapenzi kati ya Bw. Yang Naiwu na Bi. Xiao Baicai" na "Bw. Yang Silang aonana na Mama Yake" , Bw. Jin Lisheng alipata tuzo kubwa ya taifa, Mwaka 2006 bwana huyo alipokuwa na umri wa miaka 63 alichaguliwa na serikali kuwa ni mrithi wa mchezo wa sanaa ya Pingtan wa utamaduni usioonekana wa China.

    Mliosikia ni mchezo alioimba Bw. Jin Lisheng unaoitwa "Kesi ya Mapenzi kati ya Bw. Yang Naiwu na Bi. Xiao Baicai". Hadi sasa Bw. Jin Lisheng amefanya maonesho jukwaani kwa zaidi ya miaka 40. Alipokumbusha jinsi alivyojifunza usanii huo alisema:

    "Katika miaka nilipokuwa najifunza usanii wa mchezo huo kulikuwa hakuna kitabu cha kufundishia, nilijifunza kwa kumsikiliza tu mwalimu wangu, kama kuna sehemu sikuelewa nilimwomba mwalimu arudie tena. Hadithi inayosimuliwa ni ndefu ambayo huwa na milango 30 hivi, inanipasa nihifadhi na kuieleza kwa kuimba, ugumu ulikuwa mkubwa."

    Mwaka 2000 maonesho yake ya mchezo unaoitwa "Bw. Yang Silang aonana na Mama Yake" yalipata tuzo ya taifa. Bw. Jin Lisheng ameanza kuwafundisha vijana, ili arithishe kizazi kingine mchezo huo. Moja kati ya majukumu yake ni kuwafundisha vijana mchezo unaoitwa "Kesi ya Mapenzi kati ya Bw. Yang Naiwu na Bi. Xiao Baicai" ambao unaonesha uwezo wake mkubwa wa usanii, na ugumu wa kufundisha mchezo huo ni zaidi ya ugumu aliopata wakati alipojifunza. Alisema,

      "Jukumu langu ni kufundisha mambo mawili, moja ni kufundisha hadithi yenyewe, nyingine ni kiwango cha usanii kinachotakiwa ili nisipokuwa hapa duniani mchezo huo wa sanaa uendelee kuwepo bila kupungua kwa kiwango cha usanii."

      Hivi leo kutokana na kuwepo kwa wasanii wazee kama Bw. Jin Lisheng, usanii wa Pintan wenye historia ndefu ambao ni "hazina ya taifa la China" unaendelea kuota mizizi nchini China. Mkuu wa kundi la mchezo wa sanaa ya Pingtan la mji wa Suzhou Bw. Sun Ti alisema,

    "Kwa kuwa ana uzoefu mkubwa aliopata kwenye maonesho aliyofanya jukwaani katika miongo kadhaa, majukumu yake ya kufundisha ni makubwa."

    Ni sawa kama michezo mingine ya sanaa ilivyo, mchezo wa Pingtan pia unarithishwa kwa kufundishwa uso kwa uso. Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo vijana wanaopenda michezo ya sanaa ya jadi wanavyopungua, hali kadhalika kwa mchezo wa sanaa wa Pingtan. Kwa hiyo hatua ya kwanza ya kutatua tatizo hilo ni kuwavutia vijana wapende mchezo huo wa sanaa. Katika muda wa miaka minane iliyopita Bw. Jin Lisheng alifanya mihadhara mingi katika vyuo vikuu ili kuwaelimisha vijana kuhusu mchezo huo wa sanaa wenye historia ya miaka mingi. Alisema,

     "Wanafunzi waliosikiliza mihadhara yangu wanatoka sehemu mbalimbali, kupitia mihadhara na maonesho ninayofanya, nawavutia na nikifikiri pengine baadaye kati yao kutakuwa na watakaofanya utafiti kuhusu mchezo huo wa sanaa na kuuendeleza zaidi."

      Xiao Su ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Suzhou aliyetoka sehemu ya kaskazini magharibi mwa China, mchezo wa sanaa wa Pingtan ni kigeni kabisa kwake. Mwezi Machi mwaka huu alishiriki kwenye mhadhara ndipo alipoelewa usanii wa mchezo huo. Alisema,

      "Nilitoka sehemu ya mbali na Suzhou, kwangu ni mara ya kwanza kusikiliza mhadhara kuhusu mchezo wa sanaa wa Pingtan, ingawa siufahamu sana mchezo huo wa sanaa, lakini mvuto wa fasihi yake unanivutia mimi mwanafunzi wa chuo cha fasihi."

      Hivi sasa Bw. Jin Lisheng ametimiza miaka 66, anatumia kila wakati kuratibu michezo ya sanaa aliyowahi kufanya maonesho, mpaka sasa amefundisha wanafunzi 11, lakini walimu wanaofundisha mchezo huo wa sanaa wako wawili tu, akiwa na matumaini kuwa watu wengi wataupenda mchezo huo wa sanaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako